Wednesday, 5 September 2012

Laiti watawala wetu jeuri wangesoma somo la picha hizi!Abdullah al-Senussi with Col Gaddafi in 2009

Huyo hapo juu ni jamaa aliyewahi kusifika na kuogopewa nchini Libya wakati wa serikali ya Muamar Gaddafi. Ni Abdullah al Senussi mkuu wa usalama wa Gaddafi na mtu aliyemwamini sana. Senussi alielezewa kama Black Box ya Gaddafi yaani tuseme ubongo. Muangalie anavyoonekana akiwa hajanyoa na amewekwa mbaroni hata kujitetea hawezi. Kesha kazi waswahili wangesema. Anakabiliwa na mashtaka mbali mbali yakiwemo ya kuficha pesa nje kutesa na kuua. Mwisho wake ni wa aibu ambao waingereza huita fall from grace. Je watawala wetu wenye jeuri ya kuamrisha polisi waue watu kama swala wanajifunza nini tokana na matukio kama haya? Je wanajua kuwa zama zao zaweza kufika kwa namna ya kutia aibu hata kumwaga damu? Laiti akina Senussi wetu wangejua kuwa madaraka ni ya umma na ukiamua kuyarejesha mikononi mwake hawa wanaoonekana kuwa tishio si chochote wala lolote bali mbolea.
Jikumbushe na picha hizi ili kupata somo zaidi.

Saif al Islam Gaddafi siku alipokamatwa na hapo chini kila mtu anamfahamu bazazi huyu mwenda zake

No comments: