Monday, 3 September 2012

Huyu ni shehe au shetani?


  • Pakistani cleric Hafiz Khalid Chishti, the Imam of a local mosque, looking on during an interview with AFP in Mehrabad, a suburb of the capital Islamabad on August 24. Pakistani police have arrested the cleric on suspicion of planting evidence against a Christian girl accused of blasphemyKesi ya msichana wa miaka 14 nchini Pakistani anayeshikiliwa na polisi kwa zaidi ya miezi miwili ilivutia hisia za watu wengi duniani. Kilichofanya kesi hii iwe maarufu ni madai kuwa msichana huyu ambaye anadaiwa kutokuwa na akili timamu na mkristo anadaiwa alichoma Korani na vitabu vingine vya dini. Kosa la namna hii nchini Pakistani hubeba adhabu kali. Baada ya kutokea tukio hili, kuklitokea mapigano baina ya waislamu na wakristo huku waislamu wakiwataka wakristo waondoke kwenye eneo lao. Lakini sasa ukweli umegundulika kuwa kumbe yule msichana hakuchoma Korani bali shehe wa msikiti katika eneo hili Hafiz Khalid Mohamed Chishti, ndiye aliyechanganya karatasi za Korani kwenye taka anazodaiwa kuchoma yule binti ili kuanzisha mzozo unaoweza kutumika kuleta vurugu hata kuwaondoa wakristo kwenye eneo hili. Chishti amekamatwa baada ya wasaidizi wake wawili kutoboa siri hii. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Labda ni shetani!! duh pole na msichana kwa kusingiziwa

anjela said...

ndio akili za ndugu zetu zilivyo,tuwavumilie tu

Anonymous said...

Sheikh,Shehe, Shekha,
Huyu sio katika hao huyu ni Imam na sio kila Iman anakuwa shekhe
usipopowe tuu