Thursday, 11 December 2014

Kuombea taifa au kuganga njaa?

Baada ya ufisadi na ujambazi kulipa, umezuka mtindo mwingine mpya wa wasaka tonge kula kwa kujifanya wanajali taifa. Hapo juu ni waganga njaa wanaojificha nyuma ya dini za kuzua eti wanapanga kuombea taifa. Taifa linahitaji kuombewa au kuchapa kazi na kuondokana na uongozi mbovu na tapeli wa akina Kikwete? Hawa nao ni sehemu ya tatizo kwa taifa letu. Mijitu imeshindwa kusoma na kupata ajira nzuri au kujihangaisha na shughuli za kuzalisha inajifanya ina uchungu na taifa. Shame on you all! Ukichunguza wengi hapo unaweza kukuta wala si watanzania bali matapeli toka nje wanaojificha nyuma ya dini.

2 comments:

Anonymous said...

Hao wala sadaka(Makusanyo ya fedha) waamini wao! hakna jipya hao wababaishaji

NN Mhango said...

Anon usemayo ni kweli tupu hawa wanasumbuliwa na njaa na ujinga wa kujiona wajanja ukiacha mbali kuwa hawana njia nyingine iliyosalia kwao kujiondoa kwenye umaskini na njaa zaidi ya kuwaramba makalio mafisadi na watawala.