Thursday, 23 October 2014

Uprofesa wa Kikwete je ni aina mpya ya rushwa?

Rais Kikwete akipewa uprofesa wa heshima
Ukiwa na kasoro wengi wanaitumia kukugeuza kinyago hata mwanasesere. Wanakuchezesha kama kile kinyago cha Joyce Wowowo. Hivi Kikwete na uprofesa tena wa kilimo wapi na wapi? Je hawa kuna kitu wanachotaka kama vile kupewa ardhi wakalime chakula cha kulisha watu wetu. Je hii nayo si aina mpya ya rushwa? Kama hii si rushwa, mbona huo udaktari na uprofesa wa heshima hawapewi viongozi wa mataifa makubwa? Sijawahi kusika Obama kazawadiwa uprofesa wala Putin udaktari. Kuna haja ya kuwa na katiba inayozuia viongozi malimbukeni kuhongwa upuuzi kama huu. Kama unataka uprofesa au udaktari kasome.

4 comments:

Anonymous said...

Inashangaza Tena sana kupewa PhD na u profesa na zenye ufisadi na rushwa duniani
Kama kweli ni mtu safi mbona hapewi nishani ya Nobel kama Malala

NN Mhango said...

Anon usemayo ni kweli.Angalau mhusika mwenyewe angekuwa mtu msomi na mtu safi. Nishani apewe mtu ambaye utawala wake unasifika kwa kuwaua na kuwaibia raia wake!

Samwel Leonard said...

Ukisikia Nchi yenye maajabu bhana ni Tanzania. Kuna vitu havijawahi kutokea kokote Ulimwenguni, ila Tanzania tu.

Huyu jamaa amepewa uprofesa tena? Siku zijazo atapewa daraja lingine la elimu ambalo liko juu ya uprofesa; na hiyo itakuwa "exclusively made in Tanzania doctorate degree". hahahah. Kikwete, kasome baba!!

NN Mhango said...

Samweli umenena vema. Atakuwa professor emeritus kabla ya kuwa philosopher. Baada ya hapo nadhani ataitwa saint of knowledge who knows. Mtu mwenye kilaza hakuna mfano.