Taarifa zilizosambaa ni kwamba Tanzania sasa inakumbwa na machafuko karibu kila kona. Hii ni kutokana na wananchi kuishiwa imani na serikali wakati serikali yenyewe ikiendelea kufanya madudu. Siyo kujisifu bali kukumbusha. Kinachotekea Mtwara kuhusiana na gesi asili nilikitabiri miaka minngi iliyopita katika kitabu changu cha Saa Ya Ukombozi.
Saa Ya Ukombozi inamtumia mzee Njema na wakazi wenzake kijijini mwake ambapo mwekezaji mzungu alikuwa kanunua eneo lao ili achimbe madini. Mtafaruko ulifumka hadi askari wakatumwa toka mji mkuu wa Neema ambapo hwakufua dafu hadi mkuu wa mkoa alipopata kipigo na hatimaye serikali kuangushwa kwenye uchaguzi uliofuata.
No comments:
Post a Comment