Saturday, 12 March 2011

Wajua jiji lenye mabilionea kuliko majiji mengine?


Penye miti hakuna wajenzi. Nani angejua kuwa Moscow ingeipindua New York hata Tokyo na London kwa kuwa na mabilionea? Usishange ikafuatia Dar es Salaam kama wezi wetu wataamua kufichua utajiri wao waliochuma kupitia ufisadi. Hayo ndiyo maajabu ya dunia yetu.Kwa habari zaid, Bofya hapa

3 comments:

Jaribu said...

Ndio shida ya nchi ziliacha ujamaa na kuingilia ubepari kwa nguvu. Mafisadi waliuziwa mashirika ya umma kwa bei poa, ndio inaleta skewed tabaka ambapo kuna matajiri wachache juu, middle class ndogo halafu masikini wengi waliobakia. Ndio maana unakuta wapambe wa JK wakitetea safari zake zisizoisha kuwa kwa mfano, nauli ya kwenda Addis Ababa sio kubwa. Au Waziri Mdogo Nyalandu kusema Watanzania wengi waanze kupanda ndege kwenda mikoani. Swali ni kwamba, wananchi wangapi wanaweza kupanda ndege kwenda Mwanza wakati nauli ya daladala tu ikipanda watu wanalalamika?

NN Mhango said...

Jaribu,
Huyo waziri ni mwendawazimu na limbukeni. Mwambie akawambie wanyaturu wenzake aone watakachomfanyia. Ni mpuuzi aliyepewa madaraka kwa vile anatumika kama nepi kufanya kazi za mafisadi na sasa amejisahau.
Usemayo ni kweli. Watu wametumia ujamaa kutusaliti na kutuchuuza. Mwalimu aliishi kijamaa na kufa kijamaa. Lakini wale waliosoma kutokana na ujamaa huu huu ni mabepali na mabeberu wa kutupwa. Nenda Masaki uone tunavyotawaliwa na watu wenye sura za binadamu lakini roho za fisi na panya.

Anonymous said...

Iweje waliokuwa wajamaa wa kweli few years ago leo ni "wawekezaji" wakubwa kwenye nchi hii?