How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 14 May 2013

Je mbunge wako ni kati au sawa na hawa kwenye picha?





Baada ya wabunge wa Kenya kuwasaliti waliowachagua kwa kuonyesha uchu na uchoyo wa ajabu---'greed charged', wakenya wamekuja na njia ya aina yake kuonyesha hisia zao. Kumekuwapo na maandamano ambapo uroho wa wabunge kutaka waongezewe mishahara hata kabla ya kuanza kazi unaonyeshwa kama unguruwe. Nguruwe wengi wamemwagwa kwenye eneo la maandamano wakiwakilisha wabunge. Kwa wanaomjua mnyama nguruwe alivyo wa hovyo, wanashangaa ubunifu huu uliobeba ukweli kuhusu karibia wanasiasa wengi barani Afrika. Je hawa 'nguruwe' wataacha uroho kwa maandamano au hadi umma ukalie bunge kama wakenya wasemavyo--occupy the parliament? Wanaharakati wameamua kuwaita wabunge au Members of Parliament (MPs) MPigs! Patamu hapo! Nampongeza kiongozi wa vuguvugu hili rafiki yangu Nahashon Gacheke Gachihi kwa ushupavu wake na taasisi yake ya Bunge la Mwananchi ambayo nilikuwa mshiriki nilipokuwa nchini Kenya. Je nawe mtanzania unaona mbunge wako ni sawa na hawa? Je wewe ungependa utumie nguruwe au mbwa kama siyo kujaribu fisi? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

3 comments:

Jaribu said...

Afadhali Wakenya wamechangamka. Watanzania wakizidiwa wanaongeza maombi na dua mpaka CCM waamue kuwa wametosheka kuwaibia wananchi waondoke wenyewe.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu una maana kuwa MPigs wetu ni walafi na wachafu kuliko Mpigs wa Kenya siyo? Mie siongezi neno. Nangoja watetezi wao wasiolipwa waje wamwage sera hapa. Kwa ufupi ni kwamba hali inatisha kwenye nchi yetu. Nikiangalia vijana waliowezesha hili nashangaa sisi tunakosa nini. Mfano kiongozi wao aitwaye Nahashon Gacheke Gachihi namfahamu. Ni kijana mdogo kiumri ambaya ana mwili mdogo lakini mwenye moyo mkubwa. Ni shabiki wa kufa wa mwalimu Julius Nyerere. Miaka michache iliyopita alishiriki kwenye kongamano la Kigoda cha Mwalimu. Aliniandikia akisema kuwa ametimiza mojawapo ya ndoto ya maisha yake yaani kuwa karibu na hisia na mawazo ya mwalimu hata kama hakupata bahati ya kukutana na mwalimu alipokuwa hai. Tanzania tuna bahati mbaya kuwa na vijana kama Mwigulu Nchemba ambao wanapoteza muda kuwaandalia misiba na kesi wenzao kutokana na kushiba mabaki ya ufisadi.

Jaribu said...

Mpigs wetu wanakatisha tamaa. Wao ndio mfano mzuri wa "rubber stamp parliament."

Ingawa Nyerere alikuwa na mapungufu yake, inafurahisha kuona angalau kuna sehemu anaheshimika kwa mchango wake. Sijui lini tutapata vijana kama huyo Nahashon