Free Thinking

I Fear Nothing But Fear Itself

The Curse for Salvation

The Curse for Salvation

Wednesday, 31 May 2017

Forgery is boil but not goosebumps

President John Magufuli receives a report on
            Recently, Tanzania has been teetering and tottering with news revolving around chronic and systemic forgery. No news is good news. When news broke that the government would audit academic certificates and credentials for all its employees, for forgers, it was a read-it-and-weep sort of thing.  It came to pass that the government shockingly, found that about 10,000 souls were working on forged certificates, thus they lacked credentials. This number is bigger than expected and small than the real culprits. This means that, for years, the nation was losing millions if not billions of shillings to pay such half-backed employees. So, too, such an anomaly has, for many years, denied jobs to qualified jobseekers that the country has in thousands if not tens of thousands.
             Again, this noble exercise left many abhorrently dumbfounded and affronted. For, it excluded some connected politicos among who is one region nawab aka Bashiiite whose closeness to the raja seems to have worked miraculously to his advantage and the disadvantage of the raja. For, while others were weeping and gnashing teeth, the guy has gone on enjoying public yum-yum his position offers. So, too, while the forgers were grief-stricken for losing jobs and emoluments, for us with genuine credentials, it was “hooray at last this exercise has arrived!”
             Again, is this the end of the story really? Nay! We need to see all forgers being rewarded for their delinquency. They must be made to pay back through their nostrils the monies they undeservedly scooped for the entire time they were erroneously employed. Furthermore, provided that the Penal Code stipulates that whoever commits an offence be by commission or omission must be charged, they too must face the music so that we can send the right signals to those still contemplating to replicate the same offence.
            The story’s still fresh to say the least. How can it reach the apex while to some, forgery is a very stinking boil while, for others, it is but goosebumps? This is nothing but a systemic double standard resulting from systemic technical knows who. It is bad and surreal so to speak. For, our constitution clearly stipulates that we’re all equal before the law including equal in getting academic credentials; and punishing forgers. I’m not trying to be a nut-job as Don Trump would put it. Instead, I’m trying to be fair. So, those thinking I’ve lost my marbles should think again. I need; and cry for justice. This is why I’ve a big bone to pick with the whole exercise of rooting out forgers, be they big or small. A forger is a forger. He or she’s a criminal under our law regardless he’s a commoner, or a nawab. Therefore, I candidly submit that the timing and reasoning applied on hunting down forgers needs to be deconstructed if not overhauled so as to do equal justice for all.
            Time without numbers I’ve heard people complaining about the nawab in question to no avail. Again, the powers that be seem to turn a blind eye to this umbrage next to a sacrilege.
            Suffice it to say, although the noises about this consigliere are dwindling, soon such partiality will fall on its weight if common sense is to be entertained. There’s no logical reason for the raja to throw his reputation to opprobrium pointlessly. Therefore, it is not lost of me to say that the melee is offended by the ongoing antics in which some are sacred cows while others are the black sheep of the land. This hunk is our equally. We therefore must enjoy it equally.
Source: Citizen Wednesday today.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 05:47 No comments:

Tuesday, 30 May 2017

Magufuli: Mwalimu wa maendeleo Afrika?

Image result for photos magufuli mkapa, kikwete and mwinyi
            Kitendo cha hivi karibuni cha rais John Magufuli kufukua makaburi yaliyozika maendeleo ya Tanzania, hata Afrika, ni cha kupongezwa na kupigiwa mfano. Baada ya kustukia wizi wa ajabu na kikatili ambao umefanyika kwa miaka nenda rudi, Magufuli aliunda kamati ya kuchunguza usafarishaji wa michanga yenye madini au makinikia. Tume hiyo iliibua mambo mengi ya kukatisha tamaa na kutia moyo kwa wakati mmoja kama Afrika itakubali kubadilika, kuwajibika na kutumia akili badala ya utumbo.
            Kamati hiyo iliyoongozwa na profesa Abdulkarim Mrumu iliundwa na wataalamu wa madini, kemia pamoja na mengine. Wataalamu hawa licha ya kuonyesha umahiri katika taaluma yao, walionyesha uzalendo wa hali ya juu. Kwani, kama alivyosema rais Magufuli, kulikuwa na kila mbinu ya kuwahonga ili wasifichue wizi huu wa kikatili unaofanywa na makampuni ya kimataifa yakisaidiana na watanzania wasio na utu wala uzalendo.
            Kitendo cha Magufuli kinatoa masomo mengi mojawapo yakiwa:
            Mosi, kuna watanzania waliosomeshwa kwa fedha ya umma wanaoitumia kuuhujumu umma huo huo uliwasomesha na kuwaajiri.
            Pili, kumbe Tanzania na nchi nyingine nyingi za kiafrika zilizojaliwa raslimali lukuki ni maskini wa ima kujitakiwa au kusikinishwa na mfumo kandamizi na nyonyaji  na wa kikoloni wa kimataifa ambapo nchi zinazodaiwa kuendelea zimekuwa zikitajirika kwa kuziibia nchi maskini. Mfano mdogo ni kwamba, tokana na makontena 277 ambayo ni shehena ya mwezi mmoja, Tanzania ilikuwa ikipoteza kiasi cha takriban shilingi 1.441 trilioni sawa na dola za Kimarekani 644,137,499 ambazo ukizidisha mara 12 yaani mwaka mmoja na ukazidisha mara miaka 19 unapata jumla ya dola 146, 863,349,772 ambazo licha ya kuwa kiwango kikikubwa ajabu kwa nchi maskini kama Tanzania, ni mara takriban kumi ya deni la Tanzania la takriban dola 14,120,000,000 hadi hapo 31 Decemba, 2014. Na huu ni wizi wa kampuni moja na mgodi mmoja tu wa dhahabu. Je kwa makampuni yote makubwa na madogo yaliyotapakaa nchini yakichimba dhahabu na madini mengine ya thamani, Tanzania na Afrika imeishapoteza utajiri kiasi gani?
            Kwa kuangalia mahesabu hayo hapo juu, ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania haikupaswa kuwa nchi ombaomba bali ya kutoa misaada kwa nchi nyingine duniani. Hivyo basi, kama Afrika itakubali kubadilika na kujifunza tokana na mfano wa Magufuli, uwezo wa kugeuka bara tajiri kuliko yote kimaendeleo ni mkubwa na si jambo la kama inawezekana bali ni ukweli ulio wazi.
            Katika kitabu chake cha Africa Reunite or Perish, mwandishi wa makala hii anayadurusu matatizo makubwa ya Afrika kuwa ni ukosefu wa uongozi wenye akili timamu za kawaida yaani common sense kwa kiingereza. Kwani, anachofanya Magufuli ni kutumia common sense ikichangiwa na uzalendo na uchungu wake kwa Tanzania na Afrika ukiachia mbali hamu yake ya kubadili mfumo uliopo na kuleta maendeleo yenye kulenga kuinua hadhi ya mtanzania na mwafrika popote alipo.
            Sasa tuangalie baadhi ya masomo tunayoweza kupata tokana na mfano huu adimu na adhimu wa Magufuli.
            Mosi, si chuku. Inaonekana Magufuli ameamua kubadili msimamo wake dhidi ya kufukua makaburi aliyosema alikuwa akiogopa kuyafukia. Bila shaka, kwa safari aliyoianza, makaburi hayatanusurika hasa ikizingatiwa kuwa wizi huu uliasisiwa na wale waliojidanganya kuwa wanaweza kupona. Hapa lazima wote waliowahi kuwa mawaziri wa Nishati na Madini tangia mwaka 1998 wakae mkao wa kuliwa. Kama Magufuli atataka kukata mzizi wa fitina, lazima achunguze watangulizi wake ambao waliwapa fursa marafiki na wateule wao kuuza taifa kwa kuingia na kuridhia mikataba ya kijambazi iliyozaa wizi huu usio na huruma.
            Mbali na hili, kama nchi za kiafrika zikatkuwa nyepesi kujifunza, Magufuli anaingia kwenye vitabu vya historia kama kiongozi aliyejaribu na kuanzisha somo halisi la ukombozi wa Afrika litakaloiwezesha kutumia na kufaidi raslimali zake.
            Je Magufuli atafanikishaje somo hili? Hapa lazima awe tayari kuweka kujuana, urafiki na ukaribu kando ili kuweza kutenda haki na kufanikisha kile anacholenga kufanikisha. Hii maana yake ni kwamba, hataangalia sura ya au cheo, wala ukaribu wa mtu.
            Tumalizie kwa kuwataka waafrika na viongozi wao kutoona aibu wala kuchelewa kuanza kujifunza somo hili la ukombozi ambalo chimbuko lake ni Tanzania.  Wahusika wanapaswa kushirikiana na viongozi wao kutunga sheria zitakazowawezesha kusimamia mali zao huku wakitunga sheria kali za kupambana na wale wote wanaoibia bara letu wawe wananchi wenyewe au washirika wao toka ughaibuni. Wakati wa Afrika kuwa shamba la bibi unapaswa kuwa historia.
            Kimsingi, alichofanya Magufuli ni kujibu swali l a kwanini Afrika iwe tajiri wa raslimali lakini sambamba na hili iwe maskini kimaisha. Nadhani jibu limok wenye matendo ya kupongezwa na kujivunia ya rais Magufuli. Heko rais Magufuli. Je Magufuli atakumbukwa kama gwiji na mwalimu wa ukombozi na maendeleo ya Afrika? Mwenye macho haambiwi tazama.
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano kesho.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 14:42 No comments:

Kijiwe kwenda ikulu kumpongeza rais


            Baada ya kuvunja mwiko wa kugeuzwa kichwa cha mwendawazimu kulikofanywa na rais Joni Kanywaji Makufuli, kijiwe kinapanga, kwa dhati kabisa, kwenda ikulu kumpa tano kikimtaka akaze buti na kufumua sekta nyingine bila kusahau tanzanie, almas na madude mengine ya thamani bila kubakiza ardhi na mbuga zetu za wanyama.
            Akiwa anaonyesha wazi kufurahi na gazeti lake mkononi, Msomi  Mkatatamaa anaingia kwa staili tofauti. Maana, kawaida, huingia mpole na mkimya na mwenye mawazo kama dalili za usomi.
            Baada ya kuamkua, anamtupia gazeti Mchunguliaji na kusema “mwenzenu kwa mara ya kwanza leo nina furaha sina mfano. Nani aliamini kuwa profwedheha Sossie Muongo angetumbuliwa kavu kavu kama ilivyotokea? Bila shaka hata Bashite ajiandae kupambana na visu vya daktari mtumbuaji. Mijitu ilijisahau na kujiona miungu kwa vile inafahamiana na rahis. Sasa yako wapi?  Sitaki niwakawize, timua timua ya juzi ilimenikosha imenikosha. Nangoja kumuona mbele ya pilato na baadaye lupango akifanya vitu vyake kwenye mtondoo. Alikuwa anatutia aibu wasomi ukiachia mbali kuitia kaya hasara kwa kumsomesha akaishia kuitumia elimu yake kulihujumu. Yako wapi sasa? Tulionya tangu kashfa ya Escrow kuwa jamaa ni jipu tena linalotoa usaha wa damu tukapuuziwa. Yako wapi sasa? Mwanaharamu hata ukimficha kwenye chupa atatoea kidole nje.”
            Mpemba anadakia “wallahi kwa hili nakuunga nkono ami. Hata mie nfurahi sana; na naanza rejesha matumaini kuwa kweli hakuna mjanja mbele ya dokta Kanywaji. Kwa vile jamaa aonesha anza ona mwanga, nangoja kuona atavochukua hatua kwa wevi wengine ukiachia hatua nyingine dhidi ya huyu Muongo. Maana washatuliza. Lazima nasi tuwalize ati. Haiwezekani wendelee tugeuza bichwa la mwendawazimu kama so shamba la bibi ati. Mijitu inafanya vitu kana kwamba haikwenda shule yarabi! Sasa faida iko wapi kupoteza njuluku za umma kuisomesha tusijue ingejaza ujinga vichwani kiasi cha kutumia masaburi badala ya vichwa? Inauma; nyie achene tu.”
            Mipawa anakula mic “yote tisa mie nangoja kuona kama kweli wote walioasisi ujambazi huu ulioingiza kaya kwenye umaskini watashughulikiwa. Hapa sijui kama rafiki yake Njaa Kaya ambaye aliingia mingi ya mikataba ya kijambazi atamnusuru na abaki na udhu kama mpiganaji wa kweli.”
            Mogshi Machungi anakwanyua mic “Waahi hii imefuaisha kiasi cha kutitaka sisi kama wana kijiwe tiende ikuu kumpongeza doktai Kanywaji ii kumtia moyo na hamasa. Nadhani hapa titamkuna kiasi cha kumuacha hoi.”
            Mijinga anampoka mic na kulonga “ni bahati mbaya sana walio karibu na daktari wa majibu hawamjui vizuri. Huyu jamaa ni wa nyumbani namfahamu sana. Hata akina Denjaman Makapi na Njaa Kaya usishangae siku moja arobaini yao ikafika. Bila shaka ndugu yangu Jimmy Rugemalayer na Singasinga hawalali usingizi. Kwani arobaini yao naiona inawasogelea bila wao kutarajia. Halo halo!”
            Kapende anakwanyua mic “pamoja na hili kuwa jaribu kubwa kwa Kanywaji, bado tusiache kumpongeza japo kwa kuthubutu kupambana na mfumo huu zandiki wa kikoloni na kinyonyaji. Walizoea kutugeuza vichwa vya wendawazimu machizi kujifunzia kunyoa. Acha sasa nao wanyolewe tena bila maji. Hawajui misheni ya dokta Kanywaji hawa. Hawajui kuwa alijiandaa kuwa mkuu na si kwa bahati mbaya kama Njaa Kaya na Makapi mzee wa uvivu wa kufikiri. Sasa itakula kwao.”
            Mheshimiwa Bwege anakamua mic “mie nitashangilia siku nikiona mimali waliyokwanyua inarejeshwa huku nao wakipelekwa lupango wakafanyiwe kitu mbaya na kufia huku wana hizaya hawa. Ni bahati mbaya kuwa dokta Kanywaji amezungukwa na vipofu na viziwi tena wanaojiachia wasijue mwenzao ana mipango mikubwa na kaya yetu. Laiti wachovu wote wangemwelewa hata nusu, kaya ingepaa kimaendeleo na kuheshimika kimataifa. Lazima tumpe tafu awatumbue mabwege wote wenye mizigo kama kughushi, kuibia umma na ufisadi.”
            Kanji anakula mic “duguni yangu, mimi iko na vazo. Kwanini jive siandae tuzo na kuchunuku hii dokta ya Jipu ili jipu yote hata kama nakaa kwake jumbani ijue mambo iko badilka sana?”
            Kabla ya kuendelea da Sofia Lion aka Kanungaembe anamchomekea kwa kumkosoa “Kanji siyo kuchunuku bali kutunuku au nawe ni sawa ni ile gabachori naita dokta Kanywaji Mapombe Makufuri? Iko unga kono vazo lako Kanji. Tukiacha utani, japo nilikuwa naye maya kwa kuvunja nyumba ya mjomba wangu pale Jangwani Bondeni, sasa namsamehe na nimekubali kinoma huyu mwamba wa maendeleo na uzalendo. Nitume fursa hii kupendekeza kuwa tukienda ikulu kumpongeza lazima tumkumbushe kuacha wanasiasa wafanya siasa ili wasimharibie. Maana nijuavyo haya manchi fadhili yanaweza kutumia hii kumhujumu.”
            Mzee Kidevu anakwanyua mic “mie nikienda nitamshauri awe macho na wale waliomzunguka hasa ikizingatiwa kuwa anagusa ulaji wa wengi. Maana hata Isa bin Mariam au Yesu alisalitiwa na mijitu kama Muongo. Hivyo, achunge wale wanaojifanya wanamhusudu na kumuabudia.”
            Kijiwe kikiwa kinanoga mara tukasikia kelele za machinga wakizomea shangingi la Muongo aliyekuwa akipita kuelekea Relini.
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano kesho.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 14:39 No comments:

Sunday, 28 May 2017

Magufuli Amtumbua Kamishina Mkuu wa Polisi

Image result for photos of mangu and sirro
Image result for photos of muhongo and magufuli
Mwezi wa Mei utaingia kwenye historia kama wa uamsho wa utumbuaji ambao anaufanya rais John Magufuli. Hii ni baada ya kuwa amelaza zoezi la utumbuaji kidogo, juzi Magufuli alimtumbua rafiki yake aliyekuwa waziri wa Madini na Nishati profesa Sospeter Muhongo baada ya kutimua watendaji na bodi wengi wa Mamlaka ya Ukaguzi wa Madini au Tanzania Mineral Audit Agency (TMAA). Kama haitoshi, leo amewashangaza watanzania kwa kumtumbua Kamishina Mkuu wa Polisi (IGP) Ernest Mangu na kumteua Kamada Simon Sirro kuchukua nafasi yake. Nadhani sasa wengi wanangojea kujua ni lini atamtumbua Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda aka Daudi Albert Bashite.
Image result for photos of magufuli and makonda
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 10:38 No comments:

Graves, Magufuli, mineral sands and Muhongo

            When President John Magufuli’s told to revisit scandal-laden former regimes, he said he’d not exhume graves for the fear of not being able to re-cover them.  It’s as if Abyssus aabyssus invocat or deep calls to deep; or hell calls to hell while, in reality, noises were for the love of the nation. Again, when Magufuli axed the former Energy and Mineral Minister, Prof Sospeter Muhongo, I wasn't shocked. If I may say but one thing, I saw it coming the day Magufuli ordered the formation of the squad to probe gold and copper remnants in mineral sands. Naturally, whenever the person that entrusted power in you forms a taskforce to look into your actions, take note. You’re done. What’s essentially left when such a thing occurs is when, but not, if you’ll face the music.
            Muhongo’s fate’s sealed when the taskforce exhumed a lot of rot in mineral business whereby since 1998 Tanzania’s been allowing its mineral sands to be exported without being thoroughly checked; thus, acting as a conduit of concealing the actual amount of minerals mined and exported.
            Again, an Igbo proverb has it that a man who doesn’t know where the rain began to beat him cannot say where he dried his body. Muhongo, too, didn’t know when it started raining on his parade. Had he known, he wouldn’t be caught pants down. None the less, Magufuli’s warned that Muhongo’s a boil after being implicated in a multibillion scam famously known as Escrow. It’s alleged that Muhongo was one of the recipients of Tshs. Billions from the architect of the scam, James Rugemalira. As a Swahili proverb says, love is always blind. Being a friend, Magufuli decided to ignore all noises the media and activists made. He, thus, went on appointing Muhongo to such a very important ministry without knowing that he who scoops honey doesn’t do it once.
             Now that Muhongo’s dirty linens are in the agora for everybody to see, what next as far as Muhongo is concerned? For, his role in sabotaging the country–this is according the report released by the taskforce Magufuli formed–is highly noticeable and unconcealable to say the least. Who wants to hide an elephant in the sitting room?
            Now, the prima facie verdict is out. What’ll the government do about Muhongo and the whole coterie of saboteurs that used their positions to ruin the country? I remember. Magufuli once said that he’s afraid of exhuming graves for the fear of failing to cover them thereafter. Those who don’t know what graves means, they’re just blunders and criminality Magufuli’s predecessors committed when in power. Even this simmering scandal’s its root from two previous regimes. Thus, it’s more of a grave in this context than a mere scandal. Will it be stymied or much must be expected?
Source: Citizen Sunday today.
            There are many important questions behind these revelations. First, for how long Tanzania’s been robbed pointlessly simply because some of its officials decided to collude with foreign carpetbaggers who come as investors while they actually are but robbers? How much money’s the country lost?  Which foreign companies or countries are involved in this sabotage?
            To make matters worse, the taskforce discovered that even the scanners used at the Dar es Salaam Harbour are flawed. This means, Tanzania hasn’t only been losing in minerals but also in other resources such as Rhino horns, elephant trophies and others. Again, who purchased these gadgets, from which countries, for how much; and for how long have they been operating? If this is the case, can Tanzania stop becoming a good entry point for drugs?  For, if you look at such an anomaly deeply, you find that there are so many things that have been going on that the general public; and government doesn’t know. Further, this speaks to the fact that there’s a syndicate behind this sabotage.
            When it comes to the exhumation of graves, many’d think that given that the graves are now opening themselves, the president should change his stance on them.  So, too, there’s no way he can turn a blind eye on them provided that everything is now open and clear.
            Will Magufuli stick to his guns while his country is robbed wantonly? Ironically, if you look at the trend of Tanzania, much time’s spent by two former presidents, Benjamin Mkapa and Jakaya Kikwete travelling abroad in their begging missions while their governments were blindly allowing a few crosiers to rob the country. What’s been unearthed in Tanzania is but a typical replica of what’s been going on almost in all African countries with minerals and other resources. This has to stop now. This is why Africa’s poor not simply because it was created poor. It is because of having leaders devoid of probity and patriotism, simple.
            Again, if Muhongo has been shown the door, even Bashite will one day.
Source: The Citizen Sunday today.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 06:50 No comments:

Saturday, 27 May 2017

Makaburi, makinikia, Magufuli na Muhongo

Image result for photos of magufuli and muhongo
            Japo rais John Magufuli aligoma kufukua makaburi kwa hofu kuwa angeshindwa kuyafukia, sasa makaburi yanajifukua yenyewe ili watanzania wayachunguzee; na baadaye wayafukie. Tukio la hivi karibuni la kumtumbua rafiki yake kipenzi profesa Sospeter Muhongo aliyetuhumiwa kunufaika na fedha za wizi katika kashfa ya mabilioni ya Escrow ni ushahidi tosha kuwa sasa makaburi yanaanza kujifukua ili watanzania wayafukie.
            Hata alipoonywa kuwa Muhongo ni jipu, tena la kunuka, Magufuli alitumia mabavu na madaraka yake kumsafisha na kumteua tena asijue la kufa halina ubani. Abyssus aabyssus invocat walatini walisema yaani jehanamu huita wa jehanamu! Tusisitize hapa: Kama siyo kutumia ubabe, rais Magufuli hakupaswa kumrejesha profesa Muhongo tena kwa kumzawadia nafasi tena nono na nyeti ili aendelee kufanya mambo yake kwa mazoea. Marehemu baba wa taifa Mwl Julius Nyerere aliwahi kusema: Kwa mke wa Kaisari kosa si kutenda kosa bali hata kutuhumiwa. Hata hivyo, hongera kwa kumtimua Muhongo na pole kwa kumteua hata alipotuhumiwa.
            Sasa ukweli umeishadhihiri shahidi. Je nini kifanyike katika kushughulikia haya makaburi ambayo rais anayaogopa kuyafukua kwa vile atashindwa kuyafukia? Tunapendekeza yafuatayo:
             Mosi, wahusika wote waliosababisha hasara hii ya mabilioni wunguliwe mashtaka kuanzia mwaka 1998 wote waliowahi kutumikia wadhifa huu ili haki kwao na kwa watanzania itendeke. Kwani wanajulikana na wapo tena wana ukwasi usioweza kutolewa maelezo.
            Pili, mali zote zinazomilkiwa na watuhumiwa au washirika zao zikamatwe na kutaifishwa wakati uchunguzi wa namna walivyozipata ukiendelea.
            Tatu, kwa wale waliokwisha kustaafu na kufa, warithi wao wanyang’anywe mali zote walizopata au kurithi toka kwa marehemu.
            Nne, serikali itekeleze ushauri wote wa tume iliyochunguza sakata hili huku ikihakikisha vyombo vya usalama vinajikita kwenye kulinda mali za umma badala ya kuhangaishwa na masuala ya kisiasa likiacha nchi ikiibiwa kana kwamba haina vyombo vya usalama.
            Tano, mikataba yote ya madini ikaguliwe na kuangalia kama imekidhi viwango na itakayokutwa inaruhusu wizi huu wa ajabu ifutiliwe mbali huku wahusika wakilazimika kuingia mikataba mipya au kupigwa marufuku kufanya biashara nchini. Hili suala si la mchezo. Ni suala la usalama wa taifa. Hivyo, wale wanaojidai kutetea uwekezaji wa kijambazi kama huu wasisikilizwe zaidi ya kuchunguzwa kama kuna namna wanavyonufaika na jinai hii kwa taifa.
            Hebu tujiulize kama taifa sakata hili limetupa somo gani ukiachia mbali kuacha maswali mengi bila majibu kama vile:       
            Je tumeishaibiwa kiasi gani kwa miaka yote hii ambayo mambo yamekuwa yakijiendea? Na fedha hiyo ingeweza kulisogeza mbele kimaendeleo kiasi gani? Je wahusika ni nani? Lazima wasakwe na kutangazwa kwenye vyombo vya umma ili umma uwajue na kuweza kutoa ushahidi pale serikali itakapohitaji taarifa zao. Pia ni vizuri kujua wahusika wana mali kiasi gani iliyotokana na ujambazi huu wa wazi ili kuweza kujua ni kiasi gani kilitoroshewa nje na washirika wao kwenye jinai hii ambao pia tunaweza kuwaandama warejeshe fedha zetu; na wakigoma tunashika mitambo na mali zao walizo nazo nchini.
            Pia lazima serikali itunge sheria za kuepusha kurudi au kuendelea mchezo huu wa kuligeuza taifa shamba la chizi siyo la bibi maana shamba la bibi angalau hubakiza mabaki kwa ajili ya wajukuu.
Takukuru na usalama wa taifa ni wa nini na wanafanya nini? Hapa lazima wachunguze hii syndicate nzima na wanufaika wakamatwe na kutaifishwa tena haraka sana kabla hawajavuruga ushahidi au wengine kukimbia nchi hasa ikizingatiwa wengi ni wageni.
            Lazima, kama taifa tutoe somo kwa nchi nyingine za kiafrika ambazo viongozi wake hupoteza muda na fedha nyingi kwende kujidhalilisha kuomba wakati makampuni ya kimataifa yanayotufanyia hivi yanatoka kwenye nchi. Hapa bila shaka lazima Magufuli afukue makaburi.
            Mbali na yaliyotajwa hapo juu, kuna haja ya kuangalia na sekta nyingine kama vile viwanda, mashamba, vitalu vya kuwindia na kila aina ya biashara inayohusiana na mali ya umma bila kusahau kuziba mianya iliyotamalaki mipakani ambapo mali nyingi za taifa hupitishwa wakati zikitoroshwa nje kwenda ng’ambo au nchi jirani ambazo nyingi zinajisifu kuwa wazalisha wa madini ambayo hazina hata chimbo moja.
            Mbali na wizi wa madini yetu, taarifa za kamati ni kwamba hata scanners zilizofungwa bandarini ni bomu. Je nani walinunua scanners hizi; kwa fedha kiasi gani, toka nchi gani na zilianza kufanya kazi lini? Hii itasaidia kutathmini ni kiasi gani Tanzania imeishaibiwa ili hata itakapochukua hatua dhidhi ya wahusika ijue ukubwa wa hasara inayoshughulika nao. Pia kuna haja ya kuyabana makampuni au watu walionufaika na wizi huu ndani na nje ili warejeshe fedha yetu tena ikiwa na interests juu. Je wamelitia taifa hasara kiasi gani? Nao wakamatwe na kushughulikiwa baada ya kutaifisha mali wanazomilki.
            Tumalize kwa kuipongeza serikali angalau kwa kuamka usingizini na viongozi wake kuonyesha uzalendo wa hali ya juu. Tunadhani huu ni mwanzo ambao utasambaa nchi nzima katika sekta zote zenye kutia shaka ili kubadili na kuliendeleza taifa kwa kutumia raslimali lilizojaliwa na Mungu.
Chanzo: Tanzania Daima Jumapili leo.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 21:10 No comments:

Eti Dom ni the big city of Bongo? Wow!


            Baada ya kufichuliwa madudu kwenye vitabu vya kiada kayani, walevi wengi walipigwa na butwaa kiasi cha kuamua kuhoji hata kama ni kilevi. Wengi walisikika wakitukana matusi ya nguoni ambayo pamoja na ulevi wangu siwezi kuyarudia.
            Kisa chenyewe kilianza pale ilipogundulika kuwa moja ya vitabu hivi hatarishi kimeandika eti Dodoma is the big city of Bongo; kikimaanisha mji mkuu. Huu ni ushahidi kuwa waliotunga hivyo vitabu ni vilaza, vibashite na vihiyo waliopaswa kuwa wanauza nyanya badala ya kupunyua mabilioni ya walevi ili kuwajaza sumu na ujinga vitegemezi vyetu. Na hapa lazima kuwa na mkono wa mtu mkubwa tena fisadi wa kunuka. Maana, bila hivyo, haiwezekani upuuzi kama huu ukafanyika tena kwenye sehemu nyeti ya ilm. Hapa lazima kuwa na majipu tena makubwa na yanayonuka yaliyoiva yakingoja kuguswa ili yatumbuke. Mnawanyima kazi watunzi wenye uwezo kwa kuendekeza njaa wakati hata sifa ya kuandika vitabu vilivyokwenda skuli hamna? Shame on you and kumbaff sana manyang’au nyie wana hizaya wajalaana na walaaniwa wakubwa. Hamna aibu wala maana. Heri yetu walevi kuliko nyinyi mnaojitiatia wasomi wakati ni vibashite vitupu.
            Baada ya kuinyaka Mlevi mmoja msomi akatoa mpya kuwa tujiandae kusikia vituko vingine. Hivyo usishangae kusikia mkiti wa CCM akiandikwa kwa kitasha kama the owner of the chair of CCM or the party of coup d’etat is John Alcohol Magufuli and the first wife is Mama Janet Magufuli.  Pia usishangae kusoma kuwa dini kubwa nchini ni Jesusism and Islamism. Sitashangaa kusikia watoto wakifundishwa kuwa the biggest mountain of Africa is Kilimanjaro na the largest Lake is Nyanza au the big sheik of Tanzania is so and so.
            Kesho utasoma the big minister of Tanzania is Katelephone Endowment Katelephone kama siyo big judge is professor Juma na mengine mengi. Hivi hawa walioandika utumbo huu walisomea wapi na lini? Je nani huyu mwenzao au wenzao waliowapa hii tenda ya mamilioni kujaza sumu na urongo kwenye vichwa vya vitegemezi vyetu? Je wanene wetu walikuwa wapi; au ni kwa vile wanapeleka vyao ughaibuni kupata elimu mufti huku vitegemezi vya walevi vikijazwa ujinga wa kudumu na kununua kwa kodi zao zinazotumika kuwalipa vilaza walioandika vitabu husika?
            Heri wangesema the biggest city of Bongo is Dar Si Salama but not Dom. Kwa sababu hata kama tutachukua mantiki ya lugha iliyotumika, bado Dodoma si kubwa kuliko Mwanza wala Arusha. Sitashangaa kusikia wakisema enchilada ni sambusa badala ya samosa kwa kitasha sahihi na mufti. Sishangai kusikia kuwa vitabu vingi ni mabomu. Kumbe ndiyo maana vyangu wetu wanaojifanya wapiga buku pale Chuo kikubwa cha Manzese wanabukanya! Utamsikia akisema “my milk are still standing and I’m a handsome lady that’s looking for a beautiful man to marriage me.” Juzi nilimsikia dingi mmmoja tena dingi kwelikweli akisema the deal had a lot of controversials badala ya controversies. Kama haitoshi aliongeza tell your children to come Bongo badala ya to come to Bongo! Jamani, kuna haja ya kujifunza lugha za watu kwa ufasaha japo kidogo kuliko kutuletea aibu na broken na mibomu yenu. Kumbe kuna akina Bashite kila sehemu hata kwenye elimu yenyewe! Hawa waliondika upuuzi huu wapelekwe kwa pilato na kufungwa maisha huku wakiamriwa warejeshe njuluku ya walevi na wawaombe msamaha kwa kuwajaza sumu vichwani vitegemezi vyao.
Hawa wafichuliwe hadharani na kuchukuliwa hatua. Maana ukiona hivyo wameishapunyua njuluku za umma.
            Ukikutana nao mitaani wanavyojidai wamepiga buku kumbe bashit mtupu.  Kama nilivyosema, hawa wafikishwe kwa pilato lau wakanonihino kwenye mtondoo au debe kule lupango.
Kwanini mnawalisha vitegemezi vyetu ujinga wakati wenu mkipeleka majuu ili visome vilivyo na kuja kuwala na kuwatawala vitegemezi vyetu? Kwani hatuwajui vitegemezi vya vigogo ambavyo sasa vimerithi ulaji wa wazazi wake kwenye ofisi za umma huku vikila kuku kwa umma watokanao na mali ya umma isiyouma? Kawaulize akina Jan Makambale, Hussy Muinyi, Emmy Nchimvi, Riz Kitwitwi, Sal Kitwitwi na wengine wengi wanaoendelea kutanua tokana na kuwa na majina makubwa.
            Kwa tamaa na upogo na ulafi wenu, mmeua watunzi na wachapishaji mahiri wa vitabu kwa kutaka kujipa tenda wakati hamnazo wala uwezo wa kutoa vitu vilivyokwenda shule? Hapa Dokta Kanywaji asipomtumbua mtu najinyotoa roho au kuhama kaya. Je mazabe haya yalianza lini na yameishaiingizia kaya hasara kiasi gani? ukisikia collective imbecilization si nyingine bali hii. Nina hasira sitatafsiri neno hilo lenye kufurahisha. Kwanini,kama kaya hamuoni hata aibu? Mnadhani mtaishi milele wakati mu makaburi yanayotembea? Shame on you! Mnatuimbia wimbo wa kuingia karne ya 21 ya sayansi na teknolojia wakati mnaendelea kufanya mambo ambayo hata Adam na Eva wasingefanya kwa kuogopa kuchekwa. Senzi kabisa na mkome na mkomae na broken zenu zitokanazo na kukwepa kupiga buku huku mkitumia masaburi na utumbo kufikiri badala ya vichwa.
Chanzo: Nipashe Jumamosi leo.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 06:48 No comments:

Thursday, 25 May 2017

Wiki hii nimekumbuka Botswana baada ya Tanzania kustukia wizi kwenye madini


Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 16:51 2 comments:

Wednesday, 24 May 2017

Leave Tanzania out of Kenya’s upcoming election

  

              Recent damning allegations made by Majority leader Aden Duale that the NASA has established a pony-trekking center in Tanzania are shocking. Up until now, I don’t know the rationale behind such jaw-dropping allegations; made without being substantiated. On 12th March, 2017, the Daily Nation quoted Duale as saying that”it is outrageous that a top Cord leader, who has been at the forefront of claiming that Jubilee would rig the elections, is linked to repeated attempts to infiltrate the IEBC database through hacking.” Thereafter, on 7th May was videotaped alleging that the center for hacking was established in Tanzania http://www.nation.co.ke/video/1951480-3917548-1gka5pz/index.html 
            Although such murky and toxic allegations were aired on a political rostrum, Jubilee needs to know the type of the country they are dealing with. We all know that the president of Tanzania, Dr. John Magufuli, is the personal friend to NASA’s flag bearer, Raila Odinga. However, personal friendship has nothing to do with national issues. Again, why did Duale make such damning and unsubstantiated allegations? What are likely to be the effects and consequences of such allegations? Why such careless allegations are made at this time the relationship between Kenya and Tanzania is a wee bit frosty? is there what's cooking many Kenyans do not know? Suppose Tanzania takes such allegations seriously?
            Swahili sage has it that “akumulikaye mchana, usiku hukuchoma” or he who shines lights on you during the day, torches you at night (my translation). I don’t want to believe that Jubilee is that desperate so as to smudge the image of the country resulting from its grudges and vendetta. Is there any bad blood between the Jubilee government and Tanzania? Is there any big bone to pick with Tanzania? Is such a move psychological preparations for unexpected come August? There are many more questions than answers so to speak.
            Now, what should be done? The NASA must ask Duale to substantiate his allegations before Tanzania does so. So, too, Duale should be squeezed to know if such allegations are personal or his party’s position vis-à-vis such criminality that aims at impairing democracy in Kenya which is not only treason but also espionage. It is not a small thing for a foreign country to abet with whoever that wants to superimpose the president to another country. currently, the US is at loggerheads with Russia after it came to light that Russia meddled with the 2016 US elections in which the person sought to be in cohort with Russia, president Donald Trump (Republican) defeated his challenger Hilary Clinton (Democrat).  Again, why will Tanzania need to superimpose its choice for president on Kenya in the first place?
            Knowing how a no-nonsense Magufuli is, I doubt, if something is not done, the relationship between Kenya and Tanzania is likely to take a hit. To avert such an enigma, president Uhuru Kenyatta and Jubilee need to tame its loose cannons. To dispel the ruckus Duale’s misguided allegations can cause, Kenya needs to come clean on them forcefully and timely. As a Tanzanian who believes in the oneness and the unity of Africa that unfortunately is amiss, I’d like to see Kenya and Tanzania coming together but not to be torn asunder. Again, with such patterns and practices Jubilee is applying without clearly considering the timing and reasoning are likely to affect not only Kenya and Tanzania but the entire region. If Duale has lost his marbles, he should not only be tamed but also openly reprimanded for attempting to poison the relationship between the duo pointlessly. I would argue that Duale needs to avoid the generalisation of the genre of politics in that the way it is conducted in Kenya it is completely different from how it is done in Tanzania.
            In a nutshell, Jubilee needs to understand that Kenya is bigger and more important than a mere political outfit. Healthy relationship between Kenya and Tanzania is more important than power Jubilee is seeking to retain. Therefore, instead of using smear campaigns and scare politics, Jubilee needs to put its house in order instead of looking for farfetched pretexts shall anything happen in the coming elections.
Source: The Citizen Wednesday today.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 08:50 No comments:

Nani anakumbuka mauji ya kipumbavu kama ya Mvumi?

 Image result for picha za wahanga wa iringa mvumi
Tukio la kusikitisha la kinyamana na kipumbavu lilotokea Oktoba 1, 2016 huko kijijini Iringa Mvumi lilistua na kuchukiza wengi ukiachia mbali kwa taifa. Wataalamu wawili wa  Udongo na dereva wao toka kwenye kituo cha Seliani mkoani Arusha waliuawa eti kwa kudhaniwa ni wanyonya damu au mumiani.  Hii maana yake ni kwamba bado tunajenga taifa la watu mbumbumbu, washirikina na wakatili wanaoweza hata kuondoa uhai bila kujiridhisha kuwa kile wanachoshuku ni kweli au siyo. Tukio hili lilitangazwa na kulaaniwa nchi nzima wakati ule. Hata hivyo, baada ya kujitokeza upungufu wa namna hii kwenye uelewa na imani za wananchi wetu, wahanga walizikwa na huo ukawa ndiyo mwisho wa habari yao. Hatujui nini kilitokea kwa familia za wahanga kuhusiana na stahiki zao kama mafao, fidia na mengine kama haya. Leo kwa makusudi mazima, tunajikumbusha tukio hili la kikatili na kutisha lau kukumbushana kama jamii na taifa ili kuepuka kurudiwa mahali pengine nchini.
Kwanza, tunajitahidi kuvaa viatu vya wahanga au wapendwa wao kuona nini tungetaka tufanyiwe baada ya kukumbana na mkasa kama huu ambao bila shaka mwenye kulaumiwa ni serikali kwa kutowaelimisha watu wake vya kutosha ukiachia mbali kutokuwa na mfumo wa haraka wa mawasiliano ambao ungeweza kuepusha vifo hivi vya wataalamu na hasara ambayo taifa lilipata tokana na ujima na upumbavu huu.
Ni bahati mbaya kuwa wahanga wa kadhi ahii walikuwa wakipambana na kutumia ujuzi wao kuwasaidia hawa hawa waliowaua kutokana na hisia na imani za kipumbavu. Ni hasara na unyama kiasi gani? Tunashauri serikali ieleze namna ambavyo ilizifidia familia za wahanga wa ujinga wa taifa unaotishia kuliteketeza taifa letu. Kama haijafanya hivyo, tunaandika kuikumbusha wajibu wake hasa ikizingatiwa kuwa wahanga waliacha wapendwa wao waliokuwa wakiwategemea.
 Inashangaza kuona baadhi ya watu wetu wakishabikia na kushiriki mauaji ya kujichukulia sheria mikononi kama vile kuchoma moto vibaka wakati wakiabudia na kuvumilia mibaka mikubwa tu. Lazima tuseme wazi kuwa kosa hili si la wauaji wa Iringa Mvumi pekee bali taifa kwa ujumla hasa wale walioteka uhuru wetu na kuwajaza watu wetu ushirikina na ujinga. Kusema ukweli, tuna mfumo mbovu wa kishirikina na kipumbavu ambapo matapeli wachache huruhusiwa kuhubiri sumu ima kupitia dini au uganga wa kienyeji. Rejea mauaji ya mara kwa mara ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Je sasa nini kifanyike? Tutaotoa baadhi ya maangalizo hapa ili kuepusha kurudiwa kwa aibu na unyama huu ambavyo ni pigo kwa taifa:
Mosi, wataalamu au watu wetu wanaoingia kwenye maeneo mageni ima wapewe ulinzi wa askari au waruhusiwe kupeperusha bendera ya taifa kwenye magari yao. Kwani, watu wetu wamezoeshwa kuogopa bendera kama alama ya serikali.
            Pili, wananchi wetu waelimishwe namna ya kuheshimu na kutumia sheria. Inasikitisha kuona kwenye karne ya 21 bado Tanzania ina watu wasiojua hata namna ya kuripoti matukio au watu wanaowashuku hadi wanajichukulia sheria mikononi kama ilivyotokea hivi karibuni huko kwenye kijiji cha Iringa Mvumi mkoani Dodoma.  Jambo linaloonyesha kuwa tumefika pabaya sana kimfumo na kijamii ni ile hali ya serikali kuchukulia mauaji husika kwa wepesi sana. Kama ingekuwa inachukulia kadhia kama hii kwa uzito, tungesikia lau bungeni suala kama hili likijadiliwa na wabunge ili kuangalia nini kifanyike. Wahanga wa Iringa Mvumi wamesahaulika; na hakuna anayewaongelea ili kuepusha kadhia kama hii kutokea tena nchini.
            Sijui kama waziri wa mambo ya ndani analo tena kwenye kumbukumbu zake hasa wakati huu mauaji mengine kama yanayoendelea Kibiti yanaposhamiri. Vinginevyo, tungesikia lau wamepewa hata nishani au zawadi za utumishi bora katika mazingira hatarishi ambayo yaliwagharimu maisha yao. Lazima wahanga wakumbukwe kwa namna ya pekee. Kwani walikufa kazini wakitekeleza kauli ya “Hapa Kazi Tu” ya rais John Magufuli ingawa hakuliona hilo. Namuuomba na kumshauri rais aliangalie hili kwa uzito wa pekee ili kujua namna familia za marehemu zinavyoendelea.  
            Mwisho, katika kuwakumbuka wahanga wa Iringa Mvumi, serikali iangalie namna nyingine ya kukomesha kadhia hii ni kwa serikali kuwachukulia hatua watendaji wake waliowezesha kujengeka mazingira ya uhasama na kutoaminiana miongoni mwa wanakijiji uaji ambao inasemekana walishachoshwa na mauaji yanayodaiwa kutekelezwa kwa maagizo ya mwanakijiji mwenzao aliyekuwa akilindwa na wakubwa wilayani Chamwino kama gazeti moja la kila siku lilivyofichua. Hawa walipaswa kuwa korokoroni huku uchunguzi wa kina ukiendelea ili kupata ufumbuzi wa kudumu.   Hii ndiyo namna ya pekee ya kuwafariji jamaa za marehemu na kuwaenzi marehemu waliokufa kutokana na ujinga ulioachiwa kutamalaki nchini ukiachia mbali imani za kishirikina ambacho ni chanzo kizuri cha mauaji haya. Hivi kweli Tanzania bado kuna mumiani katika karne ya 21? Ni aibu kiasi gani!     
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 08:45 No comments:

Kijiwe kukamata mali za mafisadi


            Baada ya taarifa za kufumka kashfa ya ufisadi wa kutisha ambapo mhalifu fulani wa Tume ya Kupamba na Kueneza Rushua, sorry Kupambana na Kuzuia Rushua (TAKUKURU) kukutikana akimiliki mimali yenye utata ya mabilioni, Kijiwe kinataka kuisaidia sirikali kuanza kuwafichua wote wenye utajiri wa kutia shaka tena ambao wanajulikana hata kwa kunguru.
            Mpemba ndiye analianzisha leo. Baada ya kuamkua anakula mic “yakhe mmesikia hii skandali ya mkubwa wa kuzuwia rushua kukutwa na ukwasi mkubwa utokanao na kadhia aloajiriwa kupambana nayo akaishia kuishirika na kuipamba?”
            Kapende anajibu “nimeyasikia haya japo sijashangaa. Hakuna jipya hapo. Hao mbona wengi na wamefanya kaya yetu iwe maskini kwa kupewa cha juu na kuacha ihujumiwe na magabachori na sasa wachukuaji waitwao wawekezaji ukiachia mbali wazungu wa unga? Mbona wanajulikana na kila mtu hata ndege na wadudu? Hapa nadhani suala si kuongelea kutokea kwa hili bali namna ya kupambana nalo; au vipi?”
            Mgoshi Machungi anachomekea “nakubaiana nawe. Hapa lazima tianzishe utaatibu wa kia mwanakaya kutangaza, kukaguliwa na kueeza namna aivyochuma ukwasi wake ii tisiendee kuibiana kama iivyo sasa ambapo mbuua wachache wanaendee kugeuza kaya yetu shamba la chizi. Tena katika kutangaza ukwasi wetu tiepuke mambo ya kibashitebashite kama iivyo sasa ambapo kaisai ameonyesha wazi kumbeba habithi huyu hata aiposhutumiwa kuwa na mimai kibai yenye kutia shaka.”
            Mijjinga anakula mic “hata nami nakubaliana na wazo la kuamua kuwatolea uvivu wezi wetu ambao wengi wao wanatukoga utadhani wamechuma kwa stahiki au ujanja wao. Hapa, kama kijiwe, tuanze kuzitambua mali husika, ziko wapi, ni kiasi gani, zinamilkiwa na nani, halafu tuzivujishe kwenye vyombo vya habari. Nashangaa hata vyombo vyetu vya habari vimeshikilia siasa badala ya kufanya uchunguzi wa majambazi kama hawa ili watiwe adabu na kurejesha njuluku zetu.”
            Kapende anakula mic “Mijjinga hapa umemena bro. lazima tufanye utambuzi kwanza ili tuanze ukamataji au uvujishaji wa mali husika. Ni rahisi kuwatambua wezi wetu waliotumia ofisi zetu kujineemesha. Mfano, unakuta kijana kamaliza shule mwaka juzi tu lakini ghafla bin vu anatokea kuwa tajiri wa kutisha. Hapa lazima tuanze kuhoji wote kuanzia zama za mzee Ruksa ili kuwatendea wachovu haki. Haiwezekani tukaendelea kuhubiriwa na watawala kuwa wana nia ya kupambana na ufisadi wakati wakiwafumbia macho mafisadi na wezi kama hawa wanaotumia ofisi za umma kujineemesha na kuhujumu kaya. Mie nawajua mia kidogo; na niko tayari kuwataja ili washughulikiwe vilivyo.”
            Msomi Mkatatamaa anatia guu “ni kweli; mali za wizi na waliojilimbikiza wanajulikana. Hata ndege wanajua zilipo na ni kiasi gani na ni za nani na anafanya kazi ofisi gani. Nadhani kinachowasaidia wezi hawa kuendelea kutuibia na kufaidi mali zetu ni ile hali ya jamii yetu kugeuka ya kuabudia vitu badala ya haki na utu. Wengi wa wezi hawa ni wenzetu, wanetu, ndugu zetu na marafiki zetu. Hata hivyo, kama sirikali ikiendelea kuwadekeza tutakwenda kuzimakamata kama noma na iwe noma; au vipi?”
            Kanji naye hajivungi. Anakwanyua mic “mimi iko sikia vatu nalalamika naonewa sana na Kufuli. Kama nasikia vanalalamika tadhani vameonewa. Sasa kama naibia kaya nategemea ipewe sada ya ua au iweke pango naonja joto ya jiwe kama jusi. Kama nasema Kapenda, unakuta toto dogo bila juzi vovote naanza kazi leo. Keso nakubwa bilionea. Naangusa jengo kuba kuba, natongoza bibi kubakuba, nakula kwa hoteli kubakuba, naendesha gari kubakuba, nahonga toto na malaya gari kubakuba ya bei baya. Hii kama siyo chori napata vapi hii feza nachezea kama jugu?”
            Mheshimiwa Bwege anaamua kula mic “mimi nina mawazo tofauti nanyi. Kwanini tusitunge sheria ya kuwakamata wahusika na kuwanyonga na kurejesha mali zetu ili wezi wengine waogope kama wanavyofanya China. Ukikamatwa umekula njuluku ya kaya China wanakunyongelea mbali bila kujali cheo, chama, dini wala ukaribu wako na wanene kama ilivyo hapa ambapo mmeongelea kashfa ya Bashite ambaye anatuhumiwa kukwanyua njuluku kibao lakini dingi anafanya gozi gozi kumtumbua. Nakubaliana na wanaosema tuwasake hawa wezi. Tukiwakamata tuwafanyie kama vibaka ili kuepuka kupelekwa lupango wakahonga na kurejea Uswazini kumalizia mali zetu huku wakitukoga hata kuwahonga wake zetu.”
            Da Sofia Lion aka Kanungaembe anakula mic “tatizo si kuhonga wake zenu. Tatizo ni  kutuibia na kutenda vitendo vya kishenzi. Hata wangechuma kihalali, hawapaswi kuwahonga wake zetu wala binti zenu. Mbona mnawadhalilisha wanawake; kwani hakuna wanaume wanaoohongwa na hawa hawa wenye nazo yaani mashuga ladies siyo?”
            Mipawa aliyerejea toka Morogoro kumzika mkewe anaamua kula mic “kusema ukweli hali hii ya wachache kuiba mali za umma kwa kutumia ofisi za umma inasikitisha sana. Juzi nilipopata msiba wa mke wangu kipenzi, nilijua maana ya kutokuwa na kitu. Kusafirisha maiti ilikuwa ngoma usipime. Sasa inakuwa uchungu zaidi pale unapoteseka kwa ukapa na ukata wakati kuna majambazi wachache wakiibia kaya yako. Naunga mkono pendekezo la kuwachoma moto mibaka hawa wakubwa. Kwanini tuwe na uwezo wa kuwachoma vibaka tushindwe mibaka tunayoijua na kuishi nayo?”
            Kijiwe kikiwa kinanoga si likapita shangingi la kijana mmoja anayefanya kazi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mzee Mchonga. Acha tumtoe mkuku ili kwenda kumripoti TAKUKURU akanyang’anywe mimali aliyotuibia!
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.
 
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 08:44 No comments:
Newer Posts Older Posts Home
Subscribe to: Comments (Atom)

Cordially and unlimitedly welcome to this blog.


Writing and reading are two different processes but which share the same goal-to educate, communicate and entertain.
It is my pleasure to have you as the guest of this tablet.
I, thus, warmly and always, welcome you to share ideas.
Importantly and eminently, shall there be anything amiss or you think can advance this blog, please donate it.
Allow me to humbly and kindly welcome you once again.
Nkwazi N Mhango- A Man And a Half

When wisdom brings no profit, to be wise is to suffer. Not all thoughts are good and constructive. Others are even worse than bullets. The good thinkers are the ones that think constructively for the manumission of all bin-Adams regardless their diversity. Mwl. Nkwazi N Mhango,
Canada.


Hail Mama SWAPO Nandi-Ndaitwah

Hail Mama SWAPO Nandi-Ndaitwah

I Love My Country Tanzania

I Love My Country Tanzania

The Curse of Salvation

The Curse of Salvation

Gen Z and Internet Revolution

Gen Z and Internet Revolution

I Cry for Ambazonia and Darfur

I Cry for Ambazonia and Darfur

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do.

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do.

Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Yoo-hoo, Africa Is Yowling

Yoo-hoo, Africa Is Yowling

The Story of Stories

The Story of Stories

The Chant of Savant

The Chant of Savant

AFRICA’S CONTEMPORARY FOOD INSECURITY Self-inflicted Wounds through Modern Veni Vidi Vici and Land G

AFRICA’S CONTEMPORARY FOOD INSECURITY Self-inflicted Wounds through Modern Veni Vidi Vici and Land G

AFRICA MUST DEAL WITH BLATS FOR ITS TRUE DECOLONISATION

AFRICA MUST DEAL WITH BLATS FOR ITS TRUE DECOLONISATION

Epistle to Afrophobic South Africa

Epistle to Afrophobic South Africa

Magufulification

Magufulification

BORN NUDE

BORN NUDE

Total Pageviews

Heko Rais Magufuli

Heko Rais Magufuli

DECOLONISING EDUCATION

DECOLONISING EDUCATION

Kudos President Magufuli

Kudos President Magufuli

JOKEY HORSE-JOCKEY NORTH-SOUTH RAPPORT Diagnostic-cum-Prognostic-Academic Perspectives on Who Truly

JOKEY HORSE-JOCKEY NORTH-SOUTH RAPPORT Diagnostic-cum-Prognostic-Academic Perspectives on Who Truly

The Family Friend of Animals

The Family Friend of Animals
Children's Book

Matembezi Mbuga ya Wanyama

Matembezi Mbuga ya Wanyama
Kitabu cha Watoto

Our Heritage

Our Heritage
Children's Book

How Africa Developed Europe:Deconstructing the His-story of Africa, Excavating Untold Truth...

How Africa Developed Europe:Deconstructing the His-story of Africa, Excavating Untold Truth...

Africa's Dependency Syndrome: Can Africa Turn Things around for the Better?

Africa's Dependency Syndrome: Can Africa Turn Things around for the Better?

'Is It Global War on Terror' or Global War on Terra Africana?

'Is It Global War on Terror' or Global War on Terra Africana?

Perpetual Search

Perpetual Search

Africa's Best and Worst Presidents

Africa's Best and Worst Presidents

Psalm of the Oppressed

Psalm of the Oppressed
Psalm of the Oppressed

AFRICA REUNITE or PERISH

AFRICA REUNITE or PERISH
A new approach towards empowering Africa

BORN WITH VOICE

BORN WITH VOICE

Soul on Sale

Soul on Sale

Soul on Sale

Nyuma ya Pazia

Nyuma ya Pazia

We are one

We are one

SAA YA UKOMBOZI

SAA YA UKOMBOZI

Feel at home

You are always welcome to this epistle again and again time after time, ad infinitum.


Most read Posts

  • Sarkozy’s Take on African Fat Cats a Welcome Move
    At last the chicken are coming home to roost! French authorities made a groundbreaking decision by culling three most corrupt African presid...
  • Napanga kuanza kuuza mitumba na si maneno
    Ingawa mimi si mtumba, napanga kuuza mitumba. Nimechoshwa na jamii ya mitumba. Kila kitu mitumba. Mitumba, mitumba mitupu. Siasa za mitumba...
  • Better or Bitter Life for all?
    When I deeply muse on how an arrogant and brutal cabal of hoity toity (Coverted Con Men (CCM)) is tirelessly hoodwinking and dividing the ho...
  • Africa's Becoming more Despotic and Nepotistic
    "King of Kings" Gaddaffi The seven-day 40th anniversary of Libya strongman’s autocratic rule and charade elections in Gabon where...
  • Kuna siku tutataifisha haya mahekalu haki ya nani
    Taarifa kuwa waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alinunua nyumba kwa zaidi ya shilingi bilioni moja licha ya kuwastua wananchi na...
  • Nyangumi mdogo akutwa amekufa ufukweni BC
    Hii ni picha iliyotolewa ya Nyangumi aina ya Humpback ambaye alikumbwa na maji na kutupwa kwenye ufukwe wa bahari ya Pasifiki kwenye eneo l...
  • Kikwete, Charity Begins at Home!
    President Jakaya Kikwete Pea...
  • Kweli binadamu si chochote wala lolote, wamkumbuka huyu?
    Walioko madarakani mkiabudiwa kama miungu au sanamu kumbukeni vijana hawa hata baba zao  ambao maiti zao zinaoza jangwani. Ungewaambia...
  • Pinda kulia hakutoshi, awajibike
    INGAWA kilio cha Waziri Mkuu, Mizengo Peter Kayanza Pinda, kinaonekana kuyeyusha hasira za Watanzania kwa muda, kuna haja ya kudodosa zaidi....
  • Hawa si wachungaji bali ni fisi na mbwa mwitu
    KUMEZUKA mtindo mchafu na wa rejareja wa baadhi ya wachumia tumbo na matapeli kumtania hata kumtumia Mwenyezi Mungu kufanya utapeli na ujamb...

Followers

Blog Archive

  • ►  2025 (84)
    • ►  December (1)
    • ►  November (11)
    • ►  October (9)
    • ►  September (7)
    • ►  August (12)
    • ►  July (8)
    • ►  June (7)
    • ►  May (5)
    • ►  April (4)
    • ►  March (6)
    • ►  February (8)
    • ►  January (6)
  • ►  2024 (92)
    • ►  December (7)
    • ►  November (4)
    • ►  October (11)
    • ►  September (9)
    • ►  August (7)
    • ►  July (9)
    • ►  June (9)
    • ►  May (8)
    • ►  April (7)
    • ►  March (6)
    • ►  February (7)
    • ►  January (8)
  • ►  2023 (118)
    • ►  December (10)
    • ►  November (10)
    • ►  October (9)
    • ►  September (2)
    • ►  August (4)
    • ►  July (6)
    • ►  June (9)
    • ►  May (8)
    • ►  April (18)
    • ►  March (13)
    • ►  February (9)
    • ►  January (20)
  • ►  2022 (208)
    • ►  December (14)
    • ►  November (14)
    • ►  October (20)
    • ►  September (20)
    • ►  August (12)
    • ►  July (25)
    • ►  June (22)
    • ►  May (18)
    • ►  April (13)
    • ►  March (18)
    • ►  February (18)
    • ►  January (14)
  • ►  2021 (323)
    • ►  December (23)
    • ►  November (34)
    • ►  October (26)
    • ►  September (13)
    • ►  August (19)
    • ►  July (21)
    • ►  June (29)
    • ►  May (25)
    • ►  April (23)
    • ►  March (43)
    • ►  February (29)
    • ►  January (38)
  • ►  2020 (290)
    • ►  December (33)
    • ►  November (37)
    • ►  October (28)
    • ►  September (35)
    • ►  August (31)
    • ►  July (26)
    • ►  June (17)
    • ►  May (21)
    • ►  April (18)
    • ►  March (15)
    • ►  February (17)
    • ►  January (12)
  • ►  2019 (160)
    • ►  December (8)
    • ►  November (7)
    • ►  October (12)
    • ►  September (9)
    • ►  August (27)
    • ►  July (18)
    • ►  June (18)
    • ►  May (11)
    • ►  April (11)
    • ►  March (9)
    • ►  February (16)
    • ►  January (14)
  • ►  2018 (162)
    • ►  December (12)
    • ►  November (6)
    • ►  October (13)
    • ►  September (10)
    • ►  August (20)
    • ►  July (9)
    • ►  June (14)
    • ►  May (9)
    • ►  April (16)
    • ►  March (21)
    • ►  February (17)
    • ►  January (15)
  • ▼  2017 (306)
    • ►  December (20)
    • ►  November (23)
    • ►  October (20)
    • ►  September (26)
    • ►  August (31)
    • ►  July (31)
    • ►  June (34)
    • ▼  May (26)
      • Forgery is boil but not goosebumps
      • Magufuli: Mwalimu wa maendeleo Afrika?
      • Kijiwe kwenda ikulu kumpongeza rais
      • Magufuli Amtumbua Kamishina Mkuu wa Polisi
      • Graves, Magufuli, mineral sands and Muhongo
      • Makaburi, makinikia, Magufuli na Muhongo
      • Eti Dom ni the big city of Bongo? Wow!
      • Wiki hii nimekumbuka Botswana baada ya Tanzania ku...
      • Leave Tanzania out of Kenya’s upcoming election
      • Nani anakumbuka mauji ya kipumbavu kama ya Mvumi?
      • Kijiwe kukamata mali za mafisadi
      • Handcuffed President: Fall from Grace
      • Kuuawa Lowassa na Magufuli Gwajima achunguzwe
      • Fisi anapochunga kondoo wa Bwana
      • Is Trump’s move an accidental suicide?
      • Magufuli asipuuzie shutuma za Kenya dhidi yake
      • Kijiwe: Wachunaji Wachague Dini au Siasa
      • TPSF mnamuonea Magufuli bure
      • Njaa Inapopanda Kichwani PhD Hugeuka Bullshit
      • Mwakyembe Kukalia Ripoti ya Clouds Ni Kujidhalilisha
      • Kijiwe Chataka Vyeti Vya Wanasiasa Vihakikiwe Pia
      • Vyuo vya kitapeli vifutwe haraka
      • Baada ya kutemwa kwa kughushi: Mlevi kuvamia siasa
      • This Clip Will Offend Anybody That Knew and Loved ...
      • Kughushi: Viongozi wa umma wachunguzwe
      • Kijiwe chastukia zoezi la kuhakiki vyeti vya kibas...
    • ►  April (24)
    • ►  March (20)
    • ►  February (28)
    • ►  January (23)
  • ►  2016 (269)
    • ►  December (22)
    • ►  November (21)
    • ►  October (22)
    • ►  September (15)
    • ►  August (12)
    • ►  July (27)
    • ►  June (24)
    • ►  May (23)
    • ►  April (29)
    • ►  March (26)
    • ►  February (27)
    • ►  January (21)
  • ►  2015 (399)
    • ►  December (34)
    • ►  November (24)
    • ►  October (22)
    • ►  September (34)
    • ►  August (29)
    • ►  July (37)
    • ►  June (22)
    • ►  May (32)
    • ►  April (35)
    • ►  March (46)
    • ►  February (47)
    • ►  January (37)
  • ►  2014 (502)
    • ►  December (47)
    • ►  November (49)
    • ►  October (47)
    • ►  September (37)
    • ►  August (40)
    • ►  July (42)
    • ►  June (30)
    • ►  May (35)
    • ►  April (47)
    • ►  March (44)
    • ►  February (39)
    • ►  January (45)
  • ►  2013 (399)
    • ►  December (37)
    • ►  November (27)
    • ►  October (31)
    • ►  September (26)
    • ►  August (33)
    • ►  July (39)
    • ►  June (28)
    • ►  May (40)
    • ►  April (44)
    • ►  March (39)
    • ►  February (26)
    • ►  January (29)
  • ►  2012 (597)
    • ►  December (27)
    • ►  November (26)
    • ►  October (27)
    • ►  September (30)
    • ►  August (47)
    • ►  July (94)
    • ►  June (86)
    • ►  May (119)
    • ►  April (83)
    • ►  March (23)
    • ►  February (17)
    • ►  January (18)
  • ►  2011 (261)
    • ►  December (20)
    • ►  November (19)
    • ►  October (20)
    • ►  September (21)
    • ►  August (27)
    • ►  July (12)
    • ►  June (15)
    • ►  May (20)
    • ►  April (27)
    • ►  March (32)
    • ►  February (24)
    • ►  January (24)
  • ►  2010 (205)
    • ►  December (25)
    • ►  November (23)
    • ►  October (23)
    • ►  September (23)
    • ►  August (17)
    • ►  July (13)
    • ►  June (12)
    • ►  May (10)
    • ►  April (18)
    • ►  March (9)
    • ►  February (16)
    • ►  January (16)
  • ►  2009 (163)
    • ►  December (19)
    • ►  November (14)
    • ►  October (11)
    • ►  September (6)
    • ►  August (12)
    • ►  July (9)
    • ►  June (11)
    • ►  May (20)
    • ►  April (22)
    • ►  March (14)
    • ►  February (12)
    • ►  January (13)
  • ►  2008 (191)
    • ►  December (12)
    • ►  November (11)
    • ►  October (14)
    • ►  September (15)
    • ►  August (16)
    • ►  July (23)
    • ►  June (10)
    • ►  May (19)
    • ►  April (16)
    • ►  March (19)
    • ►  February (17)
    • ►  January (19)
  • ►  2007 (33)
    • ►  December (13)
    • ►  November (20)

About Me

My photo
View my complete profile

Travel theme. Powered by Blogger.