Thursday, 25 December 2014

Nukuu mbovu za mwaka 2014

“Watanzania tumejaa ubinafsi, kila mtu anafikiria kila anafanya jambo anategemea kupata posho, na niwahakikishieni mimi sina uchu wa ubinafsi wala tamaa za vyeo kwani kama ni cheo nilichoacha UN kilikuwa kikubwa zaidi,” Profesa Anna Kajumlo Tibaijuka. Hii nukuu imechukua nafasi ya kwanza kwa ubovu kwanza, kutokana na hadhi ya aliyeitoa kielimu. Na pili mjumlisho wake. Hivi huyu hakusoma kanuni na miiko ya uwasilishaji taarifa? Je hajui kuwa mjumlisho ni kiashiria kikubwa na cha juu cha ujinga? Inakuwaje profesa mzima anasema eti watanzania wote wana ubinafsi wakati yeye anayesema si mbinafsi ni mtanzania? Unawezaje kusema "kila mtanzania" utadhani umeongea na watanzania wote? Angalau angetoa hata takwimu lau kuficha ujinga na ujuha wake.
“Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipoulizwa na Kamati ya Bunge alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL,” Rais Jakaya Kikwete. Je kama fedha ni za IPTL ni kwanini umekubali kujiuzulu kwa Mwanasheria mkuu wa serikali na kumtimua waziri wa zamani wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka kwa kukatiwa fedha hiyo hiyo ambayo si ya umma bali IPTL?
Hebu soma nukuu nyingine ya Kikwete ili uamue mwenyewe, “Tumezungumza na Profesa Tibaijuka na tumemuomba atupishe ili tuweze kuteua waziri mwingine kwani viashiri vyote vinaonyesha kuwa alikiuka kanuni na sheria ya maadili ya Umma.” Maadili gani ya umma yamekiukwa kwa kupokea fedha halali sawa na serikali inavyopokea misaada toka Ughaibuni?

3 comments:

Anonymous said...

Hii ni sawa na ugonjwa wa kansa iliyoshamiri katika mwilini mwa mwanadamu, hakuna pa-kushika toka kwa Profesha Mhaji Mharefu tabajuka mpaka mkuu kaya na pale kijijini kwetu kwa mzee Runyoro na Ishengoma mwenyekiti mwenyekti wa kitongoji chetu vyote ovyo ovyo ovyo au tuite shaghalabaghala.

Anonymous said...

Hii ni kutokana na watu tuliowaweka ofisini kutokuwa na sifa ya uongozi,naam unaweza ukawa umesoma na kuwa na shahada ya juu kama wengi wanaopatikana Afrika lakini kwa bahati mbaya hawana sifa za uongozi,kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea maongezi yako au hata statement yako ikiwa ayaendani au aiendani na maadili ya uongozi unaweza kujikuta unawajibika kuicha ofisi.Na kwa upande mwingine ni dhana ya baadhi ya tuliowaweka ofisini na baadhi ya wasomi wetu kutuchukulia sisi waskilizaji wao ni kama mataahira wataongea chochote kile wanachofikiria na kukitaka bila ya kufikiria ili mradi tu wao n viongozi na ni wasomi.
Ebu angalia maongezi ya huyu Mama Ana,haya ni maongozi ya chumbani ya pillow talk kama wanavyosema wazungu au ni maongezi ya mezani akila na familia yake lakini sio statement ya kisiasa kwa hadhi ya wadhifa kama wake kuitoe mbele ya watu.
Watu kama akina Kikwete ni wazi kabisa wanawajua wasikilizaji wao na wnadhani tu siku zote wanaongea na wadanganyika tu ambao hatuna uwezo wa kufahamu na kuelewa nini kinachoongelewa,na ukijaribu kuelewa unaambiwa hujafahamu au umemnukuu vibaya.

NN Mhango said...

Anon hapo juu msemayo ni kweli tupu. Tuna kansa katika nchi inayosumbua taifa na hata watawala na watu wake. Wanajifanyia mambo hovyo hovyo wakidhani na watanzania wana fikra na akili za hovyo. Tuombe Mungu mwaka unaoanza watu wetu waamke na kuirejesha nchi yao kwenye mstari. Nawatakieni HERI YA MWAKA MPYA 2015.