Wednesday, 16 January 2013

Rais Salma Kikwete anavyopokelewa

Tukisema kuwa utawala wa Kikwete ni wa kifamilia au ufalme fulani kama siyo usultani tunaambiwa chuki. Tusaidiane. Huyu mama hapa anapokelewa kwa ma rais kwa itifaki ipi kama siyo matumizi mabaya ya madaraka? Ni ajabu hata washauri wa mumewe hawalioni hili na kama wanaliona wanaoogopa kusema ukweli wasiteme kitumbua. Jamani it is too much. Ajabu wanajeshi kama hawa wakipiga picha na wapinzani wanaambiwa ni makosa. Ni vigumu kujua rais na mkewe nani ni rais katika hali hii na matumizi mabovu ya madaraka ya namna hii.

1 comment:

Jaribu said...

Ndio mambo yale yale ya two for the price of one. Wangekuwa ma-genious tungeshukuru, but since wote wanaendana in the brain dept ndio basi tunateseka. Two for one works better for pizzas, not presidency.