Tuesday, 1 March 2011

Waziri aliyeghushi PhD aachia ngazi Ujerumani

Kikwete na vihiyo wake wasome hii hapa

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Karl-Theodor zu Guttenberg ameachia ngazi baada ya kugundulika kuwa alighushi shahada ya uzamizi. Hii imetokea baada ya wajerumani wapatao 20,000 kumwandikia barua Kansela wa Ujerumani bi Angela Merkel ambaye hakusita kumtaka mhusika kuachia ngazi.

Watuhumiwa wetu wa kughushi kama vile Emanuel Nchimbi, Mary Nagu, Makongoro Mahanga na William Lukuvi bado ni mawaziri. Kwa habari zaidi soma hapa

4 comments:

Anonymous said...

Rais mwenyewe msanii mtupu maneno meeengiii tuuu,washikaji wake ndio majangili makubwa yanayofilisi uchumi wa nchi .sasa kama ameweza ku over look au ku ignore issue nzito kama hizi unafikiria atakuwa na muda wa kuangalia masuala kama haya? dowans imevuma,kagoda na epa wamepeta,mabomu yamelipuka hii ni baadhi ya vijamabo vinavyoendelea hapo home lakini bado yeye ka lay back,sasa anaona fukuto linalotoka kwa umma ukihamisishwa na chadema, analalamika wanavuruga amani,amani na upendo Tanzania ni kuwaaangalia mafisadi yakila nchi na kutumbua raha huku ma low income earnes wanakula rhumba na life ,kula shida ,shule mbinde(mpaka migomo),huduma za afya ubabaishaji,maji safi na salama shida,huku mifumuko ya bei ya maisha inalipuka kila siku kama yale mabomu ya wanajeshi wetu,lakini wataambiwa nyamazeni ili tudumishe amani na upendo.NDIO HAWA VIONGOZI VIHIYO WANAONGOZA NCHI KWA KUTUMIA UJUZI NA UZOEFU WA VIHIYOLAZATION.SASA HAPO UNAFIKIRIA TUTEGEMEE NINI?NDIO KWA MAANA HAKUNA TUTAKALOFANIKWA KWA SABABU HAWA WATU NI UNFITS,HAWANA SIFA NA UWEZO KUONGOZA KWA SABABU HAWANA ELIMU YA KUTOSHA YA KUWEZA KUFANYA KAZI KWA UFANISI!

NN Mhango said...

Anonymous umeaua sina haja ya kuongeza nisiharibu uhondo.Asante kunitembelea na kulonga ukweli mtupu.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hizi PhD za kugushi zinamsaidia nani lakini? Na ukiangalia vizuri, wengine hawana hata haja ya kuzigushi. Je, ni ile faida ya kuitwa Dr au nini? Inashangaza.

NN Mhango said...

Mwl. Masangu usishangae. Huku North America kuitwa Daktari au chochote si big deal kama uswahilini kwetu na baadhi ya nchi za Ulaya. Ujue. Binadamu ni kiumbe dhaifu anayependa utukufu hata kama hastahili. Ni wachache waliokana haya mambo. Huoni rais wako anavyoona fahari kutumia udaktari wa heshima wakati akina Nyerere, Mwinyi na Mkapa hawakufanya hivyo? Hii hutegemea uwezo wa mtu kujua mambo.
Hongera kwa Johari kutimiza ngwe tatu. Nilitaka kubandika kwenye sebule yako baadaye nikasahau.