Saturday, 12 March 2011

Kapayukaji katimiza nusu mwaka

Kapayukaji kanakaribia kumaliza nusu mwaka hata kama hakajapayuka. Hii ni picha yake ya sasa. Tunazidi kumshukuru Mungu azidi kukawezesha kaje kupayuka baadaye na kuchukua mikoba.

12 comments:

Yasinta Ngonyani said...

HONGERA sana shangazio yangu kwa kuyimza nusu mwaka. Mwenyezi Mungu na akulinde uzidi kukua na uwe na afya njema .

Malkiory Matiya said...

Tunamtakia afya njema,sina shaka naye kwa kuridhi mikoba, mwonekano wake pichani ni kielelezo tosha kuwa ni mpiganaji makini.

Malkiory Matiya said...
This comment has been removed by the author.
Malkiory Matiya said...

Napenda nirekebishe neno hapo juu: Kurithi badala ya kuridhi.

Anonymous said...

Naam. Kametulia kapayukaji ketu katarajiwa.

Mcharia said...

Kwanza kula 5, maana hapo utakapoanza utakuwa na speed ya kimbunga sababu njia imeshatengenezwa...wuuu!!!

MwaJ said...

Mwenyezi Mungu ampe afya njema awe mtoto mwenye furaha siku zote.

Napenda sana watoto.

Baraka Mfunguo said...

HONGERA SANA KAPAYUKAJI NA MPAYUKAJI KWA KUWEZA KUMFIKISHA HAPO ALIPO. MAISHA NI HATUA.....

NN Mhango said...

Kwa niaba ya Kapayukaji,familia, nami binafsi nawashukuruni nyote mliotutakia heri na fanaka. Naamini Mungu amesikia dua zenu na atazifanyia kazi.
Kila la heri. Mungu awazidishie.

Mbele said...

Picha nzuri sana na katoto kanaelekea kufanana na baba yake. Kwa huu nusu mwaka kamefikia hapo, ni wazi kanaendelea vizuri. Kila la heri

NN Mhango said...

Asante kaka Mbele kuongeza dua. Ni kweli katoto kanaendelea vizuri maana kananyonya maziwa ya mama na si ma-junk au formulae.
Nazidi kuwashukuru wote mliotutembelea na kutuombea heri na makuzi mema kwa kitoto chetu.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hongera kapayukaji ketu. Kua salama. Harakati za Ukombozi zinakusubiri!