Friday, 4 January 2013

Ndege yauzwa sh. 500,000!


Ufisadi unapofusha na kuharibu akili za watu. Nani angeamini kuwa ndege ingeuzwa shilingi za kitanzania laki tano? Kauziwa nani? Hata waziri wa serikali anaogopa kuuliza na kupewa jibu. Je huu mchezo ulianza lini na umeishaliingizia taifa hasara kiasi gani?  Inashangaza kuona madudu kama haya yanatendwa katika nchi maskini kama yetu! Utakuta wahusika wanaiba vipuri na kuvificha halafu wanauziana ndege kwa bei ya ubuyu. Namna hii tutashindwa kuuana huko tuendako? Hivi rais Jakaya Kikwete na genge lake wanataka kutufikisha wapi yarabi?  Ukisoma jinsi waziri alivyohoji ufisadi huu na namna alivyotoa maelezo yenye utata, utagundua kuwa nchi imefikia pabaya. Hapa tunaongelea ndege, Kama ndege inauzwa laki tano hayo magari si yatauzwa shilingi tano? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

No comments: