Friday, 3 May 2013

Mafisadi wa kihindi na washirika wa mtoto wa rais waitikisa serikali ya Zuma


Mmojawapo wa Guptas akiwa na Duduzane Jacob Zuma (pichani)

Baadhi ya maafisa wa serikali ya Afrika Kusini wamesimamishwa kazi ili kuchunguzwa baada ya kuruhusu ndege binafsi kutua kwenye kambi ya kijeshi kinyume cha sheria. Waliosababisha kashfa hii ni 'matajiri' wa kutia shaka wa  kihindi wa familia ya Gupta ambayo licha ya kuwa na urafiki na rais Jacob Zuma, ni washirika wa kibiashara wa mwanae Duduzane.

Ndugu watatu wa familia ya Gupta wanaosemekana kuanza kutajirika Zuma alipoingia madarakani, walitua kwa ndege yao binafsi na kufanyia sherehe za harusi karibu na kambi hiyo jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Ushirika wa mtoto wa Zuma na urafiki wa baba yake na familia ya Gupta umeamsha tashwishi na shaka hata shuku nyingi nchini Afrika Kusini hasa baada ya familia hiyo kumtenga Zuma na ujumbe wa watu alioandamana nao kwenye ziara ya kiserikali nchini India. Si Afrika Kusini tu ambapo familia ya Gupta imetia shaka na doa. Kwenye ziara ya Zuma nchini India, watawala wa India walishangaa hadi kuwauliza baadhi ya wajumbe inakuwaje rais anaburuzwa na matapeli kiasi hiki. Kutua kwa ndege kwenye kambi ya kijeshi kumeacha maswali mengi hasa ikizingatiwa kuwa ilikuwa ikitoka nje ya nchi ikiwa na watu 200. Je ndege hii ilikuwa imepakia bidhaa haramu kama mihadarati au wahamiaji haramu? Je watu wa uhamiaji walikagua abiria na bidhaa zilizokuwamo kwenye ndege hiyo? Wachambuzi wengi wamekuja na hitimisho kuwa Afrika Kusini haipaswi kuaminiwa tena kwenye masuala ya usalama pamoja na kuwa na nguvu nyingi za kijeshi barani. Je Zuma ameendelea kujivua nguo kutokana na kuwa na historia ya ufisadi? Je ndege hii ililete biashara za Zuma au mwanae? Je maadui wa kimataifa wakiamua kutumia njia si watafanikiwa hasa kipindi hiki cha ugaidi? Maswali ni mengi kuliko majibu. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa na HAPA na HAPA.

4 comments:

mtwangio said...

Kusoma kwa taarifa hizi kuhusu South Afrika kweli ni jambo la kusikitisha,sikudhani kamwe kwa nchi ya uzito mkubwa barani Afrika na kuchukua nafasi yake katika nchi zinazoheshimiwa duniani na nchi ambayo inayohsabiwa kama ni developed inakatisha tamaa kweli.

Najua wazi kabisa kwamba wahindi ambao walikuja katika nchi hiyo mwishoni mwa karne ya 19 walishiriki kikamilifu na waafrika katika kupigania uhuru wa nchi na kujikomboa katika mikono ya utawawala wa kikaburu.

Leo mji wa Durban unazingatiwa kwambani mji wa wahindi wengi duniani ukiachia nchi yenyewe ya india.kwa hiyo wanakubalika bila ya kipingamizi kwamba wahindi wameshiriki na wanashiriki kuijenga South Afrika.

Lakini inapotokea kwa nchi kama ya South Afrika kuwa ni sehemu ya kupatikana ufisadi kwa kupitia ngazi za juu kabisa ambayo Rais mwnyewe anahusika moja kwa moja ni jambo la kutia aibu sana na kuendelea kwa mwafrika barani afrika kuzingatiwa ni mtu wa kutumia tu hata kama ni rais wa nchi.

Lakini kwa muono wangu japo ufisadi ni ufisadi du popote pale unapopatikana na hakuna kufumbia macho au kutoa sababu za kutetea lakini sidhani kwa level ya nchi kama ya South Afrika kwamba wahindi hao au familia hiyo itakuwa na msemo serikalini kama walivyokuwa na msemo ma maamuzi kama katika nchi ya bongolalaland.

Kiasi ya kwamba leo hii muhindi wa Tanzania anjihisi ana sauti na yupo huru zaidi kwa kumyanyasa mtazania kwa sababu moja au nyingine inatosha tu hata kama ni dhana ambayo hajafanyiwa uchunguzi wa kiserikali lakini wahindi hao wa Tanzania wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania ndio waliomuondoa duniani Sokoine tegemeo kubwa la nchi yetu ya Tanzania na wananchi wake,je itafika wakati wahindi hao wa Tanzania kupoteza nguvu zao za ushawishi kwa wanasiasa wetu na viongozi wake?N a je ni kweli au ni dhana kwamba kuna makubaliano ya chini kwa chini kati ya serikali za Afrika Mashariki na nchi za magharibi hususa Wingereza kwamba wahindi wa Afrika Mashariki wasiguswe kwa karibu au kwa mbali na mali ambazo walizozichuma katika nchi hizo kama ilivyototea wakati wa wa utawala wa kiongozi mzalendo wa Uganda Idi Amini?

Na kwa nini tuwe sisi tu waafrika wa bara la Afrika ndio tuwe wenye kutoa nafasi kwa ma-hustles wa dunia nzima kuja kujitajirisha kwetu je ndoto ya Afika siku moja kuwa ya Mwafika itapata nuru lini??!!

NN Mhango said...

Mtwangio sikubaliani nawe kuwa wahindi walishirikiana na waafrika kumuondoa kaburu. Kama ukisoma historia ya Mahtma Gandhi aliyeanzisha harakati za wahindi kudai haki zao, utakuta kuwa alikuwa akidai haki za wahindi kama second class citizens huko SA na si haki za wote. Hawa jamaa wamekuwa wabaguzi kila wanakoishi isipokuwa katika nchi zenye kukaliwa na wazungu.
Kimsingi waafrika tusipobadilika na kujiona kama watu sawa na wa rangi nyingine na tuna jukumu kwa nchi zetu, kuna siku tutaishia kuwa kama visiwa vingi vya bahari ya Hindi vinavyonywa na kutawaliwa na jamaa hawa. Pia hii kashfa kwangu ni baraka kwa SA kama watakubali kuwa waliingiziwa mkenge na tapeli Zuma bin Casanova Zuma ambaye hana tofauti na kilaza wetu. Dudu hana tofauti na Riz wala Muhoozi au Christel Ngwesso na majambazi wengine waliozaliwa na majambazi wenye madaraka.
Ingawa Tanzania inaweza kushangaa vitu kama hivi kwa vile siri zake hazijafichuka, ukweli ni kwamba imefanya machafu mengi kuliko hata haya mojawapo likiwa hili ulilogusia la mauaji ya kishenzi ya Sokoine.
Nashukuru kwa mchango wako adhimu na muhimu Mtwangio.

mtwangio said...

Nami nakubaliana nawe kwa kunisahihisha muono wangu huu kuhusu kushiriki kikamlifu kwa wahindi wa SA na waafrika kuundoa utawala wa Makaburu,ukiachilia mchango wa wachache kama vile mwanasiasa wa kihindi Ahmed Kathrada ambaye alijiunga na chama cha ANC na kufungwa pamoja na Nelson Mandela katika kisiwa cha Robben na kwa kuwepo kwa muhindi huyu katika harakati dhidi ya serikali ya makaburu nikasoma historia kimakosa kwa muhindi huyu mmoja kuwepo katika chama cha ANC.

Na upo sahihi kabisa uliposema" Hawa jamaa wamekuwa wabaguzi kila wanakoishi isipokuwa katika nchi zenye kukaliwa na wazungu."na ubaguzi wao huu umejizatiti katika itikadi ya dini yao ya kihindu ya caste system ambayo ni sehemu isiyokubali kujadiliwa hata kidogo kama utakumbuka hata Mahtma Ghandi alijaribu kuigusa kwa kutaka kuwafanya wahindi waondoe itikadi hiyo lakini hakuna aiyemsikia.Sasa ikiwa wenyewe kwa wenyewe wanabaguana ubaguanaji unaofanana na system ya apartheid ya wataendelea kuwa hivyo popote pale walipo duniani lakini cha kushangaza tu wanakuwa kama mbwa mbele ya chatu pale tu wanapokuwa mbele ya wazungu.

Na baya zaidi na naamini hivyo waingereza wanawatumia hadi hii kwa njia moja au ningine kulinda masilahi yao.kwa nini wengi wa wahindi wa Afrika Mashariki wana uraia wa uingereza?Na ndiyo maana baada wahindi wa Uganda kufukuzwa Uganda hawakwenda India bali walikimbilia Uingereza na wakawa ni mzigo ambao waingereza hawakuutegemea.Na je kwa nini hadi hii leo wanatajirika katika nchi zetu kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa na wa serikali wakiwemo marais wetu na kutorosha pesa na kuzipeleka nje?

Nasema tu wenye kustahiki lawama ni viongozi wetu ambao hawapo tayari kuifanya Afrika ni ya mwafrika kwa hiyo kana kwamba utajiri wetu wa asili sisi tumekuwa kama walinzi tu wa mlango tunawalindia mabwana zetu wanapoaamua kuja kuchukua utajiri huo wawe wazungu,wahindi,waarabu na leo hii wachina!!!!

NN Mhango said...

Hapa tumeelewana. Wahindi walijiunga na ANC baada ya kugundua kuwa ina uwezo kufanikisha kuleta uhuru na ukombozi wa Afrika Kusini. Angalia hata jina la chama.
Hawa jamaa ni wadhaifu sana wanaopenda kudandia kila penye uwezekano wa ulaji. Waingereza husema backing a winning horse. Bahati mbaya hawa jamaa hum-corrupt huyo horse kama unavyoona akina Kikwete Zuma na Moi na wengine wengi barani Afrika. Hata hawa wahindi mnaoona wamejaa CCM ikidondoka au kuonyesha uwezekano wa kutokidhi mahitaji yao--corruption, wataikimbia kwa mamia waingie chama kitakachokuwa na ulaji mkononi. Huu mara nyingi huuita uchangudoa wa kiuchumi. Hivyo kilichofanyika hivi karibuni huko Afrika ya Kusini ni matokeo ya kuwa na rais kahaba wa kila jambo.
Kweli Gandhi alijaribu kusambaratisha caste system lakini badala yake ilimsambaratisha. Nadhani Gandhi alithubutu baada ya kuishi Uingereza na Afrika Kusini akaona wahindi walivyo kwenye losing side hata kama alikuwa akitokea kwenye daraja la Kshatriya. Hata ukisoma falsafa yake ya Satyagraha na jinsi ilivyochukuliwa na wahindi unakuta ilichimbuka Afrika Kusini.