Thursday, 6 September 2012

Rais anapohongwa tuzo na kampuni uchwara


Rais Jakaya Kikwete akipokea tuzo toka kwa Ajay Vashee makamu mwenyekiti wa  NGO inayoshughulika na kilimo iitwayo Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN). Je hii ni tuzo kweli au nyenzo ya kuwa karibu naye ili kuwawezesha wahusika wapata deals za kutuibia. Viongozi wapenda sifa wanapokea kila upuuzi bila kuangalia hata hadhi yao. Je hii yaweza kuwa danganya toto kama ile ya Bernard Madoff na watawala wa Marekani waliomtunuku heshima nyingi wakati ni tapeli wa kawaida? Je Kikwete anapewa tuzo ya kilimo kwa lipi iwapo amekuwa akilima kwa mdomo chini ya sera yake ya Kilimo Kwanza ambayo haijalisaidia taifa zaidi ya kuwa kamba ya kupata umaarufu kisiasa?

No comments: