Wednesday, 1 May 2013

Hii ndiyo namna ya kupambana na uchakachuaji


Opposition lawmaker Julio Borges with facial bruises after clashes. Photo: 30 April 2013

Nchini Venezuela, wabunge wa chama tawala na wa upinzani walitoana ngeu wakigombea matokeo ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni ambapo chama tawala kilishindwa kwa mbinde. Venezuela ilifanya uchaguzi baada ya kufariki kiongozi wake machachari Hugo Chavez hapo Machi 5.
Baada ya kufariki Chavez, uchaguzi uliitishwa ambapo mrithi wake wa kupenndekeza na makamu wa rais Nicolas Maduro aligombea na kiongozi wa upinzani Henriqe Caprilles. Maduro alishindwa kwa asilimia 50.7 kitu ambacho kilifanya upinzani kuja juu na kudai kulikuwa na vitendo vya wizi wa kura. Jana wabunge wa upinzani na chama tawala walijikuta wakitoana ngeu wakigombea matokeo. Hakika, wakati mwingine dawa ya uchakachuaji kama ambao tumezoea Tanzania ni ubabe kama walivyofanya wabunge wa Venezuela. Kwa habari zaidi BOFYA hapa.

No comments: