Saturday, 3 January 2015

Ridhiwani: Wazazi walimpa kura anawapa watoto ndizi!

Ridhiwani Kikwete mbunge wa Chalinze akigawa ndizi kijini Kwa Msanja
Picha nyingine ukizitazama zinasikitisha na kuchochea hasira. Ukiangalia mtoto wa rais Ridhiwani Kikwete mbunge wa Chalinze anavyonunua ndizi na kuwagawia watoto kwenye kijiji cha Kwa Msanja unahoji hata huo usomi wake na uwezo wa kufikiri. Hata wanaoweka picha kwenye mitandao wanaonyesha kutojua wanachofanya sawa na walivyoweka picha ya baba yake na mama yake wa kambo wakibembea kule Jamaica wasijue ingezua mambo. Sijui kwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri unapata picha gani kwenye picha hii ambapo mbunge licha ya kushuhudia shule iliyoporomoka kuwapa ndizi watoto badala ya kalamu na madaftari au hata ahadi ya kujenga shule yao? Hawa ndiyo viongozi wetu watokanao na kurithishana madaraka tena wanaotaka eti wapewe nchi kwa vile ni vijana. Tunaambiwa huyu ana Master kwenye sheria. Mbona fikra na matendo yake havionyeshi hili?
Pamoja na kwamba wakazi wa vijiji wana njaa, kama inavyoonyesha, kuwapa watoto ndizi ni hongo ya kipuuzi. Je ndizi za siku moja zitaondoa njaa ya siku zote ukiachia mbali ujinga wa kudumu?

No comments: