Tuesday, 2 December 2014

Hii nayo imekaa vipi?


Baada ya kunusurika kukumbwa na maji, JK atakuwa anachekelea ujinga na papara za bunge letu na upinzani kwa kushindwa kushughulikia serikali nzima wakaridhika na kafara ya vijidagaa. Uamuzi hafifu na wa aibu wa Bunge umethibitisha jinsi upinzani usivyo na mipango ya kuchukua nchi. Maana kama ungekuwa na visheni na mipango mikubwa, kwa kutumia msimamo wa wafadhili ungewataka wananchi waingie mitaani na kuiondoa serikali hii fisadi na dhalimu ya JK. Bahati mbaya, kwa upofu na upogo wao hawakuliona hili. Halafu bado wanajipiga vifua kuwa wamewashughulikia mafisadi wakati mkubwa wao akiendelea kupeta katika nchi hii iliyogeuzwa shamba la bibi chizi.

2 comments:

Anonymous said...

Bara Afrika halitaendelea na litaendelea kurudi nyuma kimaendeleo kwa sababu tunafanya masihara katika mambo muhimu kufanya maumuzi ambayo nyakati zote tunahamisha matatizo na siyo kuyapatia suluhisho matatizo yaliyopo.

NN Mhango said...

Anon usemayo ni kweli kwani balaa hili kila mahali katika bara la Afrika ambalo limegeuzwa Balaa la Afrika kwa watu maskini na wasio kwenye madaraka.