Thursday, 3 January 2013

Mibaka na majambazi wetu jifunze kwa Bill Gates

Where does this man rank among the 10 richest Americans?
Tumemaliza mwaka kwa habari mbaya na chafu ya kukua kwa deni la taifa kwa asilimia 400. Mwaka 2007, kwa mujibu wa magazeti lilikuwa ni dola bilioni 3. Hadi mwishoni mwa mwaka jana lilichumpa hadi dola bilioni 14! Nini kimefanyika cha maana zaidi ya wizi kama kawa? Muulize bwana rais na wenzake.
Wakati mataifa mengine yakijifunga mikanda na kukuza chumi zao kwa kupunguza au kuachana na utegemezi na kopakopa, Tanzania ndiyo inapanua mkanda kukopa na kuombaomba. Laiti jinai hii ingeishia hapa. Wenzetu wenye madaraka wanashindana kutuibia wanyonge tena wakitumia hilo chumo la wizi kutuhonga eti tuzidi kuwapa ulaji zaidi kwa kuwachagua! Je sisi ni vichaa na mataahhira au wafu wanaotembea? Je tumekosa kumbukumbu hata ya mambo muhimu kama haya?
Kuzidi kuumka kwa deni la taifa maana yake ni kwamba wezi wetu walioko kwenye madaraka waliiba sana kwenye mwaka uliopita.
Watu wenye akili na visheni kama Bill Gates tunaambiwa kwa mwaka jana tu wametengeneza faida zaidi ya nusu ya deni letu la taifa. Ni ajabu rais Jakaya Kikwete bado anajifisia upumbavu kupitia waziri wake wa fedha (fedheha) William Mgimwa kuwa watanzania wasiwe na wasi wasi kwa vile seerikali imewekeza kwenye huduma za jamii. Huduma gani za jamii wakati mgao wa umeme, uhaba wa maji, uduni wa huduma za afya na elimu vinazidi kupanda chati?
Mgimwa bila aibu anaongeza kusema kuwa serikali imewekeza kwenye miundombinu! Anaanisha miundo mbinu ya Magufuli ya vodafasta siyo? Rejea tarehe 2 Januari daraja linalounganisha kanda ya ziwa na Pwani lilipoharibika kule Singida kutokana na kujengwa chini ya kiwango. Hiyo ndiyo miundo mbinu anayojitapa nayo Mgimwa? Shame on you Mgimwa!
Tukubaliane kuwa Kikwete ameshindwa nchi na ataishia kuwa janga la kitaifa ambalo watanzania hawatasahau maisha yao.
Kwa waliofanikiwa kama Bill Gates hebu GONGA hapa kwa taarifa zaidi.

No comments: