Wednesday, 6 July 2016

Kwa wanandoa na watarajiwa burudika na wimbo huu wa kikikuyu

 Wewe ni nyama ya nyama zangu
Wewe ni mfupa wa mfupa wangu
Wewe ndiye Mungu amenichagulia
Wewe uwe furaha ya moyo wangu

Tumekuja hapa mbele
Mbele ya wazazi wangu
Mbele ya marafiki zangu
Mbele ya kanisa ya Mungu

changu ni chako
changu ni chako
Nitaishi nawe
Si kwa muda bali milele
Tutatenganishwa na kifo


Mtunzi wa wimbo huu ni Joyce Wanjiru

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nyama ya nyama zangu eti...hakika mziki ni dawa ya moyo hata kama huelewi...nimeupenda sana.

NN Mhango said...

Nilijua nitakuibua. Kwa wakikuyu nyama ina wingi tofauti na waswahili ambapo nyama haina winge. Nimejitahidi kukumbuka kikikuyu changu na kutafsiri kama ilivyo. Kama utaweza sikiliza wimbo wake mwingine wa muthuuri yaani mwanamume anayesema ni tunu ya Mungu. Sijui mwanamke ni tunu ya nani. Silaumu kwa vile mhusika amelelewa kwenye mfumo dume.