Thursday, 23 January 2014

Kikwete azidi kuwaokoa wenzake wa kashfa ya EPA

Ajay Somai

Akiwa na zigo la kumlinda na kumhami mshirika wake mkuu kwenye kashfa ya Richmond, Edward Lowassa na yule wa kashfa ya EPA Rostam Aziz, rais Jakaya Kikwete ameonyesha kutowasahau wenzake wanaodaiwa kushirikiana naye kwenye kashfa ya EPA. Vyombo vya habari vinaripoti kuwa mmoja wa wahalifu waliofungwa kwa kosa la kukwapua pesa ya EPA, Ajay Somai ameachiwa kwa msamaha wake hivi karibuni pamoja na kufungwa kifungo kifupi cha miaka miwili. Japo Kikwete amekuwa kimya kuhusiana na shutuma dhidi yake kuhusiana na kashfa ya EPA iliyompatia pesa ya kuhonga na kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, amekuwa akifanya vitu vyake nyuma ya pazia kuhakikisha wenzake hawakamatiki wala kuadhibiwa.  Na kama wakiadhibiwa kama ilivyotokea kwa Somai wanaachiwa kwa msamaha wake. Wakati akifanya hayo anaendelea kuwaaminisha watanzania kuwa anaweza kuwaletea maisha bora kwa wote wakati ni uongo na sanaa tupu.Kwa habari zaidi GONGA HAPA.

No comments: