Wednesday, 10 December 2014

Viongozi wa dini na kujikomba kwa rais

Rais Jakaya Kikwete akiwa pichani ikulu pamoja na baadhi ya viongozi wa dini waliokwenda kumuombea baada ya kurejea toka kwenye matibabu ya kansa ya kizazi huko Marekani. Inashangaza viongozi wetu wa kiroho wanavyojigonga kwa rais. Wanapataje muda wa kwenda eti "kumuombea" lakini wakashindwa kumwambia kuwa anatawala nchi kifisadi huku akihalalisha wizi wa fedha za umma? Hawa kweli ni viongozi wa dini au wajanja wanaotumia majoho kukidhi njaa zao? Je ni wagonjwa wangapi wanaoza mahospitali na hawa hawa wanaojitia viongozi wao wa kiroho hawaendi kuwaombea? Hawa wameenda kumuombea Kikwete au kumuomba awape chochote kitu? Viongozi wa dini wanapofunga ndoa na wanasiasa wachafu mjue taifa linaangamia.

2 comments:

Anonymous said...

Kikwazo kimojawapo cha maendeleo Afrika hizi dini zisizozetu kiasili zilikuja kinyemela ili kutafahamu halafu kutupumbaza kushabikia ili tuwe laini tufanywe watumwa kiakili mpaka leo. Tena mara nyingi tunajivuna kwa kuwa waamini wazuri kwa kitu kisichochako kiasili na kusahau kuwa mababu zetu walichukuwa watumwa kutokana na hizi dini zisizozetu

NN Mhango said...

Anon umefanya nijisikie kulia.Maana kama kuna falsafa ninayoamini kuliko zote ni hii ya kuzipiga vita na ikiwezekana kuzibatilisha hizi dini nyemelezi ambazo licha ya kutunyonya zimetuachia mizigo kama vile kubaguana na kudharauliana sisi kwa sisi, kuua mila zetu na kutusingizia kila uchafu. Leo angalia kwa mfano usenge na usagaji. Vimeletwa na hawa hawa mahabithi wanaojidai kutufundisha kuwatumikia miungu yao ya kishenzi. Leo tunauana sisi kwa sisi kama vile kule Nigeria tokana na imani hizi za kishirikina za kimapokeo. Acha niishie hapa ila nakushukuru kwa angalau kumtoa paka kwenye pakacha. Karibu tena ugani uchangie utakavyo bila kubughudhiwa.