Wednesday, 13 July 2016

Tusinunue ndege kwa 'madesa'

 Image result for photos of bombardier c 400
           
            Neno desa au kuchota ujuzi, taarifa au majibu bila kuyafanyia kazi na kuyatumia kwenye kazi yako au kunakiri bila kufuata sheria au kukwepa sheria–kabla ya kuchaguliwa kwa rais John Pombe Magufuli–lilikuwa limefungiwa kwenye kuta za madarasa na vyumba vya mihadhara ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM). Hata hivyo, baada ya kuchaguliwa Magufuli ambaye ni mhitimu wa shahada tatu zote toka UDSM, neno desa limeingia kwenye msamiati tawala (mainstream).
Hivi karibuni vyombo vya habari vilimkariri Magufuli si zaidi ya mara moja akitumia neno desa kuanzia alipohutubia jumuia ya wana UDSM hadi alipomkaribisha rais wa Rwanda Paul Kagame aliyesema amempa desa au mbinu ya kununua ndege mbili kwa mpigo. Magufuli alisema, “Mwezi wa tisa tutakuwa tumepata ndege mbili mpya, nimepewa namna nzuri ya kupata ndege hizo na Rais Kagame baada ya kuwatuma maofisa wake ambao ni wataalam wa ndege waje na kunipa desa.”
Si vibaya kwa viongozi kupeana mbinu za kufanya mambo ingawa hili linatia shaka kwa namna moja au nyingine. Pia linaacha maswali mengi kuliko majibu. Je Tanzania–pamoja na kupata uhuru zaidi ya miaka hamsini iliyopita–haina wataalamu wake wenye ujuzi na wa kuaminika kufanya kazi hiyo hadi tukope wataalamu toka Rwanda? Kwa mujibu wa matamshi ya Magufuli ni kwamba Tanzania haina wataalamu wa kutafuta na kununua ndege jambo ambalo ni aibu kwake na taifa.  Vyema, kuwa Magufuli amepewa desa; je amepewa na wataalamu wa kuendesha ndege husika? Je wataalamu wetu wanaolipwa kumshauri Magufuli wanalipwa kwa kazi gani kama rais analazimika kukopa washauri na wataalamu toka nje?           Je hilo shirika litaendeswa na hao wataalamu wa Kagame?
             Kisa cha Magufuli kupewa “desa” kinanikumbusha kisa cha jamaa mmoja aliyeomba ng’ombe kwa rafiki yake ili naye akafuge na kupata maziwa, mbolea na nyama. Hata hivyo, jamaa huyu alikuwa na kasoro nyingi; hakuwa na uwezo wala ujuzi wa kumtunza ng’ombe aliyezawadiwa. Hivyo, alipoletewa ng’ombe alisema, “Asante sana rafiki yangu. Hata hivyo, naomba mtu wa kumswaga huyu mnyama.” Mwenyeji wake alimjibu, “Umepata. Je una jingine?” mgeni alijibu, “Je nitapata wapi mtu wa kumkamua, kumlisha na kumtunza?” mwenyeji alisita kidogo na kusema, “Ngoja kidogo” alimwambia yule mtumishi aliyekuwa ameleta ng’ombe, “mrudishe huyo ng’ombe kwa wenzake hadi jamaa atapopata ujuzi na uwezo wa kumtunza atajua jinsi ya kuja kumchukua na kummilki.” Jamaa alibaki kujishangaa na kushangaa namna alivyojiaibisha.  Kwa ufupi ni kwamba; sitashangaa ndege husika zikaishia kuuzwa kwa hao hao manoadesa kwao. Hili liko wazi na wenzetu wanalijua. Kwani wengi wamezaliwa na kukulia na kusomea Tanzania. Mbali na hili, hata ukiangalia tulivyoinga kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki kijinga, kuna uwezekano Tanzania ikaishia kuwa kimbilio la watu wasio na ardhi au kuja kuchuma na kurejea kwao. Mimi huwa siamini katika mashirikisho na jumuia za kimajimbo bali muungano wa haraka na moja kwa moja wa Afrika. Je muungano wa Afrika unawezekana wakati kila rais anang’ang’ania ulaji wake? Hili humu si mwake leo.
Japo Magufuli anasherehekea na kujisifia kupewa desa, anapaswa kufikiri na kuangalia mbali zaidi hasa usawa huu ambapo kila nchi inatafuta kila fursa kuwanufaisha watu wake baada ya nchi za kiafrika–kwa ujinga, uroho, upogo na kongwa za kikoloni zilikataa kuungana na kuwa nchi moja kama Marekani au China.  Watanzania kukiri kuwa hamna ujuzi na kuwaamini hawa watoa madesa, mmewapa kishawishi cha kuanga kujiandalia kurejesha ng’ombe zizini hadi mtakapopata uwezo na kuwa tayari kummlilki na kumtunza ng’ombe husika. kama shida ni wataalamu, kwanini Magufuli hakuwatuma wataalamu wake kwenda Rwanda kujifunza badala ya kuwaamini kazi wanyarwanda ambao hawako chini ya kiapo chochote wala uwajibikaji kisheria wa kuitumikia Tanzania? Kwanini hatutaki kujifunza tokana na wale tuliwatengeneza tukidhani ni watanzania wakaishia kutuacha Solemba?  Kwanini watanzania tunakuwa wepesi kufanya mambo muhimu kuwa ya mzaa kama kuamini uchumi wetu kuwa mikononi mwa wageni kama inavyozidi kubainika ambapo matapeli wa kigeni huja nchini wakijifanya wawekezaji wakiwa mikono mitupu na kuondoka na utajiri wa kutisha wakati watu wetu wakiwa maskini?
Kama tutakuwa wakweli, nchi iliyopata uhuru zaidi ya nusu karne ahitaji msaada hata wa namna ya kununua ndege. Hii maana yake–kama inashindwa kuwa na wataalamu wa kununa ndege–maana yake haina hata wataalam wala mipango madhubuti ya kuendesha shirika la ndege linalokusudiwa kuanzisha? Je tatizo ni wataalamu au uzalendo na mfumo bora? Mbona baadhi ya wataalamu wa Rwanda wamesoma tena bure hapa Tanzania wakijionyesha kama watanzania wakati ni wanyarwanda? Ajabu hatukuwachukulia hatua ikizingatiwa kuwa nchi yetu hairuhusu uraia wa nchi mbili. Je hawa waliotukimbia wataweza kutusaidia kweli? Mjinga ni yule anayeng’atwa na nyoka mara mbili kwenye shimo moja.
Tumalizie kwa kumshauri rais Magufuli kufikiria upya kuhusiana na mpango wake wa kuazima wataalamu toka Rwanda au kwingineko. Kununua ndege hakuna haraka. Anapaswa kutuma wataalamu kujifunza si Rwanda tu bali Kanada zinakotengenezwa ndege husika. Kama tunashindwa na jambo dogo ambalo makampuni ya watu binafsi kama lile la bilionea Richard Bronson yamefanya, nini maana ya kuwa huru akiri bila kufuata sheria au kukwepa sheria–kabla ya kuchaguliwa kwa rais John Pombe Magufuli–lilikuwa limefungiwa kwenye kuta za madarasa na vyumba vya mihadhara ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM). Hata hivyo, baada ya kuchaguliwa Magufuli ambaye ni mhitimu wa shahada tatu zote toka UDSM, neno desa limeingia kwenye msamiati tawala (mainstream).
Hivi karibuni vyombo vya habari vilimkariri Magufuli si zaidi ya mara moja akitumia neno desa kuanzia alipohutubia jumuia ya wana UDSM hadi alipomkaribisha rais wa Rwanda Paul Kagame aliyesema amempa desa au mbinu ya kununua ndege mbili kwa mpigo. Magufuli alisema, “Mwezi wa tisa tutakuwa tumepata ndege mbili mpya, nimepewa namna nzuri ya kupata ndege hizo na Rais Kagame baada ya kuwatuma maofisa wake ambao ni wataalam wa ndege waje na kunipa desa.”
Si vibaya kwa viongozi kupeana mbinu za kufanya mambo ingawa hili linatia shaka kwa namna moja au nyingine. Pia linaacha maswali mengi kuliko majibu. Je Tanzania–pamoja na kupata uhuru zaidi ya miaka hamsini iliyopita–haina wataalamu wake wenye ujuzi na wa kuaminika kufanya kazi hiyo hadi tukope wataalamu toka Rwanda? Kwa mujibu wa matamshi ya Magufuli ni kwamba Tanzania haina wataalamu wa kutafuta na kununua ndege jambo ambalo ni aibu kwake na taifa.  Vyema, kuwa Magufuli amepewa desa; je amepewa na wataalamu wa kuendesha ndege husika? Je wataalamu wetu wanaolipwa kumshauri Magufuli wanalipwa kwa kazi gani kama rais analazimika kukopa washauri na wataalamu toka nje?           Je hilo shirika litaendeswa na hao wataalamu wa Kagame?
             Kisa cha Magufuli kupewa “desa” kinanikumbusha kisa cha jamaa mmoja aliyeomba ng’ombe kwa rafiki yake ili naye akafuge na kupata maziwa, mbolea na nyama. Hata hivyo, jamaa huyu alikuwa na kasoro nyingi; hakuwa na uwezo wala ujuzi wa kumtunza ng’ombe aliyezawadiwa. Hivyo, alipoletewa ng’ombe alisema, “Asante sana rafiki yangu. Hata hivyo, naomba mtu wa kumswaga huyu mnyama.” Mwenyeji wake alimjibu, “Umepata. Je una jingine?” mgeni alijibu, “Je nitapata wapi mtu wa kumkamua, kumlisha na kumtunza?” mwenyeji alisita kidogo na kusema, “Ngoja kidogo” alimwambia yule mtumishi aliyekuwa ameleta ng’ombe, “mrudishe huyo ng’ombe kwa wenzake hadi jamaa atapopata ujuzi na uwezo wa kumtunza atajua jinsi ya kuja kumchukua na kummilki.” Jamaa alibaki kujishangaa na kushangaa namna alivyojiaibisha.  Kwa ufupi ni kwamba; sitashangaa ndege husika zikaishia kuuzwa kwa hao hao manoadesa kwao. Hili liko wazi na wenzetu wanalijua. Kwani wengi wamezaliwa na kukulia na kusomea Tanzania. Mbali na hili, hata ukiangalia tulivyoinga kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki kijinga, kuna uwezekano Tanzania ikaishia kuwa kimbilio la watu wasio na ardhi au kuja kuchuma na kurejea kwao. Mimi huwa siamini katika mashirikisho na jumuia za kimajimbo bali muungano wa haraka na moja kwa moja wa Afrika. Je muungano wa Afrika unawezekana wakati kila rais anang’ang’ania ulaji wake? Hili humu si mwake leo.
Japo Magufuli anasherehekea na kujisifia kupewa desa, anapaswa kufikiri na kuangalia mbali zaidi hasa usawa huu ambapo kila nchi inatafuta kila fursa kuwanufaisha watu wake baada ya nchi za kiafrika–kwa ujinga, uroho, upogo na kongwa za kikoloni zilikataa kuungana na kuwa nchi moja kama Marekani au China.  Watanzania kukiri kuwa hamna ujuzi na kuwaamini hawa watoa madesa, mmewapa kishawishi cha kuanga kujiandalia kurejesha ng’ombe zizini hadi mtakapopata uwezo na kuwa tayari kummlilki na kumtunza ng’ombe husika. kama shida ni wataalamu, kwanini Magufuli hakuwatuma wataalamu wake kwenda Rwanda kujifunza badala ya kuwaamini kazi wanyarwanda ambao hawako chini ya kiapo chochote wala uwajibikaji kisheria wa kuitumikia Tanzania? Kwanini hatutaki kujifunza tokana na wale tuliwatengeneza tukidhani ni watanzania wakaishia kutuacha Solemba?  Kwanini watanzania tunakuwa wepesi kufanya mambo muhimu kuwa ya mzaa kama kuamini uchumi wetu kuwa mikononi mwa wageni kama inavyozidi kubainika ambapo matapeli wa kigeni huja nchini wakijifanya wawekezaji wakiwa mikono mitupu na kuondoka na utajiri wa kutisha wakati watu wetu wakiwa maskini?
Kama tutakuwa wakweli, nchi iliyopata uhuru zaidi ya nusu karne ahitaji msaada hata wa namna ya kununua ndege. Hii maana yake–kama inashindwa kuwa na wataalamu wa kununa ndege–maana yake haina hata wataalam wala mipango madhubuti ya kuendesha shirika la ndege linalokusudiwa kuanzisha? Je tatizo ni wataalamu au uzalendo na mfumo bora? Mbona baadhi ya wataalamu wa Rwanda wamesoma tena bure hapa Tanzania wakijionyesha kama watanzania wakati ni wanyarwanda? Ajabu hatukuwachukulia hatua ikizingatiwa kuwa nchi yetu hairuhusu uraia wa nchi mbili. Je hawa waliotukimbia wataweza kutusaidia kweli? Mjinga ni yule anayeng’atwa na nyoka mara mbili kwenye shimo moja.
Tumalizie kwa kumshauri rais Magufuli kufikiria upya kuhusiana na mpango wake wa kuazima wataalamu toka Rwanda au kwingineko. Kununua ndege hakuna haraka. Anapaswa kutuma wataalamu kujifunza si Rwanda tu bali Kanada zinakotengenezwa ndege husika. Kama tunashindwa na jambo dogo ambalo makampuni ya watu binafsi kama lile la bilionea Richard Bronson yamefanya, nini maana ya kuwa huru na kupoteza fedha kusomesha wataalamu ambao hawawezi hata kununua ndege?

No comments: