Tuesday, 14 October 2014

Rais anapohongwa saa ya dola 5,000!


Kuna wakati ukisikia tuhuma zinazowakabili viongozi wa Kiswahili unatamani ulie au hata ujitoe roho. Miaka michache iliyopita zilizuka tuhuma ambazo kwa kiasi fulani zilionekana kuwa za kweli kuwa rais Jakaya Kikwete alihongwa suti na tapeli mmoja aliyejifanya mwekezaji. Mwaka huu tena kabla ya kuachia ngazi mwakani imefumka kashfa ambapo rais amehongwa saa aina ya Rolex ambayo hata kwa per diem yake anaweza kununua. Saa hiyo inasemekana alihongwa na tapeli mmoja aliyemteua kuwa balozi wa heshima wa Tanzania Marekani jambo ambalo tulilipigia kelele. Je  huyu tapeli anayedaiwa kuwa mbioni kupata mradi wa doola milioni 35 ni kuwadi tu  na msimamizi wa biashara za bwana mkubwa au ni tapeli wa kawaida aliyemuingiza mjinga fulani mjini? Kama ni kweli au la? Hata kungekuwa na shaka, rais anapojiruhusu kuwa rahisi kiasi hiki lolote lawezekana. Nakumbuka jinsi rais wa zamani Daniel arap Moi alivyohongwa pesa ya Kenya shilingi milioni tano tena zenye picha yake akaitumbukiza nchi kwenye kashfa iliyoponea kidogo kuifilisi ya Goldenberg ambayo inahusishwa na jizi la IPTL Harbinder Sethi Singh. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

2 comments:

Anonymous said...

CCM
Chukuwa Chako Mapema

NN Mhango said...

Anon Nadhani ni Chukua Chao Mapema maana wezi hawa hawana chao wanachochukua zaidi ya kuibia umma.