Monday, 4 March 2013

Ukitaka kumtapeli Kikwete msifie au mtetee

Jakaya Kikwete juu na Sarah Hermitage chini ambao wametokea kulumbana juu ya ufisadi.Hermitage Blogger Wins $1.9 Million Against Tanzanian Media Tycoon, Reginald Mengi
Vyombo vya habari viliripoti kuwa taasisi ya mfukoni iitwayo  Human Settlement of Tanzania (Huseta), inapanga kufanya maandamano ya kumlaani raia wa Uingereza Sarah Hermitage kwa kumkashifu rais Jakaya Kikwete na Tanzania alipoongelea ukweli kuhusu ufisadi.
Matapeli hao wamepata mwanya wa kujiweka karibu na Kikwete kama ilivyo ada ili awalipe fadhila. Hii ni baada ya kugundua kuwa Kikwete ni mpenda sifa na mlipa fadhili hata kama ni kwa mambo ya hovyo. Kilichowasukuma kumtetea Kikwete utadhani wanalipwa kwa kazi hiyo ni kauli za mama huyu. Moja ya kauli yake alikaririwa akisema, "Mahakama za Tanzania zimejaa rushwa na hazina uwezo. Rais ndiye msimamizi wa katiba na yeye ndiye mhusika mkuu wa ukiukwaji wa sheria." Je huu ni uongo? Mahakama inawezaje kuwa na uwezo wakati baadhi ya majaji waliotajwa kwa majina ni vihiyo au mafisadi na watoa rushwa wanahudumu kwenye mahakama? Kwani mahakama ya Tanzania ni huru? 
Kauli nyingine waliyokariri Huseta iliyotolewa na Hermitage inasema, "Kikwete aitaka PCCB (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) kupambana na rushwa hadi katika Baraza la mawaziri,’kundi moja la majambazi linaliambia kundi jingine la majambazi kukamata mwizi." Je huu ni uongo? Takukuru ni huru? Mbona ni Takukuru hii hii iliyotaka kumsafisha rafiki na mshirika mkuu wa Kikwete katika utawala na ufisadi Edward Lowassa kabla ya bunge kumkuta na hatia na kumlazimisha kuachia ngazi.Ukitaka kujua kuwa Takukuru ni majambazi wanaopamba rushwa badala ya kupambana nayo itisha uchunguzi juu ya mali za maofisa wake. Ukitaka kujua Takukuru si huru rejea kukiri na kulalamika kwa mkurugenzi wake Edward Hosea alikowahi kufanya kwa balozi mmoja wa kigeni na baadaye kukanusha baada ya vyombo vya habari kuripoti ukweli huu. Je kwa sasa Tanzania kuna taasisi inayoweza kuaminika zaidi ya kila taasisi kuwaibia walipa kodi? Jiulize ni kwanini nchi yenye raslimali na utajiri kama Tanzani ainakuwa maskini hadi kuzidiwa na viinchi kama Kenya na Rwanda kama huu ni uongo.
Kwa vile Kikwete ni msanii anayewatapeli watanzania, nao wanajua jinsi ya kumtapeli. Utawasikia wakisema wanaandaa sara ya kumuombea yeye na taifa na upuuzi mwingine. Kwa vile ni mpenda sifa na huruma, naye huuingia mkenge.
Kweli ni rahisi kumtapeli Kikwete. Ningekuwa Kikwete ningejitetea mwenyewe badala ya kuruhusu matapeli kunitumia kama sina akili.

government fed by the peopleKesho tutasikia maandamano ya kulaani aliyechora katuni hii. Tuache ushenzi nchi yetu imeharibiwa na utawala wa Mkapa na Kikwete kwa kuendekeza maslahi binafsi.

No comments: