Tuesday, 21 May 2013

Huu ni utani au utabiri?

Baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahaman Kinana kusemekana kuwa nyuma ya genge linaloua ndovu wetu na kuuza pembe zake nje, naona wataalamu wa mambo wamekuja na njia nyingine ya kueleza hisia zao. Je hawa wanatabiri kuisha kwa tembo wetu wakabaki kwenye chupa au kulewa kwa watawala wetu pesa ya ndovu kiasi cha kutuingiza katika chupa. Kinana anangoja nini? Je Kikwete aana namna anavyonufaika na kashfa hii sawa na ile ya kughushi inayowakabili watu wake? Tuwabane hawa watu wawajibike au tuwawajibishe watakapokataa kujiwajibisha.

2 comments:

Mtwangio said...

Hawa watu hawaamini kamwe kama wananchi wanaweza kuwatishia maulaji yao na kila panpokuwa maulaji Kikwete anausika tu na waramba viatu vyao hakuna dili itakayofanyika ya kuihujumu nchi na wanachi bila ya kuwepo panga lake na ndio maana uoni au kusikia anawachukulia hatua yoyote ile waramba viatu vyake au wapambe wake.Ikizidi tu ndio kwanza anawabadilisha kutoka maulaji haya na kuwapeleka katika maulaji mengine na huu ni utamduni wa uongozi wa CCM la kushangaza zaidi kusikia dakitari anapewa wizara ya ulizi au profesa akapewa wizara ya michezo na utamuduni ili mradi tu walindane wa waficiane na hakuna mmoja anaeweza kumnyooshea mwenzia kidole.Je ni mabadiliko gani ya kimsingi ambayo umeyaona anapolibadilisha baraza lake la mawaziri?.Je ni kweli sisi watanzania hatujui nini kinachoendelea,hatujui nini nchi na thamani ya nchi?je ni kweli hatuju urithi wa nchi ni nini na ni nani atakaerithi?Na tatizo hili limezuka tangu wachina kuiingia mtaani wao ndio wanaongoza kwa biashara hii ya pempe za ndovu,je wanapata wapi helikopta za kuwindia ndovu hao kama si kutoka serikalini?Na kama wazungu si kuingilia kati katika kulinda wanyama Afrika si ndovu tu bali wanyama wengi wangetoweka,kwani wazungu wao wanajua urithi wa dunia kwa kulinda mazingira na wanyama japo kwa masilahi yao ya utalii na kizazi chao.Lakini inapotokea masala ya kutuibia kirahisi utajiri wetu wa ardhini wakishirikiana na viongozi wetu wazungu hao hao hawaziti kuharibu mazingira kwa kumwaga sumu barani afrika kutuharibia maji yetu na hata kutufanya panya wa majaribio kwa kutuletea madawa kwa kuyajaribu.Naam,Mhango wewe tufichulie tu ufisadi wao,tamaa zao na wizi wao naamini ipo siku watanzania watachukua maamuzi ambayo wao hakuyategemea kuonewa na kudhalilishwa kuna mwisho wake.

NN Mhango said...

Mtwangio usipate taabu. Hili ni suala la muda kwa sababu hakuna jamii isiyobadilika. Ingawa watawala wetu fisadi hawataki kukubali hili, wanajua siku zao zinazidi kuhesabika. Zamani hatukuwa na nyenzo nyingi za mawasiliano kama sasa. Kwa mfano, kwa sasa mimi nawe na Jaribu tunajuana na kuwasiliana kana kwamba tunaishi kwenye kijiji kimoja. Hivyo, taratibu mambo yatabadilika na kuwaharibikia wale waliozoea business as usual katika ufisadi na ujambazi. It is just the matter of time so to speak.