Friday, 19 December 2014

Tibaijuka kitoe acha uhuni

mtanzaniadaily.2indd
Picha kwa hisani ya gazeti la Mtanzania
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka anachekesha. Amechemsha na anaonekana kuishi katika ndoto. Kwanza ni muongo na fisadi tokana na nyodo zake kuwa hawezi kujiuzulu baada ya kupokea kitita cha shilingi bilioni 1.6. Wengi walitegemea angeleeza amepewa fedha nyingi hivyo kwa kazi gani. Pia alishangaza wengi aliposema kuwa pesa aliyopokea si chafu wakati akijua ni ya wizi tena wa fedha za umma maskini wa nchi ombaomba. Tibaijuka alikaririwa akisema kuwa kuandamwa ni changamoto ya kusaka maendeleo. Maendeleo gani? Atakwambia anamilki shule ili kuleta maendeleo. Je maendeleo gani yanaletwa kwa fedha chafu tena ya kuuibia umma? Je hayo maendeleo kupitia shule binafsi yanamlenga nani wakati ukweli ni kwamba anachofanya Tibaijuka ni biashara tena akiwa kwenye ofisi ya umma? Pia aliwahi kusema eti James Rugemalira, mtuhumiwa na kingpin wa ujambazi wa escrow ni kaka yake. Je mbona hawaonekani ndugu wengine wa Rugemalayer kwenye mgao?
Inashangaza kwa mtu mwenye elimu ya juu hivi kushindwa kuelewa hata mambo rahisi kiasi cha elimu yake kutia shaka. Tibaijuka acha uhuni. Kitoe tu umeishaishiwa na kuisha. Kutapatapa hakutakuponya na anguko litokanalo na uchoyo, ufisi, ufisadi, ubinafsi na upofu. Watanzania wamechoka na watawala wezi wenye kujificha nyuma ya visingizio mbali mbali. Iistoshe, ofisi ya umma si mali yako binafsi kiasi cha kuing'ang'ania.
Kama unaona umeonewa nenda mahakamani. Pia ufahamu kuwa unachofanya ni dharau kwa Bunge na kamati yake hasa pale uliposema kuwa kinachodaiwa kuwa makosa ni uvumi. Si uvumi ni ukweli tena ukweli mtupu uliofikiwa baada ya kufanyika uchunguzi. Si uende ukaajiriwe na hao mabwana zako kama walivyomwajiri nshomile mwenzako Patrick Rutabanzibwa? Nenda Tibaijuka nenda. Hufai tena nenda tu. Nenda na mapema utuachie ofisi yetu. Nenda ukafanye biashara na huyo Rugemalayer wako.

2 comments:

Anonymous said...

MWIZI HUYU MAMA NAYE KAMA KWELI ALIKUWA MWADILIFU ALIPOSIKIA SAKATA HILI KWA MARA YA KWANZA KWANINI HAKURUDISHA PESA HIZO HADI AJUWE UKWELI
INASHANGAZA PENGINE WATU UKAGUZI AU TRA NI WANAFUNZI WAKE LAKINI WAMEMSHINDA KWA HILI
KAMA HUJIUZULU TUTAKUSURUBU WEWE NA SHULE YAKO

NN Mhango said...

Anon umenena. Hata hivyo kamwaga maziwa mwenyewe kwa upogo na upofu wake atajutia siku moja. Nadhani hata ndoto ya urais imeyeyuka vilivyo. Go Tibaijuka go. Humjui Kikwete siyo.