Tuesday, 15 January 2013

Nusu ukuwadi umtokee Mbatia puani

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi  James Mbatia alinusirika kipigo kutokana na kuingia kichwa kichwa kwenye sakata la gesi Mtwara. Akiwa Mtwara Mbatia aliyeandamana na wabunge wake toka Kasulu alisema maneno ambayo hayakuwafurahisha wadau wa sakata la gesi kuhamishiwa Dar Es Salaam. Kikubwa kilichomponza ni ile hali ya kuteuliwa na Jakaya Kikwete kuwa mbunge. Hivyo kwa akina njomba Mbatia si mtu wa kuweza kupingana na mtu aliyempa ulaji yaani Kikwete ambaye anaonekana kutaka miundombinu ya kusafirisha gesi iwekwe Dar na Bagamoyo kwa faida zake binafsi. Kwa habari zaidi GONGA hapa.

No comments: