Sunday, 31 July 2016

Happy Birthday Nkwazi Mhango Jr.Jana ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa kitindamimba wetu Nkwazi Mhango Jr katikati. Alitimiza miaka minne jana akiwa anajiandaa kuanza Kindergarten mwakani inshallah. Junior alijumuika na dada zake na kaka yake pamoja nasi. Zawadi yake kwa siku hiyo ilikuwa kumrusha kwa ndege kwa saa moja jambo ambalo huwa analipenda sana.

3 comments:

Anonymous said...

Salamu Mwalimu Mhango.
Wakati mwingine ninakuwa na itikadi ya kwamba tungekuwa wenye kusubiri mpaka mmoja wetu amalize safari yake ya hapa duniani kisha ndio tuanze kuısherekea siku yake ya kuzaliwa kwa vile tutakuwa tu tunasherekea kwa kuja kwake hapa duniani,mchango wake aliechangia na kutuachia katika maisha yetu na hatimae kuikumbuka pıa na kuisherekea siku ambayo aliyosafiri kwa kuiacha hii dunia.

Kwa kusema hayo Mwalimu Mhango.wache nikupongeze wewe na mshirika wako wa maisha na watoto wenu na kushirikiana nanyi katika siku hiyo ya kuzaliwa kwa kitinda mimba wenu Nkwazi Mhango Jr.Mwenyezi Mungu ampe afya njema na bora ambayo itaambatana na maisha mema yenye heri,baraka na mafanikio kwake na kwa nyiny, wazazi wake na kwa ndugu zake.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera shangazi wangu Nkwazi jr kwa kutimiza miaka minne. Pia hongera wazaz/walezi. Nkwazi uwatii wazazi pia walezi hii ni siraha yako ya maisha. Ni mimi shangazi yako...

NN Mhango said...

Anonymous na da Yasinta tunawashukuru kwa pongezi zenu na salamu zake zitafika Hilo la kwanza alilotoa anon linafikirisha na siwezi kulitolea jibu kwa kurupuka zaidi ya kuliweka akilini ili siku nyingine lau nione ni wapi pa kulifanyia kazi.