Saturday, 25 January 2014

Hawking amenichanganya na kujichanganya sijui ndiyo anachanganyikiwa au mimi?


Mwana sayansi mlemavu Stephen Hawking wa Uingereza ni super star kwa vigezo vyote. Ni binadamu aliyeitikisa duni alipokuja na dhana yake ya Black Holes akimaanisha kuwa kuna matundu makubwa angani ambayo yanaweza kuwa na siri ya jinsi dunia ilivyoumbwa. Hawking ameandika vitabu vingi na kuuza sana duniani juu ya sayansi hii. Amekuwa maarufu kiasi cha kukaribia ushufaa wa akina Einstein na Sir Isaac Newton.
Hivi karibuni Hawkin aliwaacha wengi hoi alipojipinga akisema kuwa dhan yake ya Black Holes ni uongo kwani hakuna na wala haamini katika Black Holes zake. Badala yake amekuja na dhana nyingine mpya iitwayo Mind Bending Theory. Sie tunaweza kuiita Mind Boggling Theory karibia na mazingaombwe. Hiyo nayo ni sayansi au tuseme sanaa. Kwa habari zaidi GONGA HAPA.

No comments: