Tuesday, 12 March 2013

'Gongo' yaua 51 Libya

Moutassim Gaddafi aka Hanbal akikata ulabu huko ulaya zama za utawala wa baba yake.
Taarifa zilizokariri shirika la habari la Uingereza BBC zimeeleza kuwa jumla watu 51 nchini Libya wamepoteza maisha kutokana na kunywa pombe haramu. Ripoti zimesema kuwa walibya wengi hunywa pombe kwa siri kutokana na sheria kuzuia kunywa pombe nchini humo. Hivyo watu wenye tamaa ya pesa hutengeneza pombe kienyeji majumbani mwao na kuwauzia wanywaji. Zaidi ya watu 300 wameathiriwa na unywaji wa pombe haramu. Hii si mara ya kwanza kwa Libya kukumbwa na kashfa ya unywaji pombe. Baada ya kuangushwa kwa imla wa nchi hiyo, Muamar Gaddafi hapo mwaka jana, kulifichuka kashfa ya unywaji pombe za bei mbaya uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watoto wa Gaddafi. Kwa habari zaidi GONGA HAPA.

No comments: