Sunday, 5 May 2013

Ziara za siri za Kikwete zina manufaa kwa taifa?


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakipigiwa nyimbo za mataifa hayo mawili kabla ya kukagua gwaride rasmi mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei, 5, 2013. 

 Rais Jakaya Kikwete ataingia kwenye vitabu vya historia kama rais wa hovyo na dhaifu ambaye Tanzania imewahi kupata. Inakuwaje rais wa nchi anafanya ziara tena nje ya nchi na umma wa watanzania haufahamishwi? Nimeshangaa kusikia kuwa rais Kikwete yuko ziarani nchini Kuwait. Nimeshangaa kusikia kuwa rais ameondoka kimya kimya bila umma kujua kana kwamba anakwenda kule kuiwakilisha familia yake yake na si nchi.  Inashangaza kuona hata magazeti ya serikali hayajabeba habari hii!Hata tovuti ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliogopa kuchapisha habari hii hadi blog hii ilipolalamika wakabandika picha kama nusu saa baada ya kutoa lalamiko. Tunaipelekea wapi nchi yetu? Tumefikia mahali tunatawaliwa kihuni na kipuuzi hivi! Hii maana yake ni kwamba ziara hii ni ya shaka tupu. Je ziara za siri namna hii zina manufaa kwa taifa? Tukimuita Vasco da Gama wapambe na waramba viatu wake wanalalamika kuwa tunamkosea adabu. Tutamheshimuje mtu asituheshimu wala asiyeheshimu sheria wala taratibu? Tutamheshimuje mtu anayejitembeza kama changu akidhalilisha taifa letu? Tutamheshimu kwa lipi iwapo ameshindwa kulhali? Nani anaweza kumheshimu ombaomba anayetembea juu ya dhahabu akiomba ugolo? Ingawa juzi mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) profesa Ibrahim Lipumba aliwalaumu Benjamin Mkapa na Andrew Chenge kwa kuiuza nchi yetu kwa wawekezaji, Kikwete anaonekana kuendeleza upuuzi huu  kwa kiwango cha kutisha. Inakuwaje rais aende ziarani kwa kodi ya wananchi halafu wasifahamishwe? Hivi ikitokea akafia huko tutaelewana? Je Kikwete anaficha nini? Imefikia mahali rais wetu anafanya mambo kana kwamba anakwenda kuzini kutokana kuficha wajumbe anaoandamana nao? Blogu hii imelalamikia mchezo huu mchafu bila majibu. Hata hivyo, hatutaacha kupiga kelele. Hata wakinyamaza wanapata salamu zetu. Zinawaudhi na kuwatisha hata kama hawasemi. Kuna haja ya wajuzi wa mambo kufuatilia alichokwenda kufanya Kikwete Kuwait ambacho amekifanya siri. Anaweza kutuficha leo. Kesho tutajua. Maana akishaingia mikataba yake ya kijinga tutawaona hao wanaomhangaisha hadi anafanya vitu ambavyo hata hayawani hawezi kufanya mitaani kama siyo kwenye mbuga zetu. Nani mara hii kasahau kuwa waarabu wanaongoza kwenye kufanya ujangili uliohalalishwa na watawala mataahira wakikuwadiwa na Abdulrahaman Kinana katibu mkuu wa CCM? Nani amesahau kashfa ya Loliondo ambapo iliuzwa kwa mwarabu toka Oman ambaye ni rafiki na mshirika wa Rostam Aziz aitwaye Brig. Ali uliofanywa nwa Ali Hassan Mwinyi na mramba viatu wake Muhidin Ndolanga hadi kusababisha kifo cha Stan Katabalo alipofichua hujuma hii? Sitashangaa kusikia kuwa Kikwete amesaini mikataba ya kuruhusu Kuwait wawekeze kwenye kilimo cha kuzalisha chakula kwa ajili ya watu wao. Maana nchi nyingi za ghuba kutokana na utajiri wa mafuta zimeigeuza Afrika sehemu ya kuzalishia chakula cha watu wake wakati wenye nchi wanaishi ima kwa kutegemea misaada au kufa njaa. Ni aibu ya namna gani rais wetu kufanya vitu kama vile hatuna hata mtu mmoja mwenye akili wa kumshauri.
Hakika rais wetu ni ajali mbaya ya kihistoria ambaye madhara yake yatachukua mamia ya miaka kuondoka.

5 comments:

Jaribu said...

Alijua kuna bomu litalipuka kanisani ndio akakimbia nini? Let's face it, huyu mtu ameingia Ikulu atajirike, asafiri na kutesa awezavyo. Hana hata chembe yoyote ya uongozi. Jamaa ni bozo tu!

NN Mhango said...

Jaribu jamaa katugusa pabaya. Naamini na Mtwangio lazima atakuja hapa atwange. Jamaa anatia kinyaa. Who knows? Maana ni juzi juzi Msigwa kasema kuwa Kikwete ndiye yuko nyuma ya huu ugaidi kwa vile anaufuga. Je angeufugaje kama hana faida nao? Tungojee zawadi ya totoz wabovu wa kimanga atakazopewa ili waje kusimamia wizi wa jamaa zao.

mtwangio said...

Mwalimu Nyerere alisema"CCM si mama yangu wala si baba yangu"je alikua anakusudia nini?ukweli ulio wazi ni kwamba CCM tangu Mwalimu Nyerere aondoke imebaki kuwa ni mkusanyiko wa kikundi cha mafisadi,wabaridhifu,wezi,wachumia matumbo yao na familia zao na kuyalinda masilahi ya mabwana zao wa nje na wa ndani.CCM wanaiendesha nchi yetu katika utaratibu wa kibabe na wa kimafia!

Kwa hiyo tangu awamu ya pili hadi ya kikwete kila Rais amekuja na viroja vyake vya kuibomoa nchi na kuwadhalilisha wananchi.Huyu Rais tuliyekuwa naye sasa hivi tuna haki ya kumlaumu kumpigia makelele kwa vile yeye ndiye anaebeba jukumu la kubwa la kuinua nchi au kuididimiza na katika miaka yake ya utawala wake tumeshaona tu kwamba anaididimiza nchi kwa masilahi yake na masilahi ya wachache wanaonufaika nae.Lakini ikiwa tutamlaumu yeye peke yake tutakuwa tunamuonea je hawa washauri ambao wanaomshauri katika kuindesha nchi nao tuwaiteje?Je hawa mawaziri wake anaowachagua je wapo kwa ajili ya nani?Je wao ni akina "ndio muheshimiwa,ndio muheshimiwa"hata wanapoona wazi kabisa Rais huyu anatupeleka sipo?Au ndio kila mtu anaangalia masilahi yake na masilahi ya familia yake badala ya kuiweka nchi mbele na katiba kabla ya chochote kile?Maswali mengi kuliko majibu.

Utawala wa CCM wametugawa katika utaratibu wa mabox kwa maana sisi na wao na wananchi ni wao hatuna thamani mbele yao,hawatuwekei mahesabu ya kwamba tunaweza kufanya mabadiliko ya kuwaondoa madarakani sisi wananchi kwao wao ni tupo tupo tu kama kundi la Mbogo hawatuheshimu hata kidogo!

Wakati umeshafika kwa wananchi wa Tanzania kufanya mabadiliko ya nchi yao kwa masilahi ya wao wenyewe ifike wakati kwamba msemo huu wa "Government of the people, by the people, for the people" uchukue nafasi yake katika ukweli wa ardhini.Na CCM ni rotten egg inabidi lichimbiwe chimo na kuzikwa"

Mhango,swala la fukuto la kidini umelishaliongelea sana na umeshahadharisha sana nami nakubaliana nawe asili mia 100,lakini nachoshindwa kuelewa kwa nini viongozi wetu wamelikalia sana kimya jambo hili au wamekua na hofu na kuliingilia hadi leo hii limeshakua ni bomu la kutegwa?je hafu yao ni nini?je tukidai kwamba kuna conspiracy theory ambapo viongozi wa nchi hiyo wanataka kutufanya wajinga watushughulishe na mapambano ambayo si halali badala ya kuwakalia wao shingoni?

Hofu yangu kubwa hapo sasa ni kuwepo Boko Haram ya Tanznia.Watanzania hatuna masilahi yoyote yale ya kupigania udini au ukabila hali hiyo itazidi tu kututenganisha na kulifanya taifa hilo lisiwe na amani tena na wanasiasa kuendelea kutukandamiza.

NN Mhango said...

Mtwangio kuhusiana na udini hewa kutumika kama zana ya kuwaondoa watanzania kwenye madai ya msingi inawezekana.
Maana kila wanapobanwa lazima waje na kila aina ya sanaa. Juzi tulipokuwa tukiongelea madudu ya Mtwara na gesiasili walianzisha la Kibanda ambalo walipoona linazidi kuwasumbua wakaja na hili la kulipuka mabomu makanisani. Nijuacho ni kwamba usanii wao una mwisho. Hata akina Gaddafi walikuwa mabingwa wa usanii kama huu hadi walipokaukiwa wakaishia kuuawa kama vibaka. Na kweli walikuwa ni vibaka sema tofauti na vibaka wa kawaida ni kwamba wao walikuwa ni mibaka yenye madaraka. Hata hawa wetu wanatapatapa siku yao itafika na tutawaona wakiporomoka kama mende. Leo wataua ndovu zetu wakiongozwa na Kinana, watauza madini yetu wakiongozwa na akina Karamagi, watahujumu nishati yetu wakiongozwa na akina Lowassa na Rostam, watafanya kila watakalo lakini iko siku iso jina itafika arobaini yao.
Hili la washauri wa Kikwete ni kwamba nao umewaonea. Hivi unategemea kipofu aongoze wenye macho au vipofu wenzake? Kama washauri na watendaji wenyewe ni matapeli kama akina Salva Rweyemamu unategemea nini?
Hata hao mawaziri usitegemee chochote iwapo wengi ni washirika na washikaji zake. Hakuna siku nilitaka kupasuka kama alipomteua wakili mwizi aitwaye Mwanaidi Maajar kuwa balozi Uingereza na hatimaye Washington. Ukienda kwa wakuu wa wilaya na mikoa hata mahawara utawakuta! It is surreal1

mtwangio said...

Mhango,kuna point muhimu sana umeielezea ambayo tunatakiwa sisi watanzania tuwe makini kwa hili ulipoandika " Sitoshangaa kusikia kuwa Kikwete amesaini mikataba ya kuruhusu Kuwait wawekeze kwenye kilimo cha kuzalisha chakula kwa ajili ya watu wao. Maana nchi nyingi za ghuba kutokana na utajiri wa mafuta zimeigeuza Afrika sehemu ya kuzalishia chakula cha watu wake wakati wenye nchi wanaishi ima kwa kutegemea misaada au kufa njaa."Ninaamini na nitaendelea kuamini kwamba historia inaandikwa sababu ni ardhi na vita vinapigwana kwa sababu ya ardhi.Ardhi ndio hazina ya rasilimali zote muhimu ambazo mwanadamu anazihitaji kwa kuweza kuyaendesha maisha yake.Na kuna madai yanayosema kwamba mvutano na mgogoro mkubwa wa kimataifa siku za usoni kutalalia upande wa maji na ardhi,ukweli mataifa makubwa wanalijua hilo na ndio maana wanaufanya ulimwengu wa tatu ni kinyang'anyiro cha kupigania masilahi yao katika kila njia.Naam waarabu wa Ghuba wanajua fika kwamba siku moja utajiri wa mafuta utamalizika na wameshalenga upande wa chakula Afrika walijitahidi kwa kila njia kuona kwamba Sudani ibaki kma taifa moja ukiachilia mbali utajiri wa mafuta wa sudani ya kusini lakini walikua na mwelekeo wa kuifanya Sudani kama ghala lao la chakula kwa kuwekeza katika sekta hiyo ya ukulima ili wasife na njaa ciku za usoni.

Wairani wakati wa mwinyi walipewa bonde la Rufiji kuweza kulifanyia kazi kwa kilimo na mapka wakati huu sielewi kama taifa na wananchi wanafaidika na mradi huo wa bonde la Rufiji,ukiachilia mabali akina Carters,Clintons na Bushes ambao wana maheka mengi tu kwa hoja ya kuwekeza katika kilimo na sijui taifa na wananchi wanafaidika kivipi na miradi hiyo.kwa hiyo ni kweli hakutokuwa na mshangao kwa kutia saini mkataba kwa upande wa uwekezaji wa kilimo na hususa Kuwait wana foundation yao ambayo inalenga sana kwa upande huo katika ulimwengu wa tatu kwa hoja ya misaada.

Mimi sina kipingamizi kuwekeza katika sehemu yoyote ile kwa faida ya nchi na wananchi lakini iwapo kuwekeza kwa faida ya watia mikataba na wenye kuwekeza bila ya nchi kunufaika na wananchi wake kama ilivyo katika sehemu kubwa la uwekezeji hili sikubaliani nalo aslani hasa upande huu wa ardhi tusisahahu ukezezaji wa kilimo ulimaji wake ni wa kisasa na vifaa vya kisasa na sidhani kama watanzania wananufaika na ajira katika sehemu hiyo mana kuna utaratibu kwa zone zingine wawekazaji huwa wanawaleta cheap labour wao kutoka katika nchi masikini na hata kama wataajiri wananchi utakuta kwa oder ya serikali wananchi hao wanalipa pesa mbuzi tu na hata kama kutakua na mjuzi sawa na ujuzi aliekua nao mjuzi wa muwekazaji basi uwezi kuamini tofauti ya mshahara kwa wajuzi hawa wawili.

Nimedokezewa na mtu wa karibu sana na zone ya ardhi kwamba serikali imepokea msaada mkubwa wa kuwekeza katika sekta ya ardhi sasa wanachotaka kufanya ni kuleta sheria ya kwamba mtanzania yoyote(mwananchi wa kawaida)anaemliki ardhi kuanzia eka 10 na kuendelea kama hana uwezo wa kuindeleza ardhi hiyo basi serikali itaitwaa kwa masilahi ya taifa!!!!!Je ni masilahi gani hayo ya taifa kama si kupora ardhi ya mtanzania masikini na kujilimbikizia wenyewe au kuwapa hao wanaowaita wawekezaji?Kwa nini serikali isimkopeshe matanzania huyu masikini ili aweze kuindeleza ardhi yake kwa masilahi ya nchi,yake yeye mwenyewe na wananchi wenzake?

Je watanzania wanaweza kuitetete ardhi yao na hawa ambao wanataka kuanzisha FEUDAL SYSTEM ambayo imeshakuwa ni sehemu tu ya somo la historia?Na kama hatukuangalia tutakufa kweli na njaa na umasikini>