Wednesday, 22 May 2013

UhuRuto mwisho wa honeymoon waanza kuvurunda

Kibonzo kinachoonyesha naibu wa rais William Ruto akifaidi vitu kwenye ndege aliyokodisha kwa mamilioni ya shilingi huku ikiwaacha wakenya wamegawanyika wakilaani Hustler kupenda kuponda maraha kiasi cha kukinzana na jina lake la mgumu. Watawala wa kiswahili hawana tofauti na wachezaji wa karata tatu ambao huwatapeli watu kimasomaso. Je mwanzo wa Ruto kuporomoka hata kabla ya kuporomoshwa na ICC ndiyo umeanza? Kama naibu jaji mkuu alitimliwa kutokana na kukosa maadili itakuwaje kwa Ruto? 

No comments: