The Chant of Savant

Tuesday 4 September 2012

Wajue First ladies wa hovyo na waroho Afrika


janet_mus...Tanzania First Lady Salma Kikwete has been active in the areas of public health and ecotourism. Her husband Jakaya was elected chairman of the AU in January of 2008.
Nafasi ya mke wa rais au first lady huwa ni ya kuheshimiwa ikizingatiwa kuwa ni nafasi pekee ya kuwa karibu, kumshauri, kumliwaza na kumtunza kiongozi wa nchi. Zaidi ya hapo first lady hapaswi kujiingiza kwenye shughuli nyingine. Huu ndiyo utaratibu na utamaduni unaofuatwa na kukublika dunia nzima. Kinyume na hapa ni utaratibu wa hovyo, tamaa na ujinga ulioanza kujengeka kwenye nchi chache zinazoongozwa kifisadi ambapo first ladies wamegeuka wanasiasa na wafanya biashara uchwara. Kwa mfano kwa sasa katika Afrika kuna first ladies wanne wa hovyo ambao ni  Patience Johathan (Nigeria) ambaye hivi karibuni ameteuliwa na gavana wa jimbo la kwao kuwa msaidizi wake ukiachia mbali kuwahi kukamatwa uwanja wa ndege mjini Lagos kuhusiana na utoroshaji wa pesa nje. Mwingine ni Janet Museveni (Uganda)  mhudumu wa zamani wa ndege ambaye licha ya kuwa mbunge ni waziri katika serikali ya mumewe. Mwingine ni mwalimu wa shule ya msingi mwenye elimu ndogo Salma Kikwete (Tanzania) ambaye anajihusisha na biashara ya NGO ukiachia mbali hivi karibuni kutoa mpya kugombea ujumbe wa CCM wa mkoa wa Lindi. Wa mwisho ni  mke wa waziri mkuu wa Ethiopia aliyefariki, Azeb Mesfin ambaye pia ni mbunge na mtuhumiwa wa ufisadi anayeitwa Queen of Mega au Queen of Mega corruption. Wanawake hawa wameonyesha kuwa na tamaa na wasio na uwezo wa kuona mbali hasa baada ya waume zao kuachia madaraka. Je Afrika tunaanza kujenga kizazi kipya cha wanawake wa marais wanaofuja madaraka ya waume zao kama tulivyoshuhdia kwa first ladies kama Lucy Kibaki (Kenya), Anna Mkapa (Tanzania) na Agatha Habyalimana (Rwanda)?

2 comments:

Anonymous said...

Tuandikie kwa english kama kiswahili kinakupa taabuu.

Yasinta Ngonyani said...

Wananchi wamelala na wao wanakula mali hii ndivyo ilivyo sio kwamba wanajiingiza kwa kuwa viongozi wa kweli hapana bali ni kuchuma mali ndo maana inaenda kifamilia. Nje ya mada kidogo:- Usiye na jina hapo juu sijaona sehemu ya kiswahili hapa inaleta matata.