Wednesday, 15 May 2013

Du hii kali Kenya yaongoza kwa uvumbuzi kurudi nyuma!

Ingawa toroli  linasifika hadi kuitwa ambulance, ukweli ni kwamba uvumbuzi huu haumsaidii mwananchi aliyetapeliwa na kuhujumiwa na wanasiasa. Wanapopata vitu kama hivi huridhika na kusahau kupambana na majambazi wenye madaraka waliowaahidi maisha bora wakaishia kuwapa maisha balaa. Hivi karibuni kulivumbuliwa toroli linaloitwa ambulance. Je ambulance ambayo injini yake ni binadamu inaweza kutuvusha? Inashangaza kwenye karne ya 21 Afrika inagundua nyenzo zilizotumika wakati wa ujima. Huwa najiuliza: Hawa akina mama wanaodhalilishwa kwenye mikokoteni kama mikungu ya ndizi wangekuwa wake wa wakubwa wangeshangilia janga hili linaloitwa uvumbuz? Je uvumbuzi huu ni hatua ya maendeleo au nyenzo ya kuwanyamazisha wanyonge na kuwafanya waridhike na mateso yao?

No comments: