The Chant of Savant

Monday 22 December 2014

Je Tibaijuka ni kafara ya mwaka ya Kikwete?


Japo Profesa Anna Tibaijuka waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipaswa kutimuliwa, hakupaswa kwenda peke yake. Kama kawaida yake, bingwa wa sanaa za mazingaombwe Jakaya Kikwete amefanya vitu vyake. Kama alivyofanya kwa Edward  Lowassa mwaka 2008 ametoa kafara nyingine ya mwaka ili kuwaokoa wanawe wapendwa. Hata hivyo wengi wanajiuliza inakuwaje mtu aliyekatiwa kitu kidogo kwa sababu ya huduma za siri alizotoa kwa James Rugemalayer mmojawapoo wa watuhumiwa wa wizi wa fedha za umma kwenye fuko la escrow? Kikwete anasema tena bila aibu kuwa amewaweka kiporo waziri Nishati na Madini Profesa Sospiter Muhongo , Katibu wake Eliakim Maswi na Bodi ya Shirika la Umeme (TANESCO)ikiongozwa na Robert Mboma anayetuhumiwa kwa ufisadi wa kutisha na matumizi mabaya ya madaraka ili uchunguzi ukamilike atoe msimamo. Imekuwaje uchunguzi wa Tibaijuka ukakamilika haraka wakati wa hawa wengine ukisuasua au ni janja ya kuwakingia na kuwaokoa washirika zake? Kuna haja ya kumbana Kikwete aache kutuchezea mahepe kana kwamba hatuna akili.
Kwa hatua hii ya hovyo na kutia shaka ya Kikwete usishangae waramba makalio yake wakaandaa maandamano ya kumpongeza badala ya kumlaani kwa kuwachezea kila uchao.

2 comments:

Anonymous said...

Kwa sababu yupo nje ya genge huni la uhalifu, ikatokea kajiingiza kwenye hili bila kufahamu hivyo wamemkataa kumtetea kwa sababu siyo mwenzao kwenye kundi lao. Pia wataje majina hadharani ya wajumbe ya hiyo inayoitwa kamati ya maadili na muundo wake tufahamu isijekuwa ndiyo kamati ya species moja tuu, mfano Kima mwenyekiti, hakimu tumbili(Kama alivyosemekana Jaji na Mwanasheria Mkuu wa sirikali hivi karibuni alipojisogeza nje ya umma lakini akibaki pale pale kushughulikia mambo yale yale),Nyani wakili na Sokwe mshitakiwa..Tautegemea nini hapo?..

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon nimependa metaphor yako ya nyani, kima tumbili na ningeongeza gendaeka. Ubarikiwe sana na karibu tena.