Sunday, 24 July 2016

Makonda upangaji Nyumba za Msajili ni jipu lako


Baada ya kuondoa ombaomba, kutangaza kiama cha mashoga, mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda anakabiliwa na kibarua kingine ambacho kitapima sincerity na ithibati yake kama kiongozi wa umma. Sina shaka na uongozi wa Makonda japo mwanzoni nilikuwa na shaka naye hasa kutokana na siasa za ndani ya chama chake–hasa pale alipodaiwa kutaka kumdhalilisha waziri mkuu wa zamani Joseph Wairoba–jambo ambalo alilikanusha kwa umahiri zaidi ukiachia mbali Warioba kutolalamika binafsi.
Leo tunampa changamoto nyingine kubwa ambay–japo wengi hawapendi kuigusia –ipo na imekuwapo kwa muda mrefu. Sijui kama Makonda alishawahi kujiuliza sababu na mantiki ya jamii moja ya kiasia tena si kiasia tu bali ya kihindi kukalia karibu majengo yote ya Msajili wa Majumba ya katikati ya jiji?
Licha ya kuwa ubaguzi wa wazi wazi, kuna kila harufu ya rushwa kuhusu upatikanaji wa upangaji wa nyumba hizi ambazo–licha kuwa za bei nafuu–hazionyeshi sura ya Tanzania.
Ukiachia hayo hapo juu, kuna uwezekano wa kuwapo kwa jinai zinazoendelea ambazo zinatokana na makazi ya kibaguzi kama vile, kuficha wahamiaji haramu ambao ni wakimbizi wa kiuchumi waliojazana nchini wakiishi kinyume cha sheria ukiachia mbali kuchukua ajira na kufanya shughuli ambazo watanzania wanaweza kuzifanya.
Rejea kuwahi kufichuliwa magenge ya wasafirishaji binadamu ambapo wasichana wa kihindi walikuwa wakiletwa nchini kufanya umalaya kwa kisingizio cha kutoa burdani. Rejea tukio la mwaka jana ambapo wanaodhaniwa kuwa ni vyangudoa 22 toka nchini Nepal waliokuwa wameiingizwa nchini na kampuni ya Dhamaka Entertainment Center Limited walivyokamatwa.
Kama tutakuwa makini na wakweli, wakimbizi wa kiuchumi ni hatari kwa taifa letu kuliko ombaomba na mashoga ambao mara nyingi mambo yao ni suala la mtu binafsi na si mtandao mkubwa unaohusisha mataifa yenye watu wengi maskini na wasio na kazi wanaotumia ngozi yao kuhujumu taifa letu. Pia Makonda anapaswa kupambana na mitandao ya wazawa inayoshirikiana na wageni hawa kuhujumu taifa. Kukaa mahali popote nchini ni haki ya kila mtanzania. Inapokuja kufaidi matunda ya nyumba za umma kama vile za Msajili wa Majumba, lazima lisiwe suala la kuchagua bali kufuata sheria inayoakisi usawa wa watanzania. Bila rushwa wala ubaguzi, haiwezekani watu wa tabaka moja waishi sehemu yao maalumu halafu wawadanganye wanaowabagua kuwa wako sawa. Usawa gani huu wa bata na kuku?
Naamini Makonda amesoma historia ya ujio wa wahindi ambao waliletwa na wakoloni ili kujenga reli na baadaye wakawatumia kama watu kati wa kununua mazao ya waafrika ili kuwanyonya na kuwafanya wawe maskini ili iwe rahisi kuwatawala kwa lengo na kuwanyonya milele. Ni bahati mbaya, baada ya kupata uhuru–tokana na huruma ya baba wa taifa, mwl, Julius Nyerere aliyechukia ubaguzi–aliwaruhusu jamaa hawa waliokuwa wakihujumu uhuru wetu wazi wazi kuwa raia wa taifa jipya la Tanganyika.
Wakati wa viongozi wetu kuangalia mambo kama yalivyo ni sasa ambapo wenye uwezo waamriwe kujenga nyumba zao binafsi ili kuwapisha wasio na uwezo kutumia nyumba husika. nyumba hizi, kwanza, ni za umma; na ni alama ya uhuru wetu. Je watu wetu maskini –hasa wafanyakazi wa serikali –wataendeleaje kunyanyasika kwenye nyumba binafsi za kupanga wakati nyumba zao zinakaliwa na matajiri wenye mahekalu wanayopangisha kwa fedha za kigeni? Kama haitoshi, mfumo wetu, umeruhusu tabaka moja la wachache kutajirika wakati umma ukiendelea kuteseka kwenye umaskini. Makonda anapaswa kuanzia hapa. Na hili haliwezi kuonekana kama ubaguzi. Kwanini wao kukalia nyumba za umma tena kama tabaka moja halionekani kuwa ubaguzi wa wazi wa kiuchumi na kijamii?
Kwa wanaokumbuka huu ubaguzi wa wazi ulivyokuwa umehalalishwa, watakambuka namna marehemu Christopher Mtikila alivyoushughulikia hadi kuupunguza kidogo tena kwa muda. Kwa watu wa kizazi cha kuanzia miaka 50 kwenda juu waliokulia kwenye jiji la Dar Es Salaam, watakumbuka ambavyo wahindi–ambao Mtikila aliwaita magabacholi tokana na neno chori au mwizi ambalo walilitumia kuwaeleza waswahili kama wezi–walikuwa hata hawapandi dala dala wala kuchanganyikana na waswahili ukiachia mbali kuwatumia kama watumishi wa madukani na majumbani na walinzi wao.
Japo tunajua kuwa jamaa hawa wanatokana na mfumo mbovu wa kikaburu wa caste system, waliruhusiwa kuendelea na ubaguzi wa wazi wazi. Kama tulivyosema hapo juu, wakati wa kubomoa mfumo huu kimfumo ni sasa ambapo serikali yetu inapaswa kutangaza wazi wazi isivyoridhishwa wala kukubali jinai hii ya wazi.
Tumalizie kwa kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam –ambaye ameonyesha kuwa na nia ya kuwakomboa wanyonge–aanze kubomoa mfumo huu wa kibaguzi mkoani mwake–kwa kuanza na nyumba za Msajili wa Majumba. Lazima nyumba hizi zionyeshe sura ya Tanzania na si ya India wala utajiri. Miaka zaidi ya 50 tabaka moja limefaidi nyumba za Msajili itoshe. Tutunge utaratibu wa kuzuia ubangishanaji wa kifisadi ambao umefanikisha na kuhimiri mfumo huu wa kibaguzi.
Tanzania Daima Jumapili.

No comments: