The Chant of Savant

Wednesday 29 October 2014

Jana nilipokea kitabu cha Dk Sengondo Mvungi

Japa nilipokea nakala ya kitabu juu ya marehemu Dk Sengondo Mvungi Breathing the Constitution toka Tanzania. Kilitumwa na Kituo cha Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre-LHRC). Kwa namna ya pekee nawashukuru LHRC kwa kunitumia nakala ya kitabu hichi ukiachia mbali kutumia moja ya makala zangu kwenye kitabu husika  uk. 86. Namshukuru Dk Elen Kijo-Bisimba aliyehakikisha natumiwa nakala hii. Pia nimepata fursa ya kushiriki kwenye kueleza maisha ya nguli huyu wa sheria na haki za binadamu aliyeuawa kwenye mazingira ya kutatanisha kipindi alipohitajika kutoa mchango wake kwenye upatikanaji wa katiba safi ya wananchi ambayo hata hivyo imechakachuliwa na mafisadi ili kulinda uoza wao. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Dk Sengondo Mvungi. AAAMIN.

4 comments:

Anonymous said...

Twende Burkina Faso nako Wabunge wavivu wa kufikiri wamelewa chakari, Nilifikiri kilevi cha madarka kinanyweka hapa kijiweni kwetu pekee, kumbe hiyo pombe inanyweka katika nchi nyingi tuu za kiafrika ikijumuisha Tangenia kutoka Bango yetu tukufu hapa Didimia!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon umenichekesha kwa bangi zako. Kimsingi, kigeugeu na zandiki Blaise Compaore amekwisha rasmi leo. Wenzake wameishachukua madaraka na anangojea kulipia dhambi ya kumuua kamanda Thomas Sankara. Usicheze na kanywaji kaitwako madaraka ndugu yangu hasa kanapochanganyika na bangi iitwayo ufisadi.

Anonymous said...

Kuongezea tuu hapo Mwalimu, Thomas Sankara ni mzalendo kweli, siyo hawa wanafiki na wazandiki tulionao hivi sasa miongoni mwao wengi.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ano usemayo ni kweli. Kuna haja ya watanzania kuamka na kuondoa hii Ebola ya kisiasa inayolisumbua taifa haraka iwezekanavyo hasa ikizingatiwa kuwa watawala si chochote wala lolote bali a bunch of cowards.