Friday, 1 April 2016

BREAKING NEWS GOOD NEWS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 We are one

Ndugu jamaa, marafiki na wasomaji kwa ujumla,
Nina furaha -kwa niaba ya familia -kuwatangazia kuwa usiku wa kuamkia leo majira ya saa sita kama na sekunde kadhaa tumajaliwa watoto mapacha NGWAZI na NKWAZI. Bi mkubwa ametuletea makamanda hawa wawili na amejifungua salama salimini njiani akielekea hospitali ya Boundary Trails MB. Tunamshukuru Mungu na kuwakaribisha ndugu jamaa na marafiki kushiriki furaha hili. Mara nyingi, ni nadra kupata mapacha tena wa mwisho. Dada na Kaka zao wameishakwenda kuwaona na kuwakaribisha. Nkuzi na Jr wameshangaa na wanasema: "Dad and Mom, you have brought yet new cool toys.
 Habari ndiyo hiyo.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Naweza nikasema HABARI HII NI NJEMA SANA NA PIA HONGERENI SANA KWA KUWA FAMILIA KUBWAAA...Ila...Kaka Mhango hata picha ya hao wageni mapacha hakuna?

Anonymous said...

Hongereni sana!

NN Mhango said...

Tunawashukuru mliotutakia kila la heri na kutupongeza ingawa taarifa hii ilitolewa katika kuadhimisha siku ya wajinga duniani. Kila la heri.
Utawala.

Anonymous said...

Hongera Mwalimu na Bii Mwalimu kwa kutuletea hawa-watakaochukua atapotuachia Mugful.

NN Mhango said...

Anon nakushukuru ingawa hawa jamaa hawapo kusema ule ukweli. Ilikuwa ni kiburudisho cha siku ya wajinga. Hata hivyo, bado tunao vitegemezi vingine vitakavyoushika ukanda vilivyo baada ya kufuzu masomo yao.