The Chant of Savant

Tuesday 21 July 2015

Rais ajaye ahakikishe mkewe hatuibii kwa NGO


Msikilize kihiyo wenu anavyobukanya kimombo na kupaniki.

2 comments:

Mbele said...

Tangu mwanzo, nilikuwa nafuatilia mitazamo na shughuli za Mama Salma Kikwete katika sekta ya ualimu. Mimi kama mwalimu nilivutiwa na juhudi zake, na pia mitazamo yake kuhusu uelimishaji wa watoto. Kuna wakati niliwazia hata kuandika kijimakala kuelezea hayo. Sikupata wasaa wa kufanya hivyo.

Ninawaheshimu sana walimu wa shule ya msingi. Ninaona wanafanya kazi nzito kuliko yangu kama profesa. Ninafahamu kuwa mtazamo wangu ni tofauti na mtazamo wa jamii. Lakini ndivyo ninavyofikiri, kama nilivyoandika katika blogu yangu. Makala hiyo imo pia katika kitabu changu cha CHANGAMOTO: Insha za Jamii.

Kuhusu ki-Ingereza, Mama Salma Kikwete katika video hii anasoma kwa ubora kuliko wa-Tanzania wengi ambao wamejifunza ki-Ingereza hadi kiwango chake. Katika nchi yetu leo, hata wanafunzi wa vyuo vikuu na wasomi kwa ujumla hawakimudu ki-Ingereza kama ilivyokuwa miaka arobaini na zaidi iliyopita nilipokuwa shuleni. Ni kweli, ana lafudhi ya lugha mama, lakini huu ni ukweli kwa kila binadamu. Ingekuwa ni Mchina, Mjapani, au mtu wa taifa jingine, tungesikia lafudhi zao pia. Hili ni jambo ambalo wataalam wa lugha wanalitambua kama "mother tongue interference." Kwa ujumla si tatizo.

Hapo nimeongelea suala la elimu na ualimu. Mimi si mtetezi wa mtazamo wa kisiasa wa Mama Salma Kikwete, ambaye ni mwana CCM. Tukiongelea masuala ya siasa, mimi daima nimekuwa mpinzani wa CCM. Namwongelea Mama Salma Kikwete kama mwenzangu katika ualimu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kaka Mbele asante sana kwa mchango wako japo hukujikita kwenye kueleza huo mtazamo chanya wa Salma Kikwete ambaye ni mfinyu na wa kikabila. Kila anachoomba na kupata hupeleka kwenye shule yake ya Nakayama. Nakubaliana nawe kuwa walimu wa shule za msingi wana kazi ngumu ingawa Salma si mmoja wao. Kuhusu kiingereza chake kama utamsikiliza vizuri utagundua ubovu mwingi japo kwa kiwango chake anabukanya na kuonekana bora kwa kulinganisha na watanzania wengi akina mimi ni Maimuna. Kama tutatenda haki, hatupaswi kulinganisha mtu wa kada ya Salma na wagonjwa. Kwani alikuwa na fursa ya kujiendeleza na kufanya mambo makubwa badala ya huu uchuuzi wa NGO. Pia nadhani kusoma na kuelewa lugha ni vitu tofauti sana. Sijui kama umedurusu anavyohema na kuonyesha wasi wasi. Najua fika kuwa Salma ana elimu finyu. Wala sijagusia lafudhi kwani hata mimi ninayo ingawa wanangu hawana. Nilicholenga kuonyesha ni jinsi watu wetu wanavyopoteza fursa muhimu. Hivi kwa miaka kumi ambayo Kikwete amekuwa madarakani, kama Salma angejiendeleza badala ya kukimbizana na kuombaomba na siasa angekuwa mbali kiasi gani?