Thursday, 13 September 2012

Polisi na mauaji ya Mwangosi



NGOJA niimbe ule wimbo nilioutunga kwa ajili ya jamaa zetu wa Sauzi walipokuwa wakipambana na utawala wa kikaburu wa kibaguzi.
Wao walibaguliwa kwa rangi sisi tunabaguliwa kwa kipato na itikadi za vyama vyetu hasa kijiwe kitukufu.
Naimba kwa kimombo kwa vile nimepagawa na kuchukia nusu ya kupasuka.
Naimba kwa kikameruni ili akina Kameruni wanaobeba hii mizigo yetu michafu inayonuka wasikie na kuchukua hatua.
Nawambia wasiokuwepo ili waliokuwepo wapate somo.
This is the song of peace
It aims at all S.O.B's and D.O.B's
You guys in fatigues
With your totting guns
Trigger happy as you always are
You the killing machines,
You who violate peace
You who are used by morons
Guys,
When you kill, just kill peacefully
When you rape just do it peacefully
You venal and thievish robbers
Whey you steal, just do it peacefully
Do even your corruption peacefully
For this is the hank of peace
Peace in everything you do
Cops, officials and all courtiers
When you act, please act peacefully
I am talking to everybody
All sheep and hyenas
Noble and disgraced
Please observe peace
Again I should insist
That those suffering should
not accept this
Stand up for your rights
Avoid and hate this elusive
peace
Do your pacifism and passivism
work hither?
Peace that leave in pieces
Just fight straight on and head on
Fight this Criminal Cabal of Murders (CCM).
Fight all Coverted Operessive Parloiners (COPS).
Fight all noble thiefs and their majordomos
Fight fight everywhere
Kutokana na unyanyasaji na unyama aliofanyiwa marehemu David Mwangosi, huu wimbo nilipanga kuuimba kwenye mazishi yake, lakini sikuweza kuyawahi.
Mwenzenu wiki iliyopita ilikuwa mbaya kwangu.
Wazungu hasa wainglishi wangesema it was a peevish week. But mine was even more peevish than the peevish one the English people talk of.
How could it be spiffy whilst I witnessed police diabolically felling someone just like a digidigi? Lo! Nikichukia huwa naongea kikameruni hata bila kutaka. Tusameheane. Maana sina jinsi ya kuongelea unyama na ushenzi aliofanyiwa swahiba yangu marehemu David Mwangosi huko kwa akina kamwene.
Basi bwana, nikiwa kwenye mihangaiko yangu ya kukagua kijiwe cha kwa akina Kamwene na Chakudema nao walikuwa wakifanya mikutanko yao.
Bila hili wala lile ndata nao wakatumwa na mabwana zao kwenda kuvuruga ule mkutaniko bila sababu ya msingi zaidi ya woga.
Walibeba mibunduki na mibomu utadhani walikuwa wakienda zao vitani. Upuuzi mtupu.
Yaani mnataka kuwatisha wanakaya hata kudhani wataacha kufikiri? Mlaaniwe na mteketee na wale wote waliowatuma. Hamuwezi kufanya watu wasifikiri kwa vile nyinyi na hao waliowatuma hamfikirii. Kwanini mnakuwa kama hamnazo kugundua kuwa wanaowatuma ni wachovu wanaongojea kiama chao?
Kwa taarifa yenu tutaendelea kufikiri tena zaidi ya tulivyokuwa tukifikiri.
Kweli kaya yetu imekwisha. Mijitu bila aibu inahubiri amani wakati ikifanya shari na mauaji. Kama hamtaki mikusanyiko ya kisiasa mliridhia viama vingi ili iweje?
Mnadhani mtatawala milele? Kwanini hamkujifunza kwa akina Mwamali Gazafi wa jana jana tu?
Shauri yenu endeleeni na ujuha hadi yakapowakuta ya kuwakuta.
Ngoja niwatukane hata walevi: Nanyi mmezidi kwa ufala na ukondoo. Isingekuwa hivyo nani angetumia mikodi yenu kununua misilaha ya kuwalipa au kuwafunga wauaji wenu? Mnaogopa kunyotoka roho lakini bado mnanyotolewa kama alivyofanyiwa comrade Dav Mola aiweke roho yake pema peponi.
Kwenye sera za kijiwe, kuna kanuni moja muhimu ambayo inasema; Kijiwe kinaogopa watu woga hasa wenye maulaji kuliko hata ukoma.
Kwani watu wa namna hii hawana tofauti na nyoka mwenye sumu ambaye yuko tayari hata kung’ata mti asijue sumu yake haiwezi kuufanya kitu. Hivi unaposhindana na wengi unategemea nini zaidi ya kujichimbia kaburi ukiwa hai?
Hivyo kwa kijiwe chetu, woga na ufala ni kitu kimoja tena cha kuogopwa. Inaamsha hasira sana unapogundua kuwa mwoga ni mwizi, fisadi na muuaji ambaye yuko tayari hata kutumia bunduki kuulia mbu.
Mambo huwa mabaya hasa akitumia mijitu isiyo na akili wala utu kama ili mijamaa iliyomnyotoa roho rafiki yangu Mwangosi.
Nasikia waongo fulani wenye akili na nafasi za kutia kila aina ya shaka wakisema waliomuua Mwangosi ni Chakudema wakati ukweli wenyewe ni kwamba aliuawa na ndata.
Mie niliwaona na kwa taarifa yenu ile picha mliyoona nilipiga mimi baada ya watu wote kuogopa na kutimka mbio.
Leo nimeamua kulaani na kuongelea ufala na upuuzi unaofanywa na watu wanaojiona wajanja wakati ni mafala tu. Jitu linaua mtu eti linapendekeza muuaji aunde tume ya kujichunguza. Akili au matope? Whom are you trying to fool thinking he is a gowk like you? For your info we are not goons and dunderheads and numskulls like you. Sorry- samahani nimekasirika ndiyo maana kinanitoka kikameruni. Natamani hawa jamaa wapate wababe wawakameruni kama siyo kuwasaddam hata kuwagadafi wao na mabwana zao.
Hakuna kitu kiliamsha Mwenembago wangu kama kuwasikia akina Saidi Mbaya aitwaye mwema na Emmy Nchimvi eti wakisema wataunda tume ya kuchunguza unyotoaji wa roho ya swaiba yangu. Nikiwa natamani haya majamaa niyakamate na kuyafanyia kitu mbaya nikasikia tena na Joni Tenda yule kibaraka anayeua viama akijidai anavisajili naye akisema eti ataifuta Chakudema. Audhubillahi minna shaitwaan rajiim niliomba Mungu amfute yeye kabla hajawaridhisha hao wahuni wenzake wanaoua watu kama swala.
Juzi niliandika juu ya wahishimiwa kuvuta mibangi na kunusa mibwimbwi. Inaonakena na hawa ndata wanaotumiwa bila kujitambua wala kutambua kuwa wanaowadedisha ni ndugu zao, nao wanavutishwa mibangi kama mbwa wakali ili waue kila wamuonaye.
Mbona hawaendi kuua majambazi na majembuzi waliotamalaki kwenye ulaji? Mbona hawaendi hata kuwakamata mafisadi achilia mbali kuwaua kama kweli hawa si majuha tena woga wa kutupwa?
Naona wale ndata wana mibomu na mitutu. Acha niishie wasije kunimwangosi bure.
Chanzo: Tanzania Daima Septemba 13, 2012.

No comments: