The Chant of Savant

Saturday 11 May 2013

Kumbe na wamanga wamo!

Nimependa wimbo huu unaoonyesha kuwa kumbe usilolijua litakusumbua kwa vile waarabu na wayahudi ni 'dugu'. Kweli waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba!

8 comments:

Anonymous said...

Soma historia ya dini ya kikristo yesu ni nani mwalimu A.k.a mpagani.

halafu tafuta maana ya wamanga
uwajuwe ni nani
JARIBU hebu msaidie mwalimu wako
not all arabs are muslim and not all muslim are arabs.

kumbe usilolijua litakusumbua tene sana

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Sijui kama anonymous hapo juu umenielewa. Sijasema kuwa all arabs are muslims or all muslims are arabs. Mie nimeweka muziku watu wafaidi sijui kama hilo ni kosa. Kama ni kusoma historia ya waarabu najua fika ni dugu moja na wahayudi kutoka kwa shehe Ibrahim. Hata hivyo karibu tena kwenye mjadala kama kuna hoja. Nadhani hata Jaribu ataliunga mkono hili. Shehe endelee kuburudika na huo wimbo mtamu wa kimanga. Inshallah siku nyingine.

Mtwangio said...

Anonymous,Tatizo siku zote unapomsoma mtu wakati umeshajijaza fikra tangulizi dhidi yake siku zote unakuwa na upofu na uziwi na matokeo yake unakuwa huna cha kuchangia katika mada.Sasa kama unameona kwamba Mhango amejingikiwa na hilo kwa nini basi wewe usituelimishe japo kwa ufupi kwani kuna wasomi wengine ambao wanasoma kimya kimya pia wanataka kufaidika na mchango wa mawazo yako.Lakini ikiwa kila ambacho anaandika Mhano kwako wewe akipendezi basi bora nawe uwe katika wale wanaomsoma kimya kimya tu na wapo wengi.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mtwangio hujakosea. Jamaa anadhani naandika kuwafurahisha watu asijue shida yangu ni public advocacy kutaka watu wabadilike. Huwa siangalii ima nani ataudhika au kufurahi zaidi ya kulenga kutoa mchango wangu. Hata hivyo sina shaka historia itatuhukumu siku moja.

Anonymous said...

Hayaa jamani wendawazimu wemengia kina mtwangio wewe alikwambia nani kuwa kila anachoandika hakipendezi
wazimu una ncha 40
kwenye msafara wa mamba na kenge wamo

public advocacy si uteremke huku dar mchango wa kueneze chuki

Mtwangio said...

Anonymous,
Unatapotaka kumuelewa mwanadamu uwezo wake wa kufikiri ni jinsi gania navyojieleleza kimawazo.Naheshimu mawazo yako kama mwanandamu,kwani bnakiri na nakubali na kuelewa kwamba Mwenyezi Mungu ametuumba sisi wanadama na kutupa uwezo wa kufikiri na katika kufikiri tunatofautiana mawazo na kama vile ambavyo ametupa sifa mbali mabli na vipaji tofauti.Lakini wengi wetu kama wanadamu jinsi tnavyoishi hatutofautiani sana na utaratibu ambao Mwenyezi Mungu aliowaumbia wanyama yaani tunazaliwa,tunatafuta chakula,maji,tunatafuta mshirika wa maisha tunazaa watoto tunawalea na hatimaye tunakufa na hakuna chochote tunachochangia katika sisi wenyewe,familia zetu,vitongoji vyetu,nchi zetu na dunia kiujumla.Naam nasema wanadamu wengi ndivyo hivyo tunavyoishi.kwa wale waumini wa kidini hususa za mbinguni wanaamini kwamba mlango wa utume umefungwa nami ni mmoja wao lakini naamini kwamba mlango wa unabii bado upo wazi na utaendelea kuwa wazi na inapotokea kupatikana mtu kama Mhango na mafano wake ambao wameikataa dunia na utamu wake kwa kupigania kufikasha ujumbe wa unabii kwa watu wao au nchi yao watu hawa wanatofautina na wale wa kundi la wengi akina sisi.

Mhango,anaheshimu wasomaji wake na anawajibu kulingana na kila mtu na jinsi anavyofikiri na kujieleza kimawazo na kwa hili anastahiki pongezi kwani kama asingekuwa ni mtu wa kufikisha risala watu kama wa mfano wako wala asingepata tabu ya kuwajibu.Naam,Mhango kama mwanadamu si mkamilifu ukamilifu ni wa Mwenyezi Mungu ambae akosoei wa hasahau kwa hiyo sisi kama ni wasomaji wake tunachohitajika ni kuchangia mchango wa kujenga kwa yale ambayo anayoandika kuhusu nchi yetu na viongozi wetu na naposema mchango wa kujenga hata kumkosoa mana katika kumkosoa pia tunamjenga na kuweza kujua wapi mapungufu yake,wapi aliposahau au wapi alipojingikiwa.Kusema kwako kwamba anaeneza chuki sijui una maana gani unaposema chuki na chuki hizo kwa ajili ya akina nani na kwa masilahi ya nani?je unadhani tukikubaliana nawe kwa hoja ya mjadala kwamba Mhango anaeneza chuki ni nini Mhango atafaidika binafsi na kwa anamtumikia nani kwa kueneza chuki hizo?

Unapojingikiwa na kitu au jambo lolote lile na ukafanya majuhudi ya kibinadamu ya kutaka kulijua jambo hilo kwa kusoma au kujielimisha basi wewe unakuwa ni miongoni mwa wenye akili timamu lakini unapoujua ukweli na haki kisha ukawa unafanya majuhudi ya kuukataa ukweli huo na kuupiga vita au haki hiyo ukaiita ni batili basi wewe ni katika wendawazimu.

Mhango,hata kama kizazi hiki hakitoju,kutothamini,kutosikia na kutoelewa ujembe wako naamini kizazi kijacho kitajua,kuthamini,kusikia na kuelewa ujumbe wako kwani risala yako itabaki miaka nenda miaka rudi muda wakudumu dunia iteendelea kuwa hai.kwa hiyo makelele ya mbwa hayazuii gari moshi kuendelea kufanya safari yeke!

Jaribu said...

Aonymous mwenye kichwa kizito:

Tatizo la Watanzania wengi ni unafiki. Afadhali kudili ni mwalimu Mhango kuliko Dr Dowans bin Kikwete any time. Maana yeye kama wafuasi wake wanajifanya wacha Mungu lakini ndio wamejaa madhambi kuliko watu wengine. Nadhani atakuwa amefurahia milipuko na majangna mengine kwa sababu inampa fursa ya kwenda kwenye mazishi. Anajali sana wafu kuliko walio hai. Namshauri muda wake ukiisha aingie kwenye biashara ya u-undertaker. Huko atakutana na maiti kedekede!

Sijui kuhusu Mhango lakini kama mimi ukiniita mpagani ndio kwanza nafurahia kwa sababu najua umenitambua kuwa mimi ni mtu rational, sijali dini au rangi ya mtu. Watu weusi kulipuana kwa dini za Wayahudi na Waarabu ni kitu ambacho nashindwa kuelewa.

Naona imekukera Waarabu kuitwa Wamanga! Kama itakufariji, ujue wao nao wanakuita wewe "abidi". (mtumwa), au "kushi", (ni**er).

Mhango, jamaa wakiishiwa hoja huwa wanadandia issue ambazo ziko peripheral wakati hoja ya msingi wanajifanya hawaioni. Ukisema hutaki viongozi wezi na wabadhirifu basi una chuki au unaona wivu. Ndio shida ya kushusha viwango katika kila kitu hata uongozi, kila mkora na ndugu yake naye anaona kuwa anastahili!

Are we still talking about the video?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Hao hata wakiitwa abdi, afarika,ami na majina mengine machafu hawasikii. Nadhani tatizo la watu wetu ni ukosefu wa habari kuhusiana na jinsi watu weusi wanavyobaguliwa na hao wanaowaabudia. Nakumbuka kisa kimoja hapa Kanada. Nilikwenda hospitali nikakuta mama mmoja wa kihindi kutoka Afrika Kusini. Mama mweusi kama msomali. Katika maongezi akawa anamtania binti yangu kuwa yeye ni mweusi wakati yeye binti yake ni brown. Ni bahati mbaya kuwa ungelinganisha huyo mama na binti yangu ni kifo na usingizi kama ni suala la nani ni maji ya kunde. Kumsaidia nilimwabia kuwa sisi tunaotoka Afrika yaani Tanzania na Afrika kusini hata mashariki ya kati kwa wenzetu wa magharibi ni waswahili tu. Mama hakupenda ukweli huo aliamua kuua maongezi na kila mtu akachukua hamsini zake. Laiti kwa mfano watu wangekuwa wamewahi kwenda nchi kama Sri Lanka wangeacha upuuzi wa kuwaona wahindi kama weupe au waarabu wanaotokea kwenye maeneo kama Ismailia kule Misri. Kwa vile kuna wenzetu ambao wamekubali kuitwa watumwa chini ya dhana mbali mbali kama dini, utauwa na upuuzi mwingine. Mie kuitwa mpagani naona sisawa kwani mbele ya dini zao mimi ni kafiri kama ambavyo nao ni makafiri mbele ya dini na imani nyingine. Kimsingi, kila mmoja ni kafiri au aliyekataa kwa namna yake. Mpagani au pagan ni jitu ambalo halikustaarabika au kuendelea jinga zuzu na taahira. Mie nadhani ni bora kuliko hao. Nimesoma nimesafiri niemeelevuka na bado natoa mchango wangu. Hivyo Jaribu kama tuacha matusi, anayekuita mpagani anaweza kuwa yeye mpagani. Pia akuitaye kafiri naye ni kafiri kwa namna fulani.