Thursday, 24 January 2013

Jakaya na mpira Jakaya na mpira!

Mambo mengine yanatia kichefuchefu ingawa kuna wanaoyaona kama ufanisi. Rais Jakaya Kikwete ni mpenzi wa mpira wa miguu. Hili halina ubishi. Pamoja na upenzi huo bado ni rais wa Tanzania. Tunadhani mambo ya michezo angemwachia waziri mhusika sawa na mambo ya nje. Yeye anapaswa kufanya kazi ya urais na si michezo. Wengi walitegemea kumuona na gavana wa benki inayosemekana imetunza pesa za ujambazi zilizofichwa huko nje. Lakini hana muda na hilo kwa vile siyo kipaumbele cha serikali yake wala halina faida kwa Tanzania. Ni balaa kuwa na rais wa namna hii. Kikwete awe somo kwa wanaokuja na udhaifu wake usaidie kurekebisha katiba yetu na kumpa madaraka kiasi rais ajaye ili kuwa na namna ya kumbana na kumsaidia hasa anapotokea kuwa mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri.

1 comment:

Jaribu said...

Jamaa ni kilaza, tusitegemee mambo makubwa kutoka kwake. Swali ni kwamba ilikuwaje mtu wa upeo kama wake afaulu kuwa Rais wa Jamhuri?