Wednesday, 17 December 2014

Nenda Werema

Nenda  Fredrick Werema nenda. Nenda jaji junk. 
Nenda jaji janga. Nenda tu umenyea kambi.
Nenda wala usiangalie nyuma. 
Nenda tu mwanakwenda. 
Msiba uliotuachia ni mkubwa. 
Nenda ukaajiriwe na PAP na VIP kama Patrick Rutabanzibwa. 
Nenda ukawatumikie mabwana zako. 
Nenda tu hakuna anayekuhitaji.
Nenda sasa unanuka.Unanuka ufisadi
umeoza na kuozeana nenda tu mwanakwenda.
 Nenda huna wa kukulilia isipokuwa Kikwete.
Kikwete atakulilia. atakumiss.
Amekusifia kwa kazi "njema" kwake na IPTL.
Umma hauoni kazi njema zaidi ya machukizo ujambazi na hujuma.
Nenda Werema nenda
Nenda kwa haraka nenda
Harbinder Sethi Singh atakumiss
James Rugemalayer atakuombolezea.
Watanzania watakuzomea
Nenda mwana kwenda
Tokomea huko utokomeako
Nenda usigeuke nyuma tukakuonea huruma
Nenda huko usirejee tena kwenye ofisi zetu
Nenda na balaa lako.
 Nenda na kazi zako chafu. 
Nenda msomi aliyefanya ujinga kuliko hata mbumbumbu. Nenda msomi mbumbumbu. 
Nenda tu. 
Tangulia mwana kutangulia. 
Muongo anangoja kukufuata. 
Nenda tu usigeuke nyuma ukawa jiwe la chumvi japo u zigo la uoza. Nenda tu mwanakwenda Werema.
Nenda usinung'unike
Nenda usisingizie
Nenda usilaumu
Nenda huenda bosi wako atakuzawadia 
kwa kazi "njema" ulofanya ya kutetea uoza wake
Huenda atakupa ubalozi kama wengine
Siku akikuteua
Nitararua nguo zangu 
Nitavaa magunia
Nitajipaka majivu
Nitaomboleza 
Nenda mjalaana nenda.
Nenda usigeuke nyuma
Nenda ushatuchafua
Nenda ushatuibia
Nenda wala hatukutaki
Nenda kwatumikie hao waliokuumba.
Nenda tuache tusherehekee
Tusherehekee anguko lako takatifu
Umetoka kwenye utukufu na kuangukia kwenye ukufu
Nenda usivuruge sherehe zetu
Nenda tuache tujipongeze
Kama kibwengo nenda
Nenda na mzigo wako wa moto kichwani
Kama mtalaka nenda
Ndoa imekushinda
Nenda kaolewe na akina Harbinder wako
Nenda na nyodo zako
Nenda usilete fyoko
Nenda Werema Nenda.

5 comments:

Anonymous said...

Anakwenda wapi huyo!!!!? Husishangae anateuliwa kuwa mjumbe au mwenyekiti kamati kuu ya kupitisha Katiba yao!

Anonymous said...

Nani tumbili sasa kati yake na Mzalendo Komredi Kafulila!?

NN Mhango said...

Anon
Hata huko aendako siko alikotegemea. Ashachafuka. Ama kuhusu tumbili nadhani yeye ni gorilla tena lile kubwa lao.

Anonymous said...

Tunataka waende wote waliotajwa
GOLILA HILO SURA MBAYA HATA ROHO YAKE
INASHANGAZA RAIS BADO ALIMBEBA LICHA YA KAULI NA DOMO LAKE LISILO NA TIJA
LAKINI MSINGAE AKAWA BALOZI HUYU
CCM HIYO

NN Mhango said...

Anon umesema kweli tena inayouma. Siku akiwa balozi nitararua nguo zangu na kuomboleza.