Sunday, 20 March 2011

January Makamba mnafiki au mtafuta umaarufu?


Kwa mtu aliyesikia mawazo ya January Makamba mbunge wa Bumbuli (CCM) ambaye ni mtoto wa katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba anashangaa. Ametoa video yake akiwalaumu baba zake chini ya kile alichokiita "Letter to my Fathers".
Wachambuzi wengi wanashangaa kwanini ametumia neno fathers badala ya kuwataja hao anaowalenga kama kweli si mwoga au mtafuta sifa? Isitoshe, anawalaumu hao baba zake kwa unazi na unafiki wakati yeye akiufanya kwa kutetea Dowans.
Ajabu anasikika akilaani kubadili mitaala, demokrasia ya majaribio, huduma mbovu, watu kupenda ukwasi wakati yeye ni tunda la uchafu huu!
Anasikika akiongea kizalendo wakati moyoni ni msaliti na fisadi wa kawaida. Je analenga kuwanasa watanzania wamuone kama mkombozi wakati ni mtoto wa fisadi tu? Je watanzania wataingia mkenge huu? Najua January hana ubavu wa kunijibu lau kwa kutoa maoni hapa. Nimeishawasiliana naye bila majibu. Je January kapata huu ufunuo lini?
Je January Makamba anatafuta mtaji wa kisiasa baada ya kugundua baba yake anaishiwa na kuzidi kuzama au ni mbabaishaji na msanii wa kawaida? Je January si tunda la ufisadi? Mtoto wa nyoka ni nyoka.Je bado January anaendelea na ulevi ule ule wa kudhani watanzania ni mataahira? Kwanini asijiondoe CCM kama kweli anadhamiria anachosema na kusema anachodhamiria?
Kusikia ufufuo wake
, Bonyeza hapa

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kama ulivyosema mtoto wa nyoka ni nyoka...

NN Mhango said...

Da Yasinta ni kweli. January hata akiongea kwa ndimi hataacha kuwa nyoka.

Anonymous said...

Eti "Wachambuzi wengi wanashangaa..". Hao ni wachambuzi gani? Wote wapo kichwani mwako? Eti "ametoa video kuwalaumu baba zake". Nini? Jamaa amerekodiwa akizungumza kwenye cultural event reading a poem. That was a poem, not a policy speech! Tatizo lako unaamini sana maneno ya mitaani kuhusu January, na ukikutana na ukweli basi kichwa chako kina freeze. The guy is genuine. Hata kama kwa kiasi fulani ni zao la CCM bado wapo wana CCM wengi ambao hawakubaliani na mambo yanavyokwenda hovyo nchini.