Monday, 11 March 2013

Ng'eee ng'eee ng'eee ndivyo nilivyozaliwa!


Mwaka 1965 tarehe kama ya leo, nilikuja duniani. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuwa niliye. Nachukua fursa hii lau kujipongeza kwa kuanza kuifikia miaka 50. Ni siku yangu ya kuzaliwa. Nashukuru nimezaa, nimelea na naendelea na maisha kwa furaha, uchangamfu na dhamira. Hakika ni siku ya furaha kwangu familia yangu na marafiki zangu. Ni bahati mbaya kuwa wazazi wangu wote walishatoweka. Hawapo leo kuniona ninavyoendelea na maisha. Hata hivyo wapo waliochukua nafasi yao--- wanetu.

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa na hasa kutimiza miaka 50 Mwenyezi Mungu ashukuruwe sana ..

NN Mhango said...

Shurani da Yacinta ingawa sijatimiza miaka 50. Natimiza miaka 48. Mungu akubariki nawe na familia yako pia.

Yasinta Ngonyani said...

Oh! samahani nilisoma vibaya kumbe umeandika unakaribia kuifia miaka 50 na sio leo..hahahaaa naona nahitaji miwani...HONGERA TENA KWA KUTIMIZA MIAKA 48..KEKI HIYO USININYIMA NIRUSHIE NA MIMI...lol

Jaribu said...

Happy Birthday Ndugu Mhango! Utimize na miaka mingi mingine!

NN Mhango said...

Nawashukuru Jaribu na da Yacinta. Keki da Yacinta umepata. Chukua umma uhomole hapo hapo. Jaribu, kama ada, nakushuru ndugu yangu. Maana hata kama hatujawahi kuonana, tushakuwa ndugu. Nadhani kwa sasa Texas mnakula upepo kwa sana huku mkipata na jibini toka kwa ma-cowboys and cowgirls.
MBARIKIWE NYOTE nami nawatakieni heri na uhai mrefu na wenye neema, furaha na mafanikio.

Anonymous said...

Heri ya siku yako ya kuzaliwa. Ubarikiwe wewe na familia yako pia uendelee kutuelimisha kwa njia hii hapa jamvini kwako.

By Mfuatiliaji Makini

NN Mhango said...

Mfuatiliaji Makini nakushuru kwa dua zako. Kadhalika nakutakia maisha mema na umri vya kutosha na kukupa furaha na ridhiko la moyo.

Jaribu said...

Amen, Mhango! Tumetulia Texas ingawa macowboys na cowgirls wanatokea siku za sherehe tu. Umenifurahisha hapo kwa sababu nilipokwenda Uholanzi nilifikiri watu wengi watakuwa wanavaa makubazi ya mbao; kumbe siyo!

jessica hamissi said...

hapi bathi day bwana kaka. maulana, akujalie maisha marefu yenye furaha na fanaka, akujaze ujazike, na usiache kumcha mola wako siku zote ili akupe mioungo mingine minne


happy birthday and many more to come

NN Mhango said...

Asante sana bi Jessica nawe Mungu akujalie maisha marefu na furaha na fanaka. Vipi mahajimati huko?