The Chant of Savant

Saturday 31 January 2015

Vasco da Gama anapokula buku!

Jamaa anasoma au mkwara na kutaka apigwe picha? Kwa wanaomjua huyu jamaa, hakuna kitu asichopenda kama kusoma. Hata kabla ya kuwa rais alisifika kwenda kwenye kumbi za muziki na mambo mengine kama hayo. Alijua kukaa kwenye vijiwe vya mpira na kusogoa zaidi ya kujisomea hata kujiendeleza.  Ukitaka kujua hofu inatoka wapi, jiulize swali rahisi. Mbona walio karibu naye wote hakuna anayesoma isipokuwa yeye? Kitu kingine, angalia wingi wa walaji alioandamana nao. Hao ni wale wanaoweza kupewa viti. Bado wapiga picha uchwara na wasaka sifa ambao wamegeuka fisi  wasiobanduka kila alipo simba. Fedha ya umma inafujwa kwenye upuuzi kama huu kila uchao. 

No comments: