Friday, 24 May 2013

Siku Mbwa alipombusu Simba!

Kuna kipindi wanyama ni wema na wakweli kuliko wanadamu. Simba akishiba hana haja ya kuua na kuficha kama binadamu wanavyotajirika na kuficha pesa Uswizi huku wanadamu wenzao wakifa kwa magonjwa yanayotibwa. Kinachokera sana ni ile hali ya hawa wanaoficha pesa nje kuwaibia maskini. Tunao watawala wanaopenda wachukuliwe kama Simba wakati hakika si Simba kitu bali Panya kutokana na tabia zao za kipanya panya. Kitendo hiki hapa juu kina mafunzo mengi yanayomsuta binadamu hasa wale wanaowatumia wenzao kujitajirisha na kuwaacha wafe makapuku wakati pesa yao ikiozea nje.

No comments: