How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Sunday, 16 June 2013

Huyu Kikwete vipi utadhani waziri wa michezo na si rais!


Wengi tulipopata habari za kutokea shambulizi la kigaidi kwenye mkutano wa kampeni kule Arusha tuliumia na kulaani kitendo hiki. Pia tulidhani taifa kwa wakati huu lingepata faraja angalau kutokana na rais wao kuwahi kwenye tukio na kuonyesha mwelekeo wa taifa. Tumeshuhudia viongozi wengi wakiacha shughuli zao nyingi na kuwahi kwenye matukio kama  haya. Rais Barack Obama anaongoza kwenye umakini huu. Jamaa yetu Vasco da Gama bin Kikwete ndiyo hana habari!
Au kwa vile walioumizwa ni wapinzani? Je Kikwete anafanya madai ya CHADEMA kuwa waliowalipua ni CCM kwa woga wa kuondolewa madarakani? Je yeye ni rais wa CCM au wa mipira na kujilisha upepo kwa kuzurura kila sehemu hata bila sababu? Kwanini Kikwete amekuwa mwepesi na mpenzi wa mambo ya hovyo hata yasiyolingana na cheo chake huku akikwepa majukumu muhimu ya ofisi yake?Je ni kosa kumuita historia ya kisiasa Tanzania? Mko wapi CCM? Yuko wapi Kinana na Mangula? Uko wapi Nape na Mwigulu?
Tujirejea kwa Kikwete,  huwa haishi vituko. Yeye yuko London mkewe Marekani akipokea tuzo ya uongo na ukweli. Nilicheka sana alipopigwa picha akipokea hiyo tuzo. Wapambe wake walirekodi mkanda wa video akipokea hiyo tuzo. Ilipofika zamu ya kuongea kiingereza chake cha mimi ni Maimuna walikata picha ili wasionyeshe kihiyo huyu anavyojikanyaga na kutoa jasho debe kwa vile hajui kimombo.
Je tutaendelea kuwa na mtawala kituko hadi lini? 
Tutafakarini.

6 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu umepotea sana. Nasikitika kuwa comment yako imefutika wakati nasafisha majunk ambayo kwa siku napokea zaidi ya mia tano hivi. Hivyo haikufutwa kwa sababu nyingine bali kwa bahati mbaya. Natamani kungekwua na njia ya kui-retrieve ningefanya hivyo kwa gharama yoyote. Apology.
Nakumbuka ulisema bi kihiyo akisema Zis Njaa kaya anasema usiseme zis sema zat au vipi?

Mtwangio said...

Mhango kama utakumbuka na nadhani unakumbuka vizuri,katika mwaka 1980 Marikani na wafuasi wake waliamua kususia michezo ya Olimpiki ambayo ilifanyika mjini Moscow kwa hoja ya ufamizi wa kijeshi wa Urusi(Soviet Union)kuifamia Afghanistan,hoja ambayo imekiuka hata maadili ya michezo yenyewe kwamba michezo isichanganywe na siasa lakini Marekani na wafuasi wake walikiuka maadili hayo na kuamua kuisusia michezo hiyo ya Olimpiki Moscow.Na kwa kufanikisha ususiaji huo Marekani ilituma wajumbe wake kulingana na zone zilivyo na Afrika ilimtuma Bondia mashuhuri wa marekani Muhamed Ali.Nadhani utakumbuka vizuri bondia huyu alitembelea nchi alizoambiwa ataembelee Afrika na katika zaara yake hiyo alipokewa na marais wa mataifa hayo ya kiafrika isipokuawa Tanzania tu ambapo mwalimu alionyesha umakini na maadili ya uongozi na kumtuma waziri wake wa elimu na michezo kwa wakati ule Daniel Mgonja ambaye alimpokea Muhamad Ali na kuongea naye au kwa lugha nyingine kumsikiliza na hatimaye Muhamed Ali aliondoka Tanzania bila ya kupata heshima ya kuonana na kiongozi wa nchi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na maamuzi ya Tanzania ilishiriki kikamiilfu katika michezo hiyo ya Olimpiki ya Moscow.

Mhang,ebu tujaribu kuangalia kama historia inweza kujirudia japo kwa mazingira tofauti ikatokea Marikani kumtuma Michael Jordan au Kobe Bryant au hata Michael tyson,au Uingereza ikamtuma David Beckham na mkewe kuja Kuja Tanzania kufikisha ujumbe wa mfano wake je unadhani Jakaya Kikwete atamtuma waziri wake wa elimu na michezo kwenda kuwapokea wana michezo hao?Hapna tena hapana kabisa yeye mwenyewe Kikwete atakuwa mstari wa mbele na mkewe kwenda kuwapokea wanamichezo hao kuongea nao na hata kuwafanyia ndafu ya kitaifa kwa kuhudhuria viaongozi wengine wa serikali na kuchukua nao picha nyingi za kumbukumbu huyu ndie kiongozi wetu mtafutaji umashuhuri rahisi kama mtu binafsi na kusahau wadhifa wake kama rais wa nchi na nadhani kumbukumbu yako ya karibuni itakurudia kwa kuonana na mchezaji maarufu wa Brazil kwa jina la Kaka na kupokea zawadi jezi yake namba 10!!!

Huyu ndie Kiongozi wetu anapofanya ziara za kiserikali na wala sio binafsi anakuwa na ushujaa wa kutembelea viwanja vya clubu kubwa kubwa na kupiga na viongozi na wachezaji picha za kumbukumbu kama ilivyotokea kuutembelea uwanja wa Real Madrid kule Spain!!!!!

Mtwangio said...

Lakini na tuangalie kwa upande wa pili kwa nini rais wetu nafanya hivi je kwa ni mzembe kiasi hiki cha kutokuwa na hofu ya wananchi wake kumuona ni kama mtu ambaye anawafedhehi kwa kutafuta umashuhuri rahisi kiasi hiki?Kwa maoni yangu Mhango ni lazima tumuangalie kama mwanasiasa jinsi gani anavyowajua wananchi wao na udhaifu wao au nini wanachokipenda na hatimaye naye hutafuta umashuri wa rahisi kupitia humo.Ebu waangalie watanzania wa leo na hususa vijana na kipi kinachowashughulisha zaidi katika kichwa chao na ukiwagusa hapo tu basi umewafikisha!Vijana wa kitanzania mchezo wa mpira wa miguu ndio unaowashughulisha sana na laiti kama mchezo huo wangetilia maanani sana timu zao za nyumbani lakini si hivyo leo hii ligi ya daraja la kwanza ya uingereza(Baclay primire league) ndio inayowashughulisha vijana utakuta vilabu vya uingereza vimechukua nafasi na wachezaji wao vimechukua nafasi katika vichwa vya vijana kuliko hata kuona dhuluma wanayofanyiwa ya kukosa haki yao ya maisha hususa ajira na kujipanga kuiondoa CCM madarakani.Ukimwamsha leo usingizini kijana yoyote yule wa kitanzania ukamwambie akupangie list ya wachezaji 11 wa timu yake ya uingereza atakupangia bila ya kusuasua.Leo hii mheni yoyote akiingia Tanzania atasitushwa kwa kuona ligi ya uingereza ilivyochukua nafasi katika nchi yetu kuliko chochote kile!!!!

Sasa kikwete kama mwana siasa nalijua hilo na nautumia udhaifu huo wa watanzania na anawapa kile ambacho wanachokitaka na kukipenda kwa hiyo watanzania hususa vijana hawaoni aibu ya aaina yoyote ile kumuona rais wao kapika picha kama iliyopo hapo juu na nyingine nyingi tu ambazo tumeshaziona kwa hiyo kikwete ajali kuwadhalilisha watu wachache wenye akili zao muda wa kudumu anawapa wengi wanachokitaka na kama utakumbuka rais Mabutu wa Zaire aliwapa wazaire uhuru wote wa starehe za aina yote uzijuazo na wananchi wa zaire wakalala usingizi wa kutosha mapaka wenye akili walipozindukana.Hawa ndio wnasiasa wetu watatumia kila mbinu na njia jinsi gani ya kubaki madarakani kwa kwa kutumia umashuri rahisi na hata wakati mwingine kutumia uchochezi wa dini na ukabila na hata kuwatia hofu wananchi, kwa mfano hofu ambayo inayowatia CCM wananchi kwamba nchi yetu ni ya usalama na amani muda wa kudumu itaendelea kutawaliwa na CCM na chama chochote kitachokuja madarakani kitaondoa amani hiyo na usalama huo na kwa bahati mbaya wananchi wengi wanaliamini hilo wakisema kwamba bora zimwi ulijualo kuliko usilolijua!!!!!

Mtwangio said...

Mhango nadhani tinatakiwa tuendelee na mapambano haya na hususa kuwaenga vijana wawe na mwamko wa kutosha zaidi wa kuyajua yepi ni muhimu kwanza katika maisha yao kuliko viburudisho vingine vyovyote vile katika maisha yao wakati umefika kwa vijana kuiona CCM ni adui yao na isiyowatakia kheri leo hii japo sina takwimi ya kielimu kwamba katika vijana 100 wangapi hawana ajira lakini kama sitii chumvi naweza kudai kwamba ni 50% vijana hawana ajira na tunapoelekea ni pabaya zaidi kwani unaweza ukawa na shahada ya elimu ya juu na ukawa huna kazi kwa sababu ya kimsingi kwamba CCM haipo tayari kubuni ajira kwa vijana wa kitanzania na matokeo yake uovu mwingi wa kijamii unapatikana na maadili muhimu ya kijamii yamekufa.Mwalimi Nyerere alikua ni kiongozi mwenye mtizamo wa mbali kwani alitoa elimu bure kwa taifa na kwa wakti ule tulikua tunasema kuchaguliwa kutoka darasa la saba kuendelea na elimu ya vidato na hatukusema kufaulu kwa maana mwalimu alijua kwamba atabakiwa na jeshi kubwa la vijana waliomaliza darasa la saba kwa hiyo aliwafikiria hawa kwanza kabala hata ya wale ambao wataendelea na elimu ya vidato na kwa wote wataoukumbuka utawala wa mwalimu kwa wakati ule wengi wa vijana ambao hawakupata bahati ya kuchaguliwa na elimu ya vidato walikuwa na ajira achilia mbali kuwaelekeza vijana wengine katika shule za ufundi ambao waliweza aidha kujitegemea wenyewe au kuajiriwa katika sekta hiyo ya ufundi.Huyo ndie aliekuwa kiongozi aliewapenda wananchi wake na nchi yake je kuna kiongozi gani kuanzia awamu ya pili hadi hii ya kikwete ambaye amejua kwamba kuna jeshi kubwa la vijana ambao inabidi kuwaangalia kwa makini na kuwajengea mustakibali wao wa maisha ili wapate kuyamudu maisha?Jibu lipo wazi hakuna!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mtwangio nakubaliana nawe. Katika uchambuzi na kumbukizi vyako nimeambua kitu kimoja kuwa hatuna rais bali mhuni mmoja tuliyefanya kosa kumpa nafasi ambayo anapwaya. Kikwete, kwa bahati mbaya, aliingia madarakani kama ajali kutokana ufisadi uliokuwa umetendwa na Mkapa ambaye tuliaminishwa na Mwalimu Nyerere kuwa alikuwa mwanafunzi wake makini asijue ni mnafiki na fisi aliyekuwa amevaa ngozi ya kondoo. Kikwete anafuata nyayo za mtu mwingine wa hovyo aliyewahi kuwa rais wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi ambaye alipoteza muda mwingi eti kwenda kuongea na fag Michael Jakson. Nadhani laana hii imelikumba taifa. Laiti Mkapa asingetenda uovu alioutenda kama vile kufanya biashara ikulu na kushiriki mauaji ya Dk Ali Juma ambaye alikuwa tishio kwa Vasco da Gama ambaye ataingia kwenye vitabu vya historia kama mhuni aliyewahi kukalia kiti cha rais.
Kuhusiana watu wetu, nina shaka nao. Ima ni woga au wanafiki. Nikiona kazi njema inayotendwa na upinzani, nilidhani wangeuunga mkono na kuondoa uoza huu uitwao CCM na ufisadi na harufu vyake. Hebu nikupe mfano mdogo wa unafiki wa watu wetu. Kama watoto wa Kiislamu waliouawa na mabomu ya Arusha wangeuawa wakati wa mkutano wa CCM ungesikia waislamu wakilaumu na hata kutishia kukichukulia hatua CHADEMA chama cha 'wakristo'. Ila kwa vile walioua ni wenzao wamenywea na kujifanya hayawahusu. Hata hivyo nadhani kwa uhuni huu wa CCM huenda watu wetu watachoka na kujitambu na kuamua kuchukua hatua mjurab.

Jaribu said...

Hamna tabu, Mhango. Point ilikuwa Salma Kihiyo hawezi akamwaga chizungu wakati mumewe Dr Kilaza ndio bingwa wa, "...Of course when we had independence we had three roads.....of course this, of course that. Of course I am a miserable excuse for a leader."

Huwa napita pita lakini si unajua kazi za wenzetu, deadlines haziishi ndio maana wakati mwingine napita pita tu bila kuacha maoni, muda unakuwa adimu.

Mtwangio unasema kweli, Kikwete siyo genius lakini ana akili ya kuwajua kuwa vijana wengi wa Tanzania hawana msimamo na ndio maana na yeye anashabikia vitu vya kijinga kama mpira na matamasha na bongo movies kwa kujitafutia umaarufu mwepesi.

Mhango, nakubaliana na wewe kuhusu Kikwete kufuata nyayo za Ali Mwinyi. Lakini kumbuka ni Ali Mwinyi anayestahili kulaumiwa kwa kumfukua Kikwete kutoka kwenye pango lake la mediocrity huko kwenye ukatibu kata wa CCM.

Sijui lini watu wetu watachoka kuuawa na kupelekeshwa. Inanikumbusha kwa uchungu mababu zetu walivyokuwa wanashindwa na Wazungu na vikosi vya wazungu hamsini. Mmarekani mmoja ambaye ni mzungu alishangaa akaniuliza ilikuwaje Waafrika walikuwa wanababaishwa na wageni kutoka Ulaya. Nikamjibu kuwa ni kwa sababu walikuwa na bunduki. Ndio wanavyotufanyia Chama cha Mafioso.