Sunday, 25 January 2015

Kikwete sijui ni kupenda misiba, misifa, uzururaji, ugonjwa au ujinga?

unnamed1jk
Alipokufa baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere sikuona wala kusikia ujumbe toka Saudia. Rais Jakaya Kikwete sijui kwa kujikomba au kwa uhusiano wa siri eti ameunguza mafuta kwenda kuhani msiba. Kama alikuwa anamthamini sana mfalme Abdullah si angehudhuria mazishi ambayo nayo nijuavyo sijui kama angeruhusiwa kuhudhuria hasa ikizingatiwa kuwa wenzetu wanazika kirahisi na si kwa ushaufu kama waswahili maskini. Kikwete amebaki na miezi michache kuondoka madarakani bila kufanya kazi yoyote isipokuwa kuwatetea mafisadi na kuzurura. Heri amalize muda wake lau nchi ipumue kutokana na kuwa na rais asiyekaa ofisini wala mwenye kutumia busara katika maamuzi na matendo yake.

No comments: